KAPUMZIKE SALAMA VENERANDA.
Veneranda Sanga aliyekuwa na umri 17, alikuwa yatima hana baba wala mama na alikuwa anaishi na VVU, mtoto huyu amekuwa akiugua mara kwa mara. Mpaka mara ya mwisho ameenda kufia Hospitali ya Ikonda tarehe 28/02/2009 mnamo saa moja na nusu jioni. Akiwa anauguzwa na Katibu wa PIUMA Anna Mwinuka.
Katibu Anna Mwinuka alieleza kwa kifupi hali ya mgonjwa kwa dakika za mwisho ilivyokuwa; Mgonjwa alipofika Ikonda aliwekewa drip. Baada ya kuhudumiwa na madaktari wa Ikonda, Katibu alimuacha na Mganga na kwenda kufuata chakula cha mgonjwa, baada ya kurudi alichukua chakula na kumlisha mgonjwa, mgonjwa alikula chakula kidogo na hali yake kubadilika ghafla, Katibu alimwita mganga na kumweleza hali ilivyotokea, mganga alimchoma mgonjwa sindano mbili kwa wakati mmoja, baada ya hapo akatulia kidogo,Katibu alipewa chai na mganga wa zamu nusu kikombe na kunywesha mgonjwa, baada ya nusu saa kupita, mganga alikuja tena wodini kumwangalia mgonjwa anaendeleaje, ndipo alipomwuliza mgonjwa kuwa anataka kula chakula gani, mgonjwa alimjibu kuwa hataki chakula chochote lakini alipoulizwa na Katibu kwa kumbembeleza alisema anataka kula maandazi, Katibu alikimbia kwenda kumnunulia maandazi, aliporudi alimpa andazi moja akawa anakula pekee yake lile andazi hakumaliza, alikula nusu, mgonjwa akamwomba Katibu amgeuze wawe wanatazamana na Katibu, Katibu alimgeuza na kumlaza vizuri, akaomba kufunikwa blanketi, alipofunikwa aliomba kushusha kitanda kichwani kwake na katibu alimshusha, baada ya hapo ndipo alipobadilika tena hali, Katibu alikimbia kumwita daktari, alipokuja Mganga alimwuliza katibu kimetokea nini? Katibu alimjibu mganga kuwa hali imejirudia ya mara ya kwanza, Mganga huyo alimpigia simu mganga aliyempokea mgonjwa wakati anafika, na kumweleza hali halisi ya mgonjwa inavyoendelea, Yule mganga aliyempokea mgonjwa alifika wodini haraka kuangalia hali ya mgonjwa, alipofika aliona mgonjwa yuko dakika za mwisho ndio anakata roho, walijitahidi kumhudumia na kumsaidia lakini ilishindikana. Katibu aliwauliza madaktari kuwa ni ugonjwa gani uliomuuwa Vene, daktari alisema kuwa alikuwa na ugojwa wa Uti wa Mgongo ndio uliomuua na kifo hiki kimetokana na kuchelewa kupata matibabu. Ndipo maiti ilipotolewa wodini na kupelekwa Mochwari.
Ndipo tulipofanya mawasiliano na ndugu wa marehemu kwa kupitia mwanachama wa Iniho Wilbadi Sanga awaambie ndugu wa marehemu kuwa amefariki kwa hiyo tunakuja na maiti kwao Iniho, na kufanya mawasiliano na Mkuu wa Sekondari Bulongwa.
Baada ya hapo tulimwomba Wilbadi Sanga aanze kufanya mpango wa Jeneza na kuchimba Kaburi.
Baada ya hapo katibu alianza kuwataarifa wafanyakazi wenzake ofisini kuwa Vene Kafariki. Mganga wa PIUMA aliondoka usiku huo huo kwenda Yatima kutoa taarifa juu ya marehemu huyu. Mkuu wa kituo yatima aliwasiliana na wafanyakazi wenzake na kusema kuwa maiti ya Vene inatakiwa kupelekwa kwao Iniho. Asubuhi ya tarehe 1/3/2009 ndipo mganga wa PIUMA alipowasiliana na Mepos kuomba gari yake itupeleke kuchukua maiti Ikonda. Tulipofika Ikonda mganga wa PIUMA alikutana na madaktari wa pale na kuwauliza hali ya marehemu ilivyokuwa, baada ya waganga walisema tumwone mlinzi wa zamu ili atupeleke mochwari, kulipofika huko tulimchukua marehemu na kuondoka nae.
Tulipofika Namaganga tulikutana walimu wa Sekondari ya Bulongwa na Mwl. Yohana Pilla wakitusubiri kwa ajili ya kuongozana nao kwenda kumsindikiza marehemu.
Tulipofika Amani tulikutana na gari la Yatima ambalo ndani yake kulikuwa na Mkuu wa kituo cha yatima , msaidizi wake, Wema Sanga, na baadhi ya watu wachache.
Tuliondoka pale mpaka kwa o Iniho, tulipofika kule tuliwakuta wananchi wa kule na ndugu wa marehemu , baada ya kushusha maiti tulianza kufanya mpango wa mazishi, ila kwa bahati mbaya kaburi lilikuwa bado halijachimbwa wala jeneza kutengenezwa .
Ndipo tuliposhirikiana na wanachi wa kule pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Bulongwa kuweza kufanya kazi hizi.
