EAWM VOLUTEER IN MAKETE DISTRICT!
WAGENI TOKA EAWM WAWASILI PIUMA-MAKETE
Wanachama wa PIUMA wiki hii wamepokea ugeni kutoka EAWM. Wageni hawa ambao walikuja kwa usafiri wa Basi la Mwafrika siku ya Ijumaa mnamo saa 10:00 jioni.
Walishukia eneo la Namanga Bulongwa , walipofika katika enelo hilo walikuta kamati ya Utendaji ya PIUMA kwa niaba ya wanachama wa PIUMA wakiwasubiri kwa ajili ya kuwapokea.
Baada ya kushuka hapo walipokelewa kwa shangwe na vigelegele na kamati hiyo, wageni hao walifurahi sana kuwaona wanachama hao wakiwa na rufaha kwa ajili ya ujio wao.
Akielezea kufurahishwa kwao na ujio huo, Mwenyekiti wa PIUMA Bwana Kabuyu Kyando aliwaeleza wageni kuwa ‘’ tulikuwa tunawasubiri kwa hamu sana, tulifikiri hatutakuja kuwaona tena, lakini tunamshukuru Mungu aliyetupa uhai na kuwawezesha katika safari yao tumeweza kuonana nao tena. KARIBUNI SANA WAGENI MJISIKIE MKO NYUMBANI”
Wageni walishukuru kwa mapokezi yao mazuri na kusema kuwa nao wamefurahi sana kuja kuonana nao tena, na wanapenda kuonana na wanachama wote wa PIUMA , Mwenyekiti aliwaeleza kuwa hilo lisiwape shida watakutana nao, utaitishwa mkutano wa wanachama wote wa PIUMA.
Katibu Mkuu wa PIUMA Anna Mwinuka aliwapokea wageni kwa kutumbuiza nyimbo mbalimbali za PIUMA kwa kucheza na kuimba pamoja na wageni hao, na baada yapo aliwaeleza wageni kuwa hawa ndio baadhi ya wajumbe wa kamati ya Utendaji na aliwaomba wajumbe hao kujitambulisha kila mmoja, baada ya utambulisho, alimkaribisha Juma Nzige mganga wa PIUMA ili akaribishe msafara wa ugeni huo ambao yeye ameupokea DSM.
Wageni hao walikuwa ni FABIAN WIRNSPERGER na WOLFGANG RAUSCH wote wakiwa wametokea EAWM.
Wageni hawa walisema kuwa wana Muda wa Mwezi mmoja wa kukaa huku kwa ajili ya kufanya kazi na wanachama wa PIUMA.
Habari ndio hiyo!
STORY BY WITNESS!




wolfgang says:
safi kabisa!!
Royal Orr says:
Great to see you made it safe and sound! Good luck to you with your work with PIUMA and congratulations to Witness for her reporting. Keep it up!!