Wednesday, October 22nd, 2008

PIUMA MOBILE VCT UGANGA.

Tarehe 16/10/2008 PIUMA tulikuwa kwenye Upimaji wa Virusi vya UKIMWI kijijini  Uganga, kijiji hiki kina umbali wa Kilomita  25, kwenda na kurudi zinakuwa kilomita 50, ambapo kilomita moja ni sh. 1500.

 

Tulipokelewa na Mtendaji wa kijiji, na baadhi ya wananchi walikuwa wameshafika tayari  kwa ajili ya kupima, Mtendaji wa kijiji alimkaribisha Mkuu wa msafara Katibu Mkuu wa PIUMA,  Anna Mwinuka kwa ajili ya kutambulisha msafara wake alioongozana nao na kuendelea na zoezi zima lililowaleta.

Katibu mkuu wa PIUMA, Anna Mwinuka alitambulisha msafara aliokuwa ameongozana nao, walikuwa watu wafuatao, Nesi kutoka Ofisi ya DMO Makete, KABELEGE, Nesi wa PIUMA POTANIA MFUSE, Mwanachama wa PIUMA Apolo Mbogela na Bwana afya wa Bulongwa  FYAVANGO.

 

Aliwaeleza wananchi kuwa lengo la kuja kijijini hapa tumekuja kutoa ushauri Nasaha na Upimaji wa Virusi vya UKIMWI kwa hiari , alisema kuwa ukisha pima na ukajua Afya yako, kama unamaambukizi utashauriwa jinsi ya kuishi na kuzuia maambukizi mapya, endapo hutapatikana na maambukizi utashauriwa jinsi ya kujikinga na maambukizi, alisema Katibu Mkuu wa PIUMA.

 

Aliwaeleza wananchi kuwa mwaka jana tulikuwa tunakuja kupima na Jackson Mbogela na Mary Musoma ambao kwa sasa sio wafanyakazi wa PIUMA tena, lakini pamoja na kuondoka kwao PIUMA haijafa bado inaendelea.

 

Upimaji ulianza saa 4:00 asubuhi mpaka saa 10:30 jioni, wakati upimaji unaendelea Katibu wa PIUMA alitoa ushuhuda wake jinsi alivyopata maambukizi, alisema kuwa tangu agundulike kuwa ana maambukizi ya VVU mpaka sasa  ana miaka 3 na mpaka sasa hasumbuliwa na ugonjwa mwingine wala hatumii dawa zingine zaidi ya ARV.

 

 

Jumla ya watu waliopima walikuwa 46, Me 20 na Ke 26, wenye maambukizi walikuwa 3 na niwanaume tu, wasio na maambukizi walikuwa 43

 

Idadi hii ilikuwa sio sawa na ya mwaka jana, kwani mwaka jana tulipima watu wengi na wengi wao waliokuwa wamepima   wanatumia dawa tayari.

 

 

Baada ya kumaliza upimaji Mtendaji wa kijiji aliwashukuru wahudumu wa PIUMA kwa ajili ya kuwaletea huduma hadi kijijini kwao na kusema kuwa kijiji chetu kiko mbali sana na vituo afya, hali hii imesababisha kuwapoteza ndugu zetu wengi sana, alisema mtendaji wa kijiji hicho.

 

Katibu Anna Mwinuka akitoa ushuhuda

Wananchi wakisubiri kupima.

Witness.

 

 

5 Responses to “PIUMA MOBILE VCT UGANGA.”


  1. Jackson says:

    Many People are in need of the service and they will be able to access the service is delivered in their villages. Hongera PIUMA 4 showinh a way!


  2. Royal Orr says:

    Impressive work! Congratulations to the team at PIUMA.


  3. Dr. Rainer Brandl, MD says:

    I am pleased to see that you are going on testing people and I hope one day you will succeed to get them sevrices free of chruch and government thefts who made a businees out of your plight instead of delivering and helping you.

    You can help yourselves

    Your Doctor

    Rainer


  4. Gottfried Mernyi says:

    Congratulations - hongera sana


  5. Asifiwe Malila says:

    Achievement needs strong fighters,you are real fighters,keep it up.

Leave a Reply