IDADI YA WANACHAMA PIUMA INAZIDI KUONGEZEKA.
Mpaka sasa PIUMA ina jumla ya wanachama 174. Haya yalikuwa ni mazungumzo kati ya LUBANO KYANDO NA WITNESS NGUMBA, witness akimhoji mwanachama huyu ambaye anakuja kujiunga na PIUMA
Mazungumzo yetu yalikuwa kama ifuatavyo.
LUBANO KYANDO ni mwananchi wa kijiji cha Ikovokovo, ana umri wa miaka 52, ameoa na ana mtoto mmoja. mwananchi huyu yeye ametaka kujiunga na shirika la watu wanaoishi na VVU PIUMA.
Kwa nini ameamua kuja kujiunga na PIUMA na ni kitu gani kimemshawishi kujiunga na kikundi hiki cha PIUMA?
Lubano Kyando alisema kuwa, amevutiwa na ushirikiano wa wanachama wa PIUMA, hawanyanyapaani, kutokana na huduma zitolewazo na shirika hili kama Huduma ya HBC, Mobile VCT na dawa za magonjwa nyemelezi kutolewa bure kwa wanachama wa PIUMA na huduma mbalimbali.
Je tangu upimwe kuna mabadiliko yeyote ya afya yako?
Lubano alisema kuwa tangu apime aliendelea kuchukua dawa za ARV lakini hakuona mabadiliko ya afya yake, aliomba kuchunguzwa zaidi afya yake lakini aliambiwa kuwa vipimo vinalipiwa, kwa kuwa alikuwa hana fedha za kulipia aliamua kwenda kuchunguzwa zaidi katika Hospitali ya Wilaya Makete, huko ndiko alikogundulika kuwa alikuwa na matatizo kwenye mapafu. Hapo ndipo alipopewa huduma ya kupewa dawa, aliambiwa kuwa akaendelee kunywa endapo kama kutakuwa na mabadiliko/tatizo lolote arudi tena Hospitali. Lakini alisema kuwa tangu hapo afya yake iliendelea kuwa nzuri na mpaka sasa anaendelea vizuri.
Je unaionaje huduma ya Bulongwa Hospitali?
Lubano alisema kuwa huduma inayotolewa Bulongwa Hospitali hajaridhika nayo (mbovu) kwa sababu mtu akiwa anaumwa anapewa dawa za kunywa bila kuchukuliwa vipimo na ukiwauliza utaambiwa kaendelee kunywa vipimo utachukuliwa siku nyingine.
Mwisho alisema kuwa isingekuwa Hospitali ya Wilaya Makete angelikuwa alishakufa muda mrefu.


Royal Orr says:
I really like this interview format, especially with the picture.
My Kiswahili can’t follow the she conversation very well, but it’s great to have a sense of some of the people behind the scenes with PIUMA!
Looking forward to more.