MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA PIUMA.
Tunashushukuru kwa misaada ya wafadhili na marafiki wote wa PIUMA kwa michango yenu mnayotoa kwa ajili ya kuisaidia PIUMA kwa mambo mbalimbali.
Mpaka sasa jengo letu la PIUMA lenye vyumba Tisa, vyumba vilivyoisha kusakafiwa ni saba na veranda imesakafiwa nusu, Vyumba vlilvyofungwa milango ni vyumba vine.
Mahitaji ya kuendeleza Ujenzi wa jengo la PIUMA.
- Mifuko 25 ya sementi kwa ajili ya kuendelea na kusakafia.
- Kufakafia vyumba viwili na kumalizia veranda
- Kokoto trip 2
- Mchanga trip 2
- Kufunga fremu na Milango ya vyumba vitano.
- Malipo kwa ajili ya fundi wa kujenga
Tunahitaji msaada wa fedha kwa ajili ya kuendelea na ujenzi, kumalizia kusakafia vyumba vilivyobaki, kufunga milango, kupiga dari, kuingiza umeme na maji.
“Kamati ya Ujenzi ilisema” Pamoja na nguvu kazi zetu wanachama bado tunahitaji msaada wa fedha kwa ajili ya kuweza kukamilisha jengo hili.
Jengo letu likiisha tutahamisha ofisi zote zitakuwa ndani ya jengo letu, kwani majengo yote tunayotumia kwa ajili ya ofisi na kituo cha VCT tumepanga na tunalipia gharama kubwa sana, hii inatuumiza sana sisi wanaPIUMA ”kamati ilisema”
Reported by Witness.




Royal Orr says:
Thanks for the update Witness!
Gottfried Mernyi says:
thank you for the information. Good luck for further efforts !
Asifiwe Malila says:
PIUMA progress is a challenge to anybody who is serious. Wishing you all the best.