Wednesday, October 15th, 2008

PIUMA MOBILE VCT KIJIJINI IMEHE.

 

Tarehe 10/10/2008 PIUMA tulikuwa kwenye Upimaji wa Virusi vya UKIMWI kijijini  Imehe, kijiji hiki kina umbali wa Kilomita  18, kwenda na kurudi zinakuwa kilomita 36, ambapo kilomita moja ni sh. 1500.

 

Tulipokelewa na Mtendaji wa kijiji, na baadhi ya wananchi walikuwa wameshafika tayari  kwa ajili ya kupima, Mtendaji wa kijiji alimkaribisha Mkuu wa msafara Katibu Mkuu wa PIUMA,  Anna Mwinuka kwa ajili ya kutambulisha msafara wake alioongozana nao na kuendelea na zoezi zima lililowaleta.

 

Akiongea na tovuti hii katibu mkuu wa PIUMA, Anna Mwinuka alitambulisha msafara aliokuwa ameongozana nao, walikuwa watu wafuatao, Nesi kutoka Ofisi ya DMO Makete, KABELEGE, Nesi wa PIUMA POTANIA MFUSE na  Mwanachama wa PIUMA Apolo Mbogela.

 

Aliwaeleza wananchi kuwa lengo la kuja kijijini hapa tumekuja kutoa ushauri Nasaha na Upimaji wa Virusi vya UKIMWI kwa hiari , alisema kuwa ukisha pima na ukajua Afya yako, kama unamaambukizi utashauriwa jinsi ya kuishi na kuzuia maambukizi mapya, endapo hutapatikana na maambukizi utashauriwa jinsi ya kujikinga na maambukizi, alisema Katibu Mkuu wa PIUMA.

 

Upimaji ulianza saa 5:00 asubuhi mpaka saa 10:30 jioni, wakati upimaji unaendelea Katibu wa PIUMA alitoa ushuhuda wake jinsi alivyopata maambukizi, alisema kuwa tangu agundulike kuwa ana maambukizi ya VVU mpaka sasa  ana miaka 3 na mpaka sasa hasumbuliwa na ugonjwa mwingine wala hatumii dawa zingine zaidi ya ARV.

 

Upimaji huo ulikuwa ni rika tofauti, walikuwepo watoto na watu wazima.

 

Watoto waliopima walikuwa 25, Me 11 na Ke14  katika kundi hili hakuna aliyeonekana na maambukizi ya VVU.

 

Watu wazima waliopima walikuwa 61, Me 24 na Ke 37, wenye maambukizi walikuwa watu 7, Me 3 na Ke 4, wasiokuwa na maambukizi walikuwa watu 54.

 

Jumla ya watu wote waliopima walikuwa 86.

 

Upimaji vijijini unasaidia sana kwa watu ambao wako mbali na Vituo vya huduma kama hii kwa sababu watu wengi wanakata tamaa  kutokana na umbali wa vituo vinavyotoa huduma hii, hivyo tunavyowatembelea vijijini ndipo tunapata watu wengi zaidi , alisema katibu wa PIUMA Anna.

 

Witness.

 

 

4 Responses to “PIUMA MOBILE VCT KIJIJINI IMEHE.”


  1. Jackson says:

    Kazi Nzuri,


  2. Royal Orr says:

    Great work! Keep it up and please continue to keep us informed of all these impressive, essential efforts.


  3. Gottfried Mernyi says:

    Hongera sana !

    Dear PIUMA-Team,

    I am very pleased and grateful to learn about your efforts.

    Please submit my warmest regards to all people involved !

    Yours

    Gottfried Mernyi, Austria


  4. Rogers Silva says:

    htlz9ove6v8so53b

Leave a Reply