Thursday, March 26th, 2009

Elimu ni haki ya watoto wetu!

  PIUMA imeendelea kuwapa kipaumbele watoto wa wanachama wake katika suala zima la elimu ya sekondari,hivi karibuni watoto wawili  wa wanachama wataendelea na mpango huo wa kupata elimu  mkoani Iringa.wakiwa na na nyuso za furaha watoto hao (pichani),wameahidi kusoma kwa bidii ili waweze kubadili maisha yao na jamii kwa ujumla.

 

 

Mwaka 2007 PIUMA iliamua kuwaunga mkono watu wanaoishi na VVU kwa kutoa nafasi za watoto wawili wa wanachama wa PIUMA watakaosomeshwa na yeye kuanzia kidato cha kwanza mpaka watakapoishia.

 

Kwa hiyo ili kupata watoto wawili kwa ajili ya kwenda kusoma huko PIUMA iliamua kufanya utaratibu wa kutunga mtihani ambao utafanywa na watoto wa wanaPIUMA waliomaliza darasa la saba kwa mwaka huo. Na kamati ya utendaji ilikubaliana kuwa kila mtoto atakayeongoza kwa wavulana atachukuliwa na mtoto atakayeongoza kwa wasichana atachukuliwa.

 

Kwa hiyo mitihani hiyo itakuwa inatungwa kila mwaka mara baada ya watoto hao kumaliza darasa la saba, na kufanya mtihani mwingine ili tuweze kupata watoto wawili tu.

 

Mwaka 2008 walipelekwa watoto wawili wa wanachama wa PIUMA ambao ni Greyson Daudi Luvanda kutoka Unyangala na Enesia Nyakisa Kyando kutoka Ilolo. Mwaka  2009 imepeleka watoto wawili wanachama wa PIUMA ambao ni Ushindi Ebsai Mahenge kutoka Utanziwa na Ashura Israeli Mbwilo kutoka Kilanji.Mpango huu utaendelea kila mwaka

 

 

 

 

 

 

Watoto wanaoenda kusoma wakiwa katika picha ya pamoja

 

 

 

Mwandishi:

 

Witness.

 

5 Responses to “Elimu ni haki ya watoto wetu!”


  1. malila says:

    Nawapongeza kwa mpango huo mzuri na endelevu,kama kungekuwa na uwezekano wa watoto wote (wenye sifa) ambao wazazi wao ni wanachama wa PIUMA wangejulikana(nina maana hata wale ambao wamekosa nafasi hiyo adimu wajulikane). Mwaka uliopita mimi nilifika Bulongwa na mtu mmoja mwenye kupenda kusaidia watoto wenye uhitaji(www.hananasif.org) na tulikuwa tumekwenda kwa kusudi la kumsaidia mtoto mmoja ili aweze kupata elimu ya kidato cha kwanza mpaka atakapoishia, kwa maajabu tulikosa mtoto hata mmoja. Lakini nijuavyo mimi Makete watoto ni wengi,tulichoogopa ni kupata mtoto asiyestahili. Nafasi ile imejazwa na mtoto mwingine. Lakini kwa mtindo huu tutashirikiana ili kuwapata watoto ambao PIUMA inawajua kwa uhakika.

    Mungu akitujalia tujipange vizuri ili kila nafasi itumike ipasavyo.


  2. Jackson says:

    Asante PIUMA
    Asante kwa wafadhiri wa Muhingo- PIUMA Scholarship
    Asante Bwana Malila na wasomaji wengine wa site hii kwa kuunga mkono juhudi za PIUMA na WaVVU Makete. Elimu ni haki ya Kila mtu.
    Watoto wa WaVVU wamekosa nafasi kutokana na kupoteza muda mwingi kuwahudmia wazazi wao wanapokuwa hospitali au nyumbani wanaumwa. Hivyo basi mipango kama hii itawasaidia wengi ambao wanastahili kupata nafasi za kusoma lakini wanshindwa kutoka na athari za UKIMWI.
    Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu;
    Nidekile


  3. Royal Orr says:

    This is great news! I walked with the father of one of the previous Hope School children, Nyakisa Kyando. He is a very impressive man and I hear his daughter is doing very well at school. So thanks to Muhingo and Fatma at Hope School and to PIUMA for this initiative.

    Royal


  4. Muhingo says:

    I would like to thank PIUMA selection team for choosing the right candidate to join our school. The information I receive from the school at Ilula, is that all four students; two in form one and two in form two are doing fine. Enesia is fast growing physically and intellectually and the rest are doing fine and very disciplined. Let us support each other in order to help the comming generation
    Muhingo Rweyemamu


  5. Royal Orr says:

    Comment:
    I would like to thank PIUMA selection team for choosing the right candidate to join our school. The information I receive from the school at Ilula, is that all four students; two in form one and two in form two are doing fine. Enesia is fast growing physically and intellectually and the rest are doing fine and very disciplined. Let us support each other in order to help the comming generation
    Muhingo Rweyemamu

Leave a Reply