Baada ya kumaliza kuchimba kaburi pamoja na kutengeneza jeneza , ndipo maiti ilipochukuliwa na kupelekwa Kanisani kwa ajili ya Ibada na mazishi.
Tulipofika Kanisani mchungaji aliendesha Ibada ya mazishi kama kawaida, na kutoa nafasi za salamu na rambirambi, Mchungaji alianza kwa kumkaribisha Mkuu wa Jimbo Bulongwa ambaye tuliongozana nae ili aanze kutoa salamu, Mkuu wa jimbo aliwashukuru PIUMA kwa kazi kubwa iliyofanyika kwa ajili ya kuokoa uhai wa marehemu, na kusema kuwa siku yake ilikuwa imefika ndio maana amefariki. Aliendelea pia kuwashukuru Kituo cha yatima kwani ndio waliokuwa wanakaa nao kwa muda mrefu na kuwashukuru Bulongwa Sekondari , na kuwapa pole kwa wote walioguswa na msiba huu.
Baada hapo alifuata Mkuu wa Sekondari Bulongwa kutoa salamu, yeye alisema kuwa anasikitika kwa msiba huu kwani mtoto huyu alikuwa mcheshi na wenzake na alikuwa mtulivu shuleni, alisema kuwa wametoa chakula kama sehemu ya rambirambi na bahasha ya fedha.
Baada ya hapo alifuata Katibu wa PIUMA, katibu alisema kuwa sisi kama PIUMA harakati yetu ni kuokoa uhai wa mtu sio kutoa rambirambi wakati mgonjwa amefariki, tulichokifanya sisi PIUMA ni kukodi gari la kumpeleka Hospitali Ikonda na kumrudisha, kutengeneza jeneza na kununua sanda ya kumzikia marehemu, aliendelea kusema kuwa kuondokewa na marehemu huyu ni pigo kubwa kwa PIUMA kwa ni marehemu huyu alikuwa ni mwanachama mwenzetu na tulikuwa tunashirikiana nae katika kutoa elimu ya janga la UKIMWI kwa jamii. Mwisho aliishukuru shule ya Sekondari, kituo cha yatima pamoja na jamii nzima kwa ushirikiaona wao.
Baada ya hapo alifuata mkuu wa kituo yatima; yeye alisema kuwa kwa niaba ya watoto wote wa yatima pamoja na wafanyakazi wenzake wanasikitishwa sana na msiba huu, pamoja na kuwa mtoto huyu alikuwa anaumwa mara kwa mara, mwisho alisema kuwa wao wamekuja kumsindikiza marehemu.
Baada ya Mwl. Yohana Pilla kwa niaba ya wanachama na walimu wa shule ya msingi pamoja na watu wote waliopima na kutumia ARV, yeye alitoa ushauri kuwa kwa wale waliopima na wanatumia dawa wanatakiwa kufuata masharti wanayoambiwa na madaktari wao.
Baada ya hapo walimalizia ndugu wa marehemu , wao walikuwa hawana neno ila waliwashukuru wate waliokuwa wanamhudumia marehemu huyu pamoja na waliofika pale
Mwisho mchungaji aliwashukuru wajumbe wote waliootoa salamu pamoja na rambirambi na kuwaomba wananchi kubeba jeneza kulipeleka kwenye kaburi kwa ajili ya mazishi.
Vene alizikwa mnamo saa kumi na nusu jioni. Baada ya kuzika watu walitawanyika kurudi msibani na wengine kwao.
MUNGU AILAZE PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU.
Akiwa Hospitali Ikonda
Kutoka kwa ndugu yake kuelekea Kanisani!
Katibu Mkuu wa PIUMA akitoa historia fupi ya marehemu
Wanafunzi wenzake wakimwimba nyimbo.
Baada ya mazishi
Witness.






Dr. Rainer Brandl, MD says:
KWA KWELI: KUPUMZIKE SALAMA VENE!
I hope that nobody will die again in future as NOBODY NEEDS to die from HIV/AIDS. Nobody, especially not someone who is on care and treatmetn for 3 years.
Provided ressources and skills are used in the right way!
PIUMA imara kama Simba!
Royal Orr says:
Deepest sympathies and condolences to Veneranda’s friends and family in Makete.
All of us who met her are outraged that she received such poor treatment at the hands of local health authorities. Her life is a shocking testament to the hollowness of government promises to care for its people.
Thanks to Ikonda Consolata Hospital for trying, too late, to save her life when she was finally transferred there for care.
More on Veneranda, her life, her death and her funeral can be found at the website http://www.highlandshope.com
Mmaka Sanga says:
RIP Veneranda.
Kapumzike salama, Veneranda. Wewe ni Malaika sasa, kama vile ulivokuwa Malaika hapa duniani.
malila says:
SIKUTEGEMEA VENERANDA SANGA KUWA ANGEKUFA,ILIKUWA NI NOVEMBA 2008 NILIPOONANA NAYE BULONGWA.SIWEZI KUSEMA CHO CHOTE ZAIDI YA KUWASHUKURU WOTE WALIOPIGANA KIUME KUJARIBU KUOKOA MAISHA YA VEN.
VEN AMEKWENDA KUPUMZIKA KTK NYUMBA YA MILELE,TULIOBAKI TUSHIKAMANE NA KUPAMBANA BILA KUKOMA.
Jackson says:
She was an insipiration to hundreads of young Angles in the Hills, RIP Ven.
Nidekila
Olivia says:
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana ni barikiwe. Amen