PIUMA waongeza Utaalam zaidi kwenye upimaji
Mganga wa PIUMA, Juma Nzige leo hii ameanza mafunzo ya wiki tatu kwa ajili ya ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya UKIMWI mjini Dar Es Salaam.
Mafunzo hayo ambayo yanatolewa na Africa Medical Research Foundation (AMREF) Tawi la Tanzania yanalenga kuwapa ujuzi na utaalam washauri nasaa na wapimaji.
Akiongea na tovuti hii katibu mkuu wa PIUMA, Anna Mwinuka amesema Mafunzo haya ni muhimu sana kwa PIUMA ili kuweza kwenda na wakati katika utoaji huduma kwa wateja wake. “Nia yetu ni kutoa huduma iliyobora na ya gharama na nafuu kwa wahitaji kwa wakati muafaka” alimalizia Mwinuka.
PIUMA shirika lisilo kuwa la kiserikali linaendesha kliniki inayotembea (Mobile Clinic) katika eneo la utoaji ushauri nasaha na upimaji wa Virusi vya UKIMWI wilayani Makete. Kupitia wataalam wake wawili na wanachama wanaoishi na virusi vya UKIMWI shirika hili limeweza kuwafikia wakulima wengi ambao wanashindwa kufika katika vituo vya Ushauri nasaha na upimaji.
Potania Mfuse, Muuguzi Mkunga, Mshauri na Mpimaji wa Virusi vya UKIMWI anayefanya kazi na PIUMA anasema PIUMA pamoja na klinik inayotembea pia inaendesha huduma hizi na kuratibu huduma ya wagonjwa majumbani kupitia kituo chake cha HIMA Bulongwa. Potania Mfuse alishapata Mafunzo yake kupitia AMREF pia.
Mafunzo ya Bwana Juma yanagharamiwa kwa kiasi na AMREF – Austria, Shirika lisilo kuwa la Kiserikali la EAWM - Austria na PIUMA.
Wakati wa kampeni ya “Tanzania Bila UKIMWI Inawezekana” iliyokuwa imezinduliwa na Mheshimiwa Rais. J. Kikwete, PIUMA kupitia klinik yake waliweza kuwafikia watu zaidi ya elfu Mbili. Na kuwa ni NGO ya kwanza ya watu wanoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania kufanikisha lengo la kupima bila bajeti ya Serikali.
Mafunzo ya Juma yataongeza tija na ufanisi wa kazi kwa shirika na wateja wake pia. Wanachama wengi wa PIUMA ambao walihojiwa na mwandishi wa habari hizi walisema mafunzo haya yamekuja wakati muafaka wakati kuna uhitaji mkubwa wa huduma hii kwa wananchi .
Wahitaji wa huduma ya Ushauri nasaha na Upimaji wilayani Makete wameshindwa kupata huduma hii kutoka na umbali wa vituo vya Ushuri nasaha na Upimaji. Kliniki inayotembea imekuwa nis suruhisho la tatizo hili. “Tukiwafuata vijijini huko waliko, huwa wanajitokeza wengi na huwa hatuna uwezo wa kupima wakaisha kwa siku moja” alimazia maelezo katibu wa PIUMA Anna Mwinuka.
Witness Ngumba


Royal Orr says:
Great to see the site being used so effectively. Thanks to Juma and Witness for this.
Jackson Ngumba says:
PIUMA mnafanya kazi nzuri sana nawapa pongezi. nimesikia furaha sana kutembelea website yenu…nadhani niseme yetu kwa kuwa inanihusu.
sina nia ya kupinga maoni ya waliotangulia kuboresha huduma ni mhimu sana endelea kufanya hivyo.
Natamani sana nione picha zaidi za huko makete tena zikiwa na maelezo ya maeneo chini yake ili tujue locations zilikopiga.
Asanteni
Jackson Ngumba
Witness Ngumba na mimi naita Jackson Ngumba wa hukohuko makete lakini naishi Dar es Salaam (0719 087878)…. hapo sasa..!!! halafu hatujuani?