Monday, December 1st, 2008

SHUKRANI ACTION MEDEOR KWA MSAADA WA DAWA PIUMA.

 

Shirika lisilo la kiserikali  la Pima Uishi kwa Matumaini – PIUMA,  wiki hiii limepokea msaada wa madawa kutoka kwa Action Medeor.

Katika barua yao ya shukrani kwa mkurugenzi wa Action Medeor, wanachama wa PIUMA wamesema mchango huo umekuja wakati muafaka na wakati amabo msaada kama huu unahitajika sana.

Action medeor lenye makao yake makuu nchini Ujerumani limetoa ruzuku ya madawa kwa PIUMA kwa ajili ya mgonjwa nyemelezi, vitendanishi kwa jili ya kupimia VVU, Kinga na utendaji kazi wa ini.

Wanachama waliohojiwa na tovuti hii, walisema msaada wa action medeor ni wa ni muhimu kufuatia kupanda kwa gharama za matibabu na pia iliwapunguzia usumbufu wa kufuata dawa katika vituo vya afya vilivyo mbali na makao yao.

Akifafanunua matumizi ya dawa hizo, Mganga wa PIUMA Bw. Juma Nzige alisema masaada huu utawanufaisha watu wote wanaoishi na VVU wilayani Makete.  “wagonjwa wengi wameshindwa kufika hopitali kwa ajili ya matibabu wakiogopa gharama za matibabu, lakini sasa wataweza kupatiwa huduma ya dawa bure na hii itaboresha afya zao zaidi” alizidi kusema Bw. Nzige.

PIUMA wamekuwa wakiendesha huduma ya Upimaji na ushauri nasaha na huduma ya Kutunza  wagonjwa majumbani. Kupitia kituo chao cha tiba HIMA wamekuwa wakiwapa wagonjwa wa UKIMWI dawa baridi bure.

 

 

 

Wanachama wa PIUMA wakikaiziwa dawa

Wanachama wa PIUMA wakikabiziwa dawa

 

 

Witness.

 

 

 

Leave a Reply