Bulongwa FC waichapa Mwakavuta Sekondari.
Na Evance Seth.
Michezo ni moja ya changamoto ya kupunguza maambukizi ya UKIMWI. Katika Wilaya ya Makete michezo huguswa sana na kupewa kipao mbele kuanzia shule za msingi, Sekondari hadi vijijini.
Katika mchezo wa mpira wa miguu uliochezwa siku ya Jumatano kati timu ya Mwakavuta Sekondari na Bulongwa football club katika uwanja wa Luvanyina maarufu kama Fly Emirates, ukiongozwa na refa bwana Aksoni Mahenge, timu ya Bulongwa football club (BFC) ilitoka na ushindi wa goli saba kwa moja dhidi ya timu ya Mwakavuta Sekondari.
Kwa kipindi cha kwanza cha mchezo Bulongwa football club ilifunga magoli mawili wakati Mwakavuta Sekondari ilitoka na goli moja, Katika kipindi cha pili cha mchezo Bulongwa football club waliongeza mashambulizi na kuibika na magoli manne na Mwakavuta sekondari kutoka bila goli. Hadi dakika ya mwisho ya mchezo Bulongwa football club ilitoka na ushindi wa magoli saba na wakati Mwakavuta sekondari ilitoka kwa goli moja.
Mwalimu wa michezo wa Mwakavuta Sekondari Bwana Robin Sanga hakuweza kuvumilia kipigo cha magoli hayo aliweza kuwaacha vijana wake uwanjani na kutoroka.
Kwani timu hizo zina upinzani wa hali ya juu, mechi ya kwanza Mwakavuta Sekondari ilishinda bao mbili kwa moja dhidi ya Bulongwa football club. Kapteni wa timu ya Mwakavuta alisema kuwa vijana wake kwa mechi hii wamecheza chini ya kiwango lakini hiyo ni moja ya mchezo, kwani mpira wa miguu una matokeo ya aina tatu, kufungwa, kufunga na kutoka droo.
Na wakati Kapteni wa timu ya Bulongwa football club Bwana Yotamu Nyasanga alisema kuwa vijana wake kwa mechi hii wamecheza mchezo mzuri kwani mechi ya kwanza walipofungwa wachezaji wake wengi hawakuwepo kufuatana na majukumu ya kimaisha.
Makapteni hao wote wawili walisema kwamba hii yote ni kupunguza maambukizi ya UKIMWI kwa vijana pamoja na kuviweka viungo fiti na kukwepa magonjwa nyemelezi.
Pamoja na michezo hiyo kuna baadhi ya matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo timu zote mbili mojawapo ni vifaa vya michezo. Wachezaji wa Bulongwa football club walisema wanachotaka huko mbele waje kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara.
Jezi ya Bluebahari ni timu ya Bulongwa FC na Nyeusi Mwakavuta Sekondari.

