Friday, August 22nd, 2008

PIUMA KAZINI!

 

Hii ilikuwa jana tarehe 21/08/08. wakati wanachama wa PIUMA walipokusanyika kwa pamoja kujaza udongo katika jengo lao lililopo mtaa wa Ilamba.

 

Shughuri hiyo iliyoongozwa vema na kamati ya ujenzi ilianza mnamo saa nne asubuhi na kukamilika saa saba mchana.

 

Ingawa idadi ya wanachama ilikuwa ndogo,kutokana na wengi wao kuwa na ratiba nyingine za maendeleo katika vijiji vyao,lakini kazi iliyofanyika huwezi amini!

Kweli ‘’imara kama simba’’

Akiongea baada ya kazi Makamu katibu aliwashukuru wanachama wote kwa moyo wao wa kujitolea na kufanya kazi kama siafu!’’Hii ndio PIUMA bwana ‘’ alimalizia katibu.

 

 

kazi kweli ilifanyika!
kazi kweli ilifanyika!

 Baada ya kazi wametulia!

 Picha,matukio.wanachama wa PIUMA wakiwa shughulini katika jengo lao.

 

 

 

 

 

Juma.

3 Responses to “PIUMA KAZINI!”


  1. Royal Orr says:

    Wonderful pictures! Thanks for the update and good luck to the building team -PIUMA House is a great accomplishment.


  2. Jaackson says:

    Taifa Litajengwa na Wenye Moyo, na wenye moyo ni akina Markus, Mzee Alwisye Kasukari, Akina mama wa Unyangala, M/Kiti Kabuyu, Mzee Daudi, Mlinzi Herode, Apollo Mbogela, Mzee wa Busara Willbard na wengine ambao sijawataja lakini mnaonekana katika picha kwa pamoja mnaitwa PIUMA.

    Nawapa pongezi kwa moyo wa kizalendo na kiushujaa, mmeonyesha kuwa kuishi na VVU sio mwisho wa matumaini, sio mwisho wa kutafuta Maendeleo. Hongera mzidi kutia bidii, tuje tuonanane siku moja tukiwa na mafanikio ya kutosha,

    Nene Nedekile


  3. Royal Orr says:

    I like this site a lot - every time I return, seeing the PIUMA activists gives me a lift. Give us more - we’re looking for reasons to celebrate your efforts. KWA PAMOJA TUTASHINDA!

Leave a Reply