May 29th, 2010
By Pamoja
Who killed Veneranda? (To watch a video click on the link)
Veneranda, who died at the age of 17, stands as a symbol of all People Living with HIV/AIDS (PLWHA) in Bulongwa/ Makete District/ Tanzania, who were denied state-of-the-art treatment due to the misuse and theft of funds designated for their health care.
The documentary is dedicated to the 70 HIV-patients – many of them activists from the HIV/AIDS self-help group PIUMA (piuma-simba.org) – who died unnecessarily since 2006 due to the lack of decent HIV-care.
If you want to know more about Veneranda and PIUMA, read the article “Veneranda: Struggle of an AIDS-infected orphan” written by the award winning Tanzanian journalist Vicky Ntetema, former bureau chief of the BBC Tanzania, under the following link: pamoja.at/Press_Archives/Veneranda_Struggle_of_an_AIDS-infected_orphan.pdf
Support combating fatal corruption and donate via credit card, PayPal or transfer your donation directly to our account: pamoja.at/support_us.html
You’ll also find more information in our press archives (pamoja.at/press.html) and on our Facebook pages:
facebook.com/home.php?#!/pages/Who-Killed-Veneranda/111468755554168?v=wall&ref=sgm
_ _
This documentary is dedicated to the 70 HIV-patients – many of them activists from the HIV/AIDS self-help group PIUMA – who died unnecessarily since 2006 due to the lack of decent HIV-care. They did not die from AIDS, but from corruption and disrespect for the human rights to life and treatment. “Veneranda: Struggle of an AIDS-infected orphan” written by the award winning journalist Vicky Ntetema, former BBC bureau chief for Tanzania, or search our press archives
PAMOJA - TOGETHER - Association for Intl. Cooperation owns the copyrights for the documentary “Who killed Veneranda?”. Feel free to download, upload and distribute the file for non-commercial use!
Source:http://www.pamoja.at/videos.html
Posted in News | No Comments »
March 31st, 2010
Na Evance Seth.
Kumetokea mabadiliko katika kiwango cha kufaulu kwa wanafunzi tofauti na mwaka uliopita katika shule ya sekondari Iwawa iliyopo wilayani Makete.
Akizungumuza mkuu wa shule hiyo Bw OMATH SANGA amesema jumla ya wanafunzi mia moja kumi na nane waliofanya mtihani wa Taifa, wanafunzi wawili wamepata divisheni one , wanafunzi kumi na tatu wamepata divisheni two na wanafunzi thelathini na saba wamepata divisheni three, wakati wanafunzi wane wamepata divisheni ziro.
Mwalimu OMATH SANGA amesema mpaka sasa hajapata tathimini ya kujua shule yake imepanda kiasi gani au imeshuka kiasi gani kulingana na shule zingine ,na hivyo mwisho amewaomba wananchi kutambua umuhimu wa kuwatafutia nafasi za masomo watoto wao.
Posted in News | No Comments »
March 31st, 2010
Na Evance Seth
Katika uwanja wa Luvanyina uliopo kata ya Bulongwa , kumefanyika mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu kati ya shule ya sekondari ya mwakavuta na shule ya sekondari kipagalo.
Kwani shule hizo zimekutana ikiwa mwakavuta sekondari ni kongwe ilianza mwaka 1992 na Kipagalo ilanza mwaka 2007.
Mchezo huo ulianza mnamo muda wa saa kumi kamili alasili na mchezo huo uliendeshwa na refarii Bw Timu Sanga. Mnamo dakika ya kumi na mbili Kipagalo walianza kuandika goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wao Noah Sanga huku Mwakavuta wakiwa hawajapata kitu, mpira uliendelea huku mwakavuta wakiendelea kushambuliwa na dakika ya thelathini na saba Kipagalo walifunga goli la pili kupitia kwa mshambuliaji wao Juma Nsemwa , hadi mpira unakwenda mapumziko Kipagalo mbili na Mwakavuta sifuri.
Kipindi cha pili kilianza kwa nguvu sana pande zote mbili, huku Mwakavuta Sekondari wakishambulia kwa nguvu sana goli la Kipagalo na dakika ya hamsini na nne mwakavuta wafunga goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wao Partson Mbogela na dakika ya sitini na tisa Mwakavuta walifunga goli la pili kupitia kwa mchezaji wao Frank Fungo lililo fungwa kwa njia ya faulo , na Mwakavuta walizidi kuliandama goli la Kipagalo huku kipagalo wakizidi kuchoka , mnamo dakika ya themanini na tatu mwakavuta walifunga goli la tatu kupitia kwa mchezaji wao Regi Sanga na dakika ya tisini na mbili za nyongeza mwakavuta walifunga goli la nne kupitia kwa mchezaji wao yuleyule Frank Fungo hadi mpira unamalizika Mwakavuta Sekondari nne na Kipagalo Sekondari mbili.
