Kujiajiri Kijijini
Na Evance Seth
Mboga mboga ni sehemu muhimu ya mlo kwa wananchi wa wilaya ya Makete. Katika kijiji cha Lumage mtandao huu uliweza kumtembelea Frank mjasiriamali anayeshughulika na kilimo cha mboga mboga.
Akiongea na mtandao huu Frank alisema alianza kilimo hicho mwaka jana akiwa na mtaji wa shilingi elfu tano zilizotosha kununua mbegu tu. “Kilimo cha mboga mboga hakihitaji mtaji mkubwa sana unachohitaji ni mbegu tu” alisema bwana Frank ukizingatia aridhi sio tatizo kwa wilaya ya Makete.
Pamoja na mtaji wa mbegu Frank alihitaji nguvu na muda wa kufanya kazi kwenye bustani yake. Frank analima kwa jembe la mkono na kumwagilia bustani yake kwa ndoo wakati wa kiangazi. Pia mboga za Frank hazitumii mbolea za viwandani kwani anatumia mbolea ya wanayama na anasema imemsaidia sana kwani inaleta mazao mazuri yanayovuti walaji.
“Katika bustani yangu nimepanda mbogamboga za aina tatu ambazo ni kabeji,chainizi na saradi” aliongeza Frank. Alisema kuwa mboga hizo zimesaidia kujipatia mboga mboga za majani kwa urahisi pamoja na kuziuza kwa jamii inayomzunguka na na kujipatia pesa zinazomsadidia kwa matumizi mengine.
Frank anayeuza mboga kuanzia shilingi mia mbili kwa fungu alipokuwa anzungumza na mtandao huu alikuwa na shilingi elfu hamsini zilizotokana na uuzaji wa mboga. “wakati mwingine nakuwa na pesa nyingi zaidi” aliongeza Frank.
Matatizo yanayomkabili ni pamoja na soko duni ,pembejeo za kilimo pamoja na madawa ya kuulia wadudu waharibifu. Frank alisema vifaa vya umwagiliaji ni tatizo kubwa, anahitaji vifaa vitakavyomuwezesha kuokoa muda wa umwagiliaji kwani anahitaji kumwagilia mara mbili kwa siku.
Mipango ya baadaye ya frank ni pamoja na kuongeza eneo kubwa zaidi la bustani na kutafuta soko kubwa la uhakika la mazao yake. Timu ya mtandao huu inampongeza Frank kwa kuwa mjasiriamali wa eneo lake na tunawahamasisha wananchi wengine kuiga mfano wake katika maeneo mengine.


royal orr says:
Thanks Evance and Jackson! Great to see material from Makete on a regular basis.