Ajira na Mazingira
Na Evance Seth
Wakati suala la mazingira ni ajenda namba moja duniani kuna baadhi wanaonekana haiwahusu. Mtandao huu ulifanikiwa kuzungumza na vijana wa kikundi cha ugongaji wa kokoto wa kijiji cha iniho. Vijana hawa walioko katika kijiji cha Iniho wamejiajiri kwa kutengeneza kokoto.
Kuanzia mwaka 2007 ushirika huu wenye jumla ya vijana wannne unajishughurisha na utengenezaji na usambazaji wa kokoto za mawe magumu. Akizungumza na mtandao huu mmoja wa vijana hao Baraka Mdonya alisema waliamua kujishughurisha na biashara ya ugongaji wa kokoto kwa sababu kulikuwa na ujenzi unaendelea kijijini Iniho na vijiji vya jirani lakini walikuwa wanakosa malighafi hiyo. “kwa mfano ujenzi wa madarasa wa shule ya sekondari ya mwakavuta unahitaji kokoto kwa wingi kwa hiyo ilikuwa lazima watu wafanye hiyo kazi” alisema kijana huyo.
Uhafifu wa zana za kutendea kazi unarudisha nyuma uzalishaji kwa kiasi kikikubwa. Kikundi hiki kinatumia nyumdo kubwa moja na nyundo ndogo kadhaa. Utaratibu wa utengenezaji wa kokoto ni kutindua miamba mikubwa baada ya hapo kuigonga kwa nyundo kubwa kutoa vipande vya ukubwa wa wastani, kisha hutumia nyundo ndogo kuvifanya hivyo vipande vya wastani kuwa na ukubwa wa kokoto inayotakiwa.
Walipoulizwa kwa miamba mikubwa inayoshindakana kuvunjika vijana walisema huwa wanaichoma moto hiyo miamba, ikipata moto mwamba mkubwa hufanya nyufa na kisha kuachaia katika vipande vikubwa vikubwa ambayo hugongwa na nyundo.
Wakizungumzia namna wanavyoweza kuufanya moto mkubwa wa kupasua jiwe vijana hao walisema kuwa “huwa tunatumia miti moto wa kuni” walisema . Miti mingi huwa ni inayokatwa katika misitu ya karibu na sehemu ya uchimbaji.
Vijana hao wanasema huuza kokoto yao kufuatana na mahitaji ya mteja. Huwauzia kuanzia wale wanaotaka kununua kwa kiasi cha ndoo moja ya lita kumi ambayo huuzwa kwa shilingi elfu moja, ndoo ya lita ishirini ambayo huuzwa kwa shilingi elfu mbili na trip moja ya roli inayouzwa kwa shilingi laki moja.
Walipokuwa wanaongea na mtandao huu vijana hao walisema wana trip sita za maroli kwenye stoo yao. “pesa tunayoipata kwenye kazi hii hutusaidia kutatua matatizo muhimu ya maisha kama kulipia ada za shule za watoto” walisema vijana hao. Mipango ya baadaye ya kikundi hiki ni kuongeza uzalishaji na kutafuta vifaa vya kisasa zaidi.
Wakizungumzia changamoto zinazowakabili walisema soko bado ni tatizo, walesema wanaweza kuuza kiwango cha kutosha cha kokoto kunapokuwa na makampuni ya ujenzi wilayani makete. Wakitaja mfano wa makampuni hayo, walisema makampuni ya simu yanapojenga minara yao, TANROAD wanapokuwa wanafanya ujenzi wa madaraja na mifereji ya maji barabarani
Pamoja na kuwa biashara ya utengenezaji wa kokoto inawapatia kipato wanaushirika huu lakini pia unasababisha uharibifu wa mazingira. Uchimbaji wa mawe na Ukataji wa miti kwa ajili ya moto wa kupasulia miamba ni sehemu ya uharibu huo. Wakiongea na mtandao huu vijana hao walisema wanatambua madhara hayo lakini hawana namna nyingine. “Hili linaweza lisiwe tatizo kama tutawezeshwa na miradi ya kutunza mazingira kwenye maeneo yetu ya machimbo au kupewa kazi mbadala” alimazia Bw. Mdonya kiongozi wa kundi hilo.
Picha na Evance

