Wednesday, April 8th, 2009

TACAIDS NA CHANGAMOTO YA KUJITAWALA NA LISHE BORA KWA WANAMAKETE

 

Tume ya kupambana na UKIMWI,TACAIDS wiki iliyopita lilifadhili mafunzo ya lishe bora na Kujitawala kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI ndani ya Wilaya ya Makete yaliyofanyika  ukumbi wa Lishe  Ikonda.

 

Akizungumza na Mtandao huu mmoja wa washiriki wa semina hiyo, Katibu Mkuu wa PIUMA Bi. Anna Mwinuka alisema kuwa mafunzo hayo yalikuwa ya siku tatu na yalitolewa na wakufunzi wa mafunzo hayo walikuwa ni Abraham Sanga  ambaye ni Mratibu wa Vijana wilaya ya Makete na William Yotham na yalihuduhuriwa na jumla ya watu ishirini na nne wanaoishi na Virusi vya UKIMWI.

 

Washiriki wa mafunzo haya walitoka katika tarafa ya Bulongwa, Magoma na Lupalilo. Pamoja na katibu mkuu wa PIUMA pia wanachama wengine wa  PIUMA walipata bahati ya kushiriki. Bi. Anna aliwataja washiriki wenzie ambao ni wanachama wa PIUMA waliohudhuria mafunzo hayo kuwa ni pamoja na Markusi Chaula, Obote Mahenge, Atumanyile Sanga, Apolo Mbogela, Josephina Sanga, Daudi Luvanda na Wilibadi Sanga.

 

Aliendelea kusema kuwa madhumuni ya elimu ya lishe bora ni kuwajengea uwezo watu wanaoishi naVirusi Vya UKIMWI kutambua namna sahihi za kuboresha lishe zao na hatimaye kuimarisha kinga za mwili kwa wanaoishi ili kuwafanya wawe na afya. Wakufunzi hao walifundisha makundi ya vyakula, ulaji bora, uhusiano wa lishe na Virusi vya UKIMWI, athari za VVU kwenye lishe, usafi na usalama wa chakula.

 

“Somo la kujitawala lilionekana kuwa na changamoto zaidi kutokana na ukweli kuwa washiriki wengi walikuwa hawajawahi kupata somo hili” alisema Bi. Mwinuka. Akifafanua maana aliyoipata kwenye semina juu ya dhana ya kujitawala Bi. Mwinuka alizidi kusema, “kujitawala ni hali ya mtu kumudu kuendesha maisha yake kifikra, kimaamuzi”. Alisisitiza kuwa dhana ya kujitawala ni pamoja na kumfanya mtu anayeishi na Virusi vya UKIMWI kutambua  huduma anazostahili kupata ikiwa ni pamoja na msaada wa tiba, msaada wa kiuchumi, msaada wa kisheria, msaada wa kidini nk.

 

Akishuhudia ni namna gani semina hiyo itakuwa imewasaidia yeye na wanachama wengine wa PIUMA Bi. Mwinuka alisema wanasemina wamefarijika na kufaidika  kwani wametambua kuwa mambo yaletayo faraja kwa mtu anayeishi na Virusi Vya UKIMWI ni kupokea na kulikubali tatizo, kujiunga katika vikundi mbalimbali, kushirikishwa na upendo dhana ambayo PIUMA imekuwa ikiisimamia na kuitekeleza.

 

Wanachama  walioshiriki semina hii wakioongozwa na Katibu Mkuu wa PIUMA waliandika Taarifa juu ya semina hii kisha kuikabidhi kwa mtendaji wa kata ya Bulongwa. Wakimkabidhi taarifa hiyo wanachama hao walisema wanatakiwa kutoa elimu hiyo kwa wanajamii wengine vijijini.

 

 

Baadhi ya wanachama wa PIUMA walioshiriki mafunzo hayo wakiandaa taarifa ya kumkabidhi Mtendaji wa Kata.

 

 

Witness.

 

4 Responses to “TACAIDS NA CHANGAMOTO YA KUJITAWALA NA LISHE BORA KWA WANAMAKETE”


  1. Royal Orr says:

    Greetings to Anna and John and all the Executive! And keep going, Witness - these are great reports and let us know that PIUMA is working!


  2. Jackson says:

    Kuambukizwa virusi vya UKIMWI sio mwisho wa Maisha na mapambano, somo la kujitawala na uraia ni muhimu sana wakati huu wa mapambano na UKIMWI. Tunayaomba mashirika mengine yafuate mfano wa TACAIDS kuwafanya WaVVU kujitambua na kuikubali hali ya maambukizi kisha kukaza mkanda na kusonga mbele, badala ya kugeuka kuwa watu Omba omba.

    Nidekile


  3. Gottfried Mernyi says:

    During the next days it will three years since the former ELCT-SCD Bishop Manyiewa has shut down the CTC, which has been set up by Dr. Rainer, Jackson, PIUMA, the Austrian supporters,…..
    Since this time the human right of PLWAH in Bulongwa to have free access to qualitative treatment with ARVs and supervision of their medical care is neglected by various church officials in Tanzania and Europe. These “servants of the Lord” are still only concerned about their personal reputation, their position and their benefit. The sick and suffering calling for justice and fair use of resources are just spoiling the good partnership between the churches and missions…
    Three years of wasted hope and time to continue the former stage of medical care and treatment for PLWAH.


  4. abdallah zuberi says:

    HI PIUMA MEMBERS
    I WOULD LIKE TO CONGRATULATE YOU ALL PIUMA MEMBERS, YOU ARE WELL ORGANIZED,KEEP IT UP,MAKE MORE EFFORTS IN ALL YOUR ACTIVITIES, LAST OPEN ROOM TO OUTSIDERS {OUT FROM MAKETE} TO JOIN PIUMA.
    BIG UP PIUMA,BIG UP MAKETE.

Leave a Reply