Mwalimu wa michezo wa shule ya Sekondari ya Kipagalo alisema kwamba nimekubali matokeo kwani mpira wa miguu una matokeo ya aina tatu kufunga , kufungwa na kutoa sale , naye mwalimu wa Mwakavuta sekondari alisema kwamba nimefurahi sana na ushindi kwani kipindi cha kwanza tulitangulizwa goli mbili bila nilipata tabu kwani kwa sasa nina jiandaa wiki ijayo kuwapeleka vijana wangu kucheza na shule ya Sekondari Ipelele.
Posted in News | No Comments »
March 31st, 2010
Na Evance Seth.
Akisoma taarifa ya shamba hilo kwa mkuu wa mkoa wa Iringa MH MOHAMEDI ABDILAZIZI mwakilishi wa shamba hilo amesema lengo la shamba hilo ni kuongeza ng’ombe wazalishaji pamoja na kufufua zaidi ya hekta hamsini za malisho kwa kutoa magugu na kuweka mbolea.
Amesema kwa kufanya hivyo utaboresha uzalishaji mkubwa wa kiwanda hicho kwa upande wa ulaji wa ng’ombe wenye afya na uzito wa kutosha punde unapofika wakati wa kuuzwa. Amesema mbali na hatua hiyo pia shamba lina mpango wa kuongeza ng’ombe katika kundi la ukamilishaji kufikia ng’ombe mia mbili ili kupata ndama bora kwa ajili ya kusambaza kwa wakulima.
Malengo mengine ni kuboresha upatikanaji wa maji hasa wakati wa kiangazi pamoja na kutengeneza njia za ndani ya shamba hili zipitike wakati wote na kumalisha ukarabati wa nyumba za watumishi pamoja na kuendelea kuingiza umeme kwenye nyumba za watumishi.
Posted in News | 2 Comments »
March 31st, 2010
Na Evance Seth.
Katika wilaya ya makete Tarafa ya Bulongwa na Magoma kata ya Ipelele na kata ya Kipagalo kumetokea na hasara kubwa itokanayo na mvua.
Viongozi wa tarafa zote mbili wakimweleza mwenyekiti wa Halmashauri wa wilaya ya makete Mh Ona Skunara Nkwama walisema wiki hii mvua kubwa sana imenyesha ikiambatana na upepo mkali imesababisha maafa ya nyumba za wananchi pamoja na shule moja ya msingi kuezuriwa.
Mwenyekiti wa halmashauri wa wilaya wa makete alifika sehemu zote za matukio na kutoa pole kwa wananchi wa tarafa zote mbili na kuahidi kutoa mchango wa bati kila nyumba .
Na wananchi walimshukuru mwenyekiti wa halmashauri na kusema tunamshukuru mungu kwani hakuna aliyepata jeraha wala kufa. Na mwisho mwenyekiti huyo aliwaambia wananchi hao kuwa mvua zinapo nyesha wazazi tujitahidi kuwa nyumbani kwenye familia zetu kwa ajili ya msaada endapo linatokea swala kama hili kwani mvua bado zinaendelea kunyesha.
Posted in News | No Comments »
March 31st, 2010
Na Evance Seth.
Imefahamika kuto jipenda kwa baadhi ya akina mama na kutokuwa na ubunifu wa miradi ndio sababisho kubwa kuwafanya wanaume kuleta visa katika ndoa zao.
Wakichangia dondoo za maisha katika kipindi cha mtazamo cha Kitulo FM Redio , baadhi ya wachangiaji hao wamesema matatizo hayo katika ndoa yanasababishwa na wanawake wenyewe kwa kukosa ubunifu katika ndoa zao.
Aidha wamesema wakati mwingine baadhi ya wanawake hujisahau mara wanapokuwa ndani ya ndoa zao pamoja na kuacha kuboresha usafi katika familia zao. Pia imeonekana baadhi ya akina baba wamekosa elimu ya ndoa pamoja na uvumilivu.
Kipindi cha mtanzamo hurushwa kila jumatatu na ijumaa kuanzia saa tatu kamili asubuhi mpaka saa saba kamili mchana katika studio za KITULO FM RADIO.
