MVUA ZA MSIMU BULONGWA
Mvua zimekuwa zikinyesha mfululizo Wilayani Makete na kusababisha barabara kuwa mbaya na wafanya biashara wa Makete kushindwa kufika Soko la Bulongwa kwa ajili ya kuja kununua na kuuza bidhaa zao.
Akizungumza mwandishi wa habari hii, baadhi ya wafanyabishara wa kijiji cha Bulongwa siku ya gulio, walisema kuwa biashara zao wanategemea sana wanunuzi kutoka Makete.
Lakini kwa sasa kutokana na kuwa mvua zimekuwa zikinyesha mfululizo na kuharibu barabara, wafanyabiashara wa Makete wanashindwa kuja kuuza bidhaa zao na kununua.
Soko la Bulongwa linategemewa na vijiji vya tarafa za Bulongwa na Magoma, Limekuwa ni sehemu muhimu ya kuuzia mazao kutoka katika wilaya ya Makete, Tukuyu na Kyela. Hali ya mvua imewafanya wachukuzi wa kutoka kwenye wilaya za karibu kushindwa kufika sokoni. Hali hii imesababisha biashara kuwa mbaya na watu wengi kushindwa kujikwamua matatizo waliyonayo.
Soko la Bulongwa
Witness.



Royal Orr says:
Thanks Witness. I like these kinds of stories about life in the villages.
JEREMIAH SWALLO says:
thanx,WITNESS it seems your too good in publishing us such kind of news.inapendeza sana.J.A.SWALLO-UDSM
Royal Orr says:
Received yesterday:
thanx,WITNESS it seems your too good in publishing us such kind of news.inapendeza sana.J.A.SWALLO-UDSM