Tuesday, July 8th, 2008

PIUMA KUHUDHURIA MKUTANO WA TANGO- MBEYA

PIUMA   imewakilisha   ASASI  zote ambazo si  za kiserikali za wilaya ya makete  katika mkutano  wa  TANGO .MKUTANO  huo uliambatana  na  mafunzo  kwa waliohudhulia , mafunzo  kwa  ujumla yalikuwa ni kuzijengea  ASASI  uwezo  wa kushiriki katika  mambo mbalimbali  yanayo  fanyika   katika  Halmashauri ,  moja   ya mada  ambazo  zilifundishwa  zilikuwa  ni  pamoja  kushiriki katika kupisha  bajeti ya halmashauri  , kushiriki katika kufanya tathimini   ya huduma    za  jamii   katika  wilaya, Hivyo  basi  kwa   mafunzo  hayo  PIUMA  ina nafasi ya kupeleka   wajumbe   wawili   katika  kamati ya kufanya tathimini  ya huduma   za jamii  wilani  makete  ,wajumbe  hao  wata  ambatana na wajumbe wengine   ambao nao walipata  mafunzo haya.   Kamati  imejumuisha  madiwani, wataalamu toka  halmashauri, wajumbe toka  asasi mbalimbali, pamoja na watu  raia toka kwenye vituo ,Hata hivyo  katika mkoa wa  Iringa    Mjumbe  kutoka   PIUMA  ndiye alipendekezwa  na asasi   za  mkoa huo  kuhojiwa  na waandishi   wa  hahari  ili kuelezea matatizo  ambayo asasi  zinayapata huko kwenye maeneo yao.

                                   Kwa pamoja    tutashinda.

Leave a Reply