Thursday, May 14th, 2009

WILAYA YA MAKETE YAPATA MKUU MPYA WA WILAYA.

A NEW DISTRICT COMMISSIONER AT MAKETE……WELCOME!

 

 

Katika mabadiliko ya wakuu wa Wilaya yaliyofanywa na Raisi mwezi uliopita. Wilaya ya Makete ilipata mkuu mpya wa Wilaya Mh. Bi Hawa Humbi.

 

Akizungumza na mtandao huu Mh. Estomih Mahenge Diwani wa Kata ya Bulongwa alisema Mh. Lephy Gembe  aliyekuwa mkuu wa wilaya Makete kuanzia mwaka 2006 amehamishiwa Wilaya ya Chamwino – Dodoma.

Alisema kuwa  Mh.Gembe nguvu zake alielekeza kwenye ujenzi wa Sekondari na Zahanati, kwani wakati anafika katika Wilaya ya Makete kulikuwa na sekondari saba, lakini mpaka anaondoka katika Wilaya ya Makete ameacha sekondari 14 ambazo zimeshafunguliwa tayari na kwa upande wa Zanahati ameondoka ameacha maandalizi ya ujenzi  yakiendelea. Kwa Tarafa ya Bulongwa sekondari mpya zilizofunguliwa ni Sekondari ya Usililo na Sekondari ya Kipagalo, na zahanati zilianza kujengwa tayari ni Zahanati ya kijiji cha Idende, Bulongwa- PIUMA shirika lisilo la kiserikali na ukarabati wa zahanati ya Utanziwa na  Luwumbu.”alisema Mh. Mahenge”

 

Mh. Mahenge aliendelea kulisema kuwa tunachotegemea kutoka kwa mkuu mpya ni kukamilishwa kwa sekondari za Wilaya Makete kwa kila kata ambazo bado, ukamilishaji wa zahanati kwa kila kijiji na kuanza kutoa huduma kwa jamii, nk.

 

 

Katika kipindi alichofanya kazi Wilaya ya Makete Mh. Gembe atakumbukwa na wana PIUMA kwa kupiga vita UKIMWI kwa kufanya kazi karibu na wanajeshi wa mapambano dhidi ya UKIMWI, Mh. Gembe aliyewahi kushiriki matembezi ya mshikamano ya PIUMA pia ndiye aliyefungua kituo cha Ushauri nasaha -  HIMA kinachomilikiwa na PIUMA.

 

 

Mh. Bi. Hawa Humbi akiwa kwenye kituo cha PIUMA.

 

 

Mh. Estomih Mahenge - Diwani Kata ya Bulongwa.

 

 

Mwandishi.

 

Witness.

 

 

One Response to “WILAYA YA MAKETE YAPATA MKUU MPYA WA WILAYA.”


  1. malila says:

    Naamini Mkuu wa Wilaya mpya hatatuangusha kabisa, kuna mambo yako ndani ya uwezo wetu wenyewe Wanamakete,mengine yanahitaji mkono wa DC na mengine yanahitaji umoja kati ya DC/halimashauri na sisi. Kufyatua matofali ya ujenzi wa Shule/zahanati,kupeleka watoto shule,kuacha ngono zembe,kufanya kazi kwa bidii nk ni yetu sisi. Ila kubeba bati toka Makete mpaka Usililo,kutafuta walimu/waganga wa zahanati na kuwafikisha Usililo,kuhakikisha madaraja vijijini yapo salama nk ni kazi yetu sote,yaani sisi na timu nzima ya DC. Dc/Halimashauri anaweza kuleta vifaa,sisi tukaacha kuvilinda vikapotea au Mwalimu kaja kijijini sisi hatupeleki watoto shule nk. Karibu sana DC mpya.

Leave a Reply