Posted in News | No Comments »
March 31st, 2010
Na Evance Seth
Katika kata ya Iniho wamejipatia Josho kwa ajili ya kuogeshea ng’ombe. Afisa mifugo wa kata ya hiyo Bw. Nova alisema kwamba tumepata josho hili kwa malengo ya kuogeshea ng’ombe ili kuua wadudu kama kupe na nk.
Pia alisema josho hili ni letu sisi wenyewe kinachotakiwa kila mwananchi mwenye ng’ombe anapokuja kuogesha atalipia shilinngi mia moja kwa kila ng’ombe na hizo fedha zitafanya kazi ya kutengenezea josho pale linapo halibika na kununulia dawa za kuogeshea ng’ombe.
Na mwisho alisema kuwa itapangwa ratiba ya kuogesha ng’ombe kwa vijiji kwani kwa mwezi ni mara moja na kwa yule ambaye ataonekana ajaogesha ng’ombe atachukuliwa hatua ya kisheria
Posted in News | No Comments »
February 26th, 2010
Na Evance Seth.
Makarani na wasimamizi wa SENSA ya mifugo wamepatiwa mafunzo yatakayo wawezesha kupima mpango mzima wa kuondoa kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa mwaka 2009/2010.
Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika wilaya ya Makete kaimu katibu tawala wa mkoa wa Iringa Bw. Adam Swai amesema mwaka 2008 mpango wa sekta ya kilimo kwa pato la taifa kulikuwa ni asilimia 25.8, kati ya asilimia hiyo ya kilimo cha mazao kilichangia asilimia 19 huku mifugo ikichangia asilimia 4.7.
Kwa upande Meneja takwimu mkoa wa Iringa amesema sense hiyo hufanyika kila baada ya miaka mitano na kwamba katika mafunzo hayo watachagua wakulima kumi , kutoka katika mafunzo hayo watachagua wakulima kumi na tano kutokana na vigezo vilivyowekwa vya wakulima bora katika kila wilaya .
Posted in News | No Comments »
February 26th, 2010
Na Evance Seth.
Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa UMA inakusudia kuwa watumishi wa serikari kuanza kupokea mishahara dirishani badara ya kuwaingizia katika akaunti zao.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa Nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa uma Mh. Hawa Ghasia alipokuwa akiwahutubia watumishi wa halmashauri ya wilaya ya makete. Alisema ofisi yake inafikilia kufanya hivyo kutokana na kulipa mishara hewa ya watumishi.
Mpango huo wa watumishi kupokea dirishani utasaidia kuondoa udanganyifu ambao serikari inalipa mishahara hewa na kusababisha serikari hasara kubwa. Amesema katika kupitia utafiti uliofanywa na wizara yake imebaini katika sekta ya afya na sekta ya elimu baadhi ya watumishi wanalipwa mishahara hewa.
Mh. Ghasia alikuwa katika ziara yake ya kutoa semina kwa halmashauri ya wilaya ya makete inyohusu mabadiliko mahali pa kazi na utawala bora ambapo hii leo akitoka hapa anaelekea wilayani Ludewa.
Mikoa mingine ambayo amepitia kutoa semina hiyo ni MANYARA, KIGOMA, LINDI, MTWARA, PWANI , IRINGA na akimalizia SINGIDA.
Posted in News | 1 Comment »
February 26th, 2010
Na Evance Seth.
Katika Wilaya ya Makete kata ya Iniho kumefanyika chanjo ya watu wazima kuanzia miaka mitano na kuendelea.
Chanjo hiyo ilikuwa ni agizo la serikari kuwa kila mwananchi anatakiwa kupata chanjo ilimradi ana miaka kuanzia mitano. Chanjo hiyo alihudumia Bw. Tigrath Sanga toka kata ya Iniho kwani ndiye aliye pata mafunzo hayo.
Bw. Tigrath kabla ya kuanza kuhudumia alitoa maelezo kwa ufupi kwa wananchi wa wake kuwa, chanjo hii ni ya vidonge na alisema maana ya chanjo hii ni ya kuzuia magonjwa nyemelezi pamoja na kuua minyoo mwilini, alitoa mfano mmoja wa magonjwa nyemelezi kama kuvimba matezi.
Alisema chanjo hii hawaruhusiwi watoto wadogo kupata kwani vidonge hivi vina nguvu sana mwilini vinapo fanya kazi , na alisema upatapo chanjo hii huruhusiwi kutumia kinywaji cha aina ya kileo kwa siku uliyopata chanjo.
Posted in News | No Comments »