POTANIA MFUSE
Nesi wa PIUMA Potania Mfuse ameshakifa kazini, tayari kwa kuja kuanza kazi rasmi.
Nesi huyu amefika tarehe 14/07/2008 mnamo saa 10:00 jioni kwenye ofisi ya PIUMA.
Tarehe 15/07/2008 alipumzika, siku iliyofuata Afisa Mtendaji, Mwenyekiti na Mtunza hazina walienda kumwonyesha nyumba waliko mtafutia jirani na kituo cha VCT cha PIUMA.
Nyumba hiyo inapatikana Mtaa wa Ilamba kitongoji cha Ilamba, makubaliano na mama mwenye nyumba kuhusu malipo kwa chumba kimoja ni shilingi elfu tatu (3000) na yeye amechukua vyumba vyumba vitatu kufuatana na familia aliyonayo, watoto watatu.
Nyumba hiyo ina maji ya bomba na maji hayo huwa hayatoki mara kwa mara hivyo atalazimika kwenda kisimani kuteka maji pia ina umeme.
Pamoja na hayo kwa mara ya kwanza mwenye nyumba alidhani shirika litamsaidia kumlipia hivyo alipanga bei kubwa ya shilingi elfu kumi kwa chumba kimoja, kwa vyumba vitatu ingekuwa shilingi thelathini elfu, lakini uongozi wa PIUMA ulioongozana nae ulijaribu kutetea kuhusu bei kubwa hiyo kuwa ipunguzwe kwani si shirika litakalomlipia bali ni yeyemwenyewe.
Tarehe 17/7/2008 uongozi wa PIUMA na nesi wataongozana kwenda kwa mwenye nyumba kuandikiana mkataba kuhusu malipo ya elfu kumi kwa vyumba vitatu kila mwezi.
kwa habari zaidi tutaendelea kuzipata.

Jaackson says:
Hi PIUMA
It is very nice reading from your web. I Support you and give you FIVE for the good work you are undertaking to ensure that the pride and integrety of your personality is observed and respected.
Congratulations to Potania Mfuse for taking a lead role in demanding for the right to better, affordable health. There are few Tanzanian of her courage that will volunteer and take such risk, I salute her spirit of volunteerism.
MATUMAINI DAIMA - KWA PAMOJA TUTASHINDA