BARUA
Barua kutoka kwa Daktari.
Hivi karibuni nimesikia kwamba watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI ambao wanatumia dawa za kufubaza VVU wanachanganyikiwa juu ya suala la unywaji wa pombe / kileo wakati wanatumia dawa hizo.
Nataka kuwasaidia na ntatumaini kwamba nitaweza kuondoa hofu hiyo ili kuwasaidia kuimarisha afya zenu na kurefusha maisha yenu.
Mara nyingi imekuwa ikisemwa kwamba siyo vizuri kutumia dawa za kufubaza VVU na kunywa pombe wakati huo huo. Ninyi wote mmeambiwa kamwe msiguse pombe mnapotumia dawa hizo zinazookoa maisha yenu!
Sasa ? msikilizeni daktari wenu na watu wanaowapenda na kuwajali kwa dhati. Mtawafahamu kwa kuwa hawatawatisha na wala hawatawafanya mjisikie vibaya.
Kwanza, ni dhahiri kwamba ni VEMA kwa afya yako KUTOKUNYWA (pombe) au kutumia dawa za kulevya wakati unatumia matibabu hayo. Kutokana na uzoefu wenu mnajua kwamba ukinywa pombe nyingi unachoka na unasahau muda na majukumu yako au wajibu wako. Katika hali hii unaweza kusahau kunywa dawa zako kwa wakati muafaka au unaweza kutokunywa dawa hizo kabisa.
Dawa zote zinalenga kukufanya uwe na afya nzuri na hivyo unapewa katika utaratibu fulani na kwa namna nzuri sana. Pombe inakufanya ubadili utaratibu huu na hii ni hatari kwa afya yako. Tumia dawa hizo kama unavyoagiza, na kamwe usibadilishe utaratibu huo.
Pili, Pombe yenyewe siyo nzuri kwa afya yako kama unakunywa sana na hasa inaweza kuleta madhara kwa ini lako katika kipindi cha miaka kadhaa. Watu wanaoishi na VVU ? hata wengine ? wana virusi vingine (virusi vya Hepatitis) ambavyo vinashambulia ini. Na hakuna vipimo vya maradhi hayo Bulongwa.
Kama umeambukizwa na virusi hivyo na pia una VVU madhara kwenye ini yataongezeka ukitumia Pombe. Kwa hiyo nitapendezwa zaidi endapo hutakunywa pombe sana!
LAKINI KAMA UNAKUNYWA POMBE na unafurahi sana:
BADO ? KUNYWA DAWA KWA WAKATI MUAFAKA kama ulivyoagizwa na daktari na kamwe usibadilishe ratiba ya kunywa dawa hizo. Hii ina maanisha kwa mfano: Kama unakunywa TRIOMUNE - kula kidonge kimoja asubuhi na kidonge kimoja jioni katika muda ule ule!
Usisahau: Haya yote ni kwa ajili ya afya yako na maarifa yako. Hakuna mtu mwenye haki ya kukunyima dawa au kukutisha? iwe daktari, muuguzi, afisa wa serikali au mtu yeyote kutoka katika kanisa au mganga wa kienyeji mwenye haki ya kufanya hivyo. Kama unatumia dawa hizo kila mara, na kama matabibu wanafuatilia tiba yako vizuri, ni vema kula dawa hizo ? hata kama unakunywa pombe!
Kumbuka: Ni bora kutokunywa pombe wala kufanya ngono. kama huwezi kujizuia kufanya ngono!kunywa dawa zako na utumie Kondomu!
Nakutakieni maisha mema yasiyo na uwoga! Na endapo una swali lolote ? muulizeni daktari katika ofisi za PIUMA! Tupo hapo kwa ajili yenu na mnaweza kupata ushauri kutoka duniani kote!!”
(Translated from english)
Dr. Rainer Brandl mwenye suti nyeusi na miwani kushoto akimpa maelezo Mh. Rais Jakaya Kikwete ya mashine ya kupima CD4 ya Cyflow_SL3 mali ya PIUMA wilayani Makete. Mashine za Cyflow hutengenezwa na kampuni ya PARTEC ya Ujerumani

