Friday, May 29th, 2009

Mahindi Tegemeo Milimani.

 

Na Witness Ngumba.

 

Zao la mahindi linategemewa sana katika Wilaya yetu ya Makete kwani ni zao kuu la biashara pamoja na chakula .

 

Akizungumza na mwandishi wa habari hii mkulima wa kijiji cha Madihani Bwana Pitulasi Sanga alisema kuwa zao hili linategemewa sana katika Wilaya yao kwani linawapatia chakula pamoja na kuuza kwa ajili ya kujikwamua matatizo mbalimbali ya kimaisha.

 

Bw. Sanga  alisema kuwa zao hili hulimwa kwa kutumia jembe la mkono  na hulimwa msimu wa kiangazi, zao hili huchukua muda wa mwaka mzima kukomaa na kuvunwa, hulimwa mwezi wa sita na kuvunwa mwezi wa tano, kwa hiyo ni karibia mwaka mzima, kuna baadhi ya vijiji hupandia mbolea lakini kwa kijiji chao hupanda bila mbolea na  palizi yake ni mara moja tu, zao hili halistawi vizuri baadhi ya sehemu kutokana na kukosa pembejeo za kilimo.

 

Aliendelea kusema kuwa hata uvunaji wake wanavuna kwa mikono lakini usafirishaji wake zamani watu wengi walikuwa wanajitwisha kichwani na kupekeka mazao nyumbani lakini siku zinavyozidi kwenda watu wamekuwa wakielimika kwa kufuga punda kwa ajili ya kuweza kuwasaidia kubeba mazao hayo kutoka shambani kuyapeleka nyumbani  na hawa punda wakati mwingine wamekuwa wakiwasaidia kubeba mazao hayo kuyapeleka sokoni kwa ajili ya kuuza.

 

“Matatizo tuyapatayo katika kilimo cha zao hili ni ukosefu wa pembejeo za kilimo pamoja na biashara kwani wakulima wengi tumekuwa tunalima zao hili lakini hatuna

Soko la uhakika, kwa hiyo tunajikuta tunauza kwa bei ya hasara”alisema Bw. Sanga

 

Pamoja na mahindi wilayani Makete pia kunalimwa Ngano, njegere, maharage, viazi vitamu, viazi mviringo.

 

 

 

 

Mkulima akivuna mahindi

 

 

Punda akibeba mahindi kutoka shambani.

 

 

 

 

 

One Response to “Mahindi Tegemeo Milimani.”


  1. Royal Orr says:

    Thanks Witness!

    I love these stories about daily life in Makete. Interesting to see a donkey being used by this farmer - I know this is a relatively recent addition to farm life in the villages. Glad to see that this development effort has at least one ongoing benefit.

Leave a Reply