KIKUNDI CHA AMANI UNYANGALA
Kikundi cha Amani Unyangala ni kikundi ambacho ni cha wanachama wanaoishi na VVU, kina jumla ya wanachama 23, kikundi hiki kimeungana na vijiji vifuatavyo, UNYANGALA, UTENGULE NA KILANJI.Kikundi hiki kilianzishwa rasmi tarehe 27/12/2007.
Nikiongea na Daudi Luvanda ambaye ni Mwenyekiti wa kikundi hiki, kwa nini mmeamua kuunda kikundi hiki.
Daudi alisema kuwa tumeunda kikundi hiki ili tuwe tunasaidiana mawazo mbalimbali na kufarijiana pia. Kazi tunazozifanya katika kikundi hiki ni; Tulianza kuchanga fedha na kukopeshana sisi wenyewe, na tumepanga kila mwezi tunapokutana tunarejesha fedha na riba yake na tunakopeshana tena.
Mpaka sasa tuna jumla y a sh. 100,000/=, na tuna miradi ya Kuku, Nguruwe na Mradi wa shamba la ngano. Hii ni miradi ambayo tunayompaka sasa ingawa kwenye matarajio yetu tunategemea kuwa na miradi ya Ng’ombe wa Maziwa, mabwawa ya samaki na bustani mbalimbali.

