Tuesday, May 19th, 2009

KIKUNDI CHA TUSAIDIANE CHA WANAWAKE KATA YA INIHO - MAKETE

 

Na Evance Seth

 

Kufuatia kuongezeka kwa ugumu wa maisha mwaka 2003 wanawake wa kata ya Iniho wilayani Makete walianzisha kikundi cha Tusaidiane chenye malengo ya kuwafanya wasaidiane wanapokuwa na shida.

 

Wakizungumza na mwandishi wa habari hii alipotembelea kikundi hicho ili  kujua jinsi wanavyosaidiana wanawake hao walisema kuwa, Lengo la kikundi chao ni kusaidiana katika matatizo mbalimbali, kama , kufiwa na ugonjwa. Kikundi cha Tusaidiane chenye wanawake wanachama mia moja na tatu (103),  kinajishughulisha  na miradi ya uzalishaji mali.

 

Katika miradi ambayo kikundi kinaiendeleza ni pamoja na kilimo cha mahindi, ngano, viazi na bustani za mboga mboga. Pamoja na kilimo pia wanatusaidiane wamekuwa wakiendesha biashara ndogo ndogo. Akina mama hao wamekuwa wakiendesha migahawa na pia kufanya kazi ya kununua na kuuza nyanya na vitunguu.

 

Alipouulizwa kuhusu matumizi ya mapato yatokanayo na miradi ya kikundi hiki mwenyekiti wa kikundi hiki Bi. Rehema Mbogela  alisema pesa inayopatikana inawasaidia wanakikundi kujikimu kimaisha. “wakati ikitokea shida kwa mwana kikundi mwenzetu kama kufiwa , huwa tunachanga fedha, tunanunua sanda, tunagharamia gharama za jeneza, unga na kuni kwa ajili ya  kumuona mwenzetu, na huwa tunasaidia kazi za msibani kama, kupika, kuchota maji na zingine zijitokezazo” alisema Bi. Mbogela.

 

Wanachama walipohojiwa faida za Umoja wao huo walisema umoja huo umekuwa na faida kubwa kwao kwani umewasaidia wakati wakiwa wagonjwa. “Mwanakikundi mwenzetu akiugua na kulazwa hospitali huwa tunachanga fedha na unga kwa ajili ya kwenda kumwona” alisema mama Janeth Mbogela mwanakikundi mwanzilishi. Wanakikundi huonana pindi ndugu zao wauguapo au kufariki, Mume, baba, mama na watoto, ni wandugu walio kwenye orodha ya ndugu wauguao wanaompa mwanakikundi kupata haki ya kuonwa.  Kwa shida za ugonjwa wa ndugu mwanakikundi ataonwa mara tatu kwa mwaka kwa upande wa ugonjwa.

 

Akina mama hawa walieleza kuwa waliamua kuingiza mpango wa kupeana pole kwenye ugonjwa na misiba kwasababu kuna wakati mwingine mtu anapo pata shida  huwa anakuwa hana fedha wala chakula ndani ya nyumba, kwa hiyo ilibidi utafutwe mpango utakaowapa nafasi ya kumsaidia mwanakikundi mwenzao. Ukosekanaji wa mahitaji muhimu wakati wa shida mbali mbali uliwasukuma wanawake  kuunda kikundi cha kusaidiana. Wakiongea na mwandishi  wetu wa habari wanakikundi hao walisema kuwa kikundi chao kimefanikiwa sana kwani kimewavuta wanawake wengi kujiunga nao.

 

Mwenyekiti wa kikundi Bi. Rehema Mbogela.

 

 

 

 

 
 
 
 

 

 

 

 

 

 

 

 
 
 
 

 

 
 
 
 

 

 

 

 

 

 
 
 

 

 

 

 

 

 

3 Responses to “KIKUNDI CHA TUSAIDIANE CHA WANAWAKE KATA YA INIHO - MAKETE”


  1. Jackson says:

    Such kind of efforts as shown by Tusaidiane women Group if goes with determination for self liberation from economic hardship will bring great changes among the members of the community. People should stand up and say NO to Ignorance, Poverty, Corruption and Diseases. They should unite, raise up their Voice and work their way through without fear to the climax of better life. There is no Free Ride for success.


  2. Royal Orr says:

    Thank you Evance for this story. I hope it’s the first of many.


  3. malila says:

    Kama kikundi hicho kimedumu kwa muda mrefu hivi,ni vizuri sisi wadau tukisaidie mawazo ili waweze kuwa na plan za muda mrefu kwa wanachama wa kudumu. Kule inawezekana kuanzisha mradi wa muda mrefu wa kikundi kama miti ya mbao. Wakiomba eneo la wazi kisha kila mwanakikundi apande miti 50 tu kila mwaka,baada ya miaka kumi watakuwa na miti 50,000. Nje ya mbao msitu huo pia utawapa kuni.

Leave a Reply