Upimaji wa Aridhi
Na Evance Seth
Wilaya ya Makete imeungana na wilaya zingine za Tanzania katika zoezi la kitaifa la upimaji wa Aridhi na viwanja. Zoezi hili linaratibiwa na kuendeshwa na Mpango wa Kurasimisha Rasimali na Biashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA).
Akizungumza na mtandao huu mwenyekiti wa kijiji cha Iniho Bw. Ferance Sanga alisema zoezi hili limeanza katika wilaya ya Makete mwezi April. Hata hivyo Bw. Sanga alisema mvua zilizokuwa zikinyesha wakati wa masika zilipunguza kasi ya upimaji wa viwanja na mashamba.
Alipohojiwa na Mtandao huu kama anaona faida zozote za zoezi hilo Bi. Roda Muhando alisema, upimaji unawasaidia watu kuwa na hati ya umiliki wa mali zao. “kukatia hati miliki hiyo ni faida kwako kwani hakuna mtu atakaye kupokonya shamba lako kwani utakuwa umekatia hati miliki na litatambuliwa ni la kwako” aliongeza Bi. Muhando.
Bi. Roda aliwaasa wanawake kujitokeza kwa wingi kupewa hati za kumiliki mashamba na Viwanja kwani inawapa nguvu wanawake. “Nikiwa mwanamke nashukuru Serikali kwa kuanzisha huu mpango kwani sasa sitanyanyaswa kutokana na jinsia yangu kwenye umiliki wa aridhi” aliendelea kusema Mama Muhando.
Pamoja na zoezi la upimaji shirika pia litasaidiana na wanachi kujenga ofisi kwa ajili ya matumizi ya maofisa wa kijiji, baraza la aridhi na maofisa wa aridhi. Katika ujenzi huo wananchi watachangia nguvu, uwanja na mawe kwa ajili ya ujenzi na gharama zingine zote zitagharamiwa na MKURABITA.


malila says:
Nawaomba ndugu zangu huko Makete msikubali kuuza ardhi kienyeji kwa watu msiowajua. Tulio nje ya Makete tunajua jinsi ardhi ya Makete ilivyo na thamani kubwa,ninyi huko hamjui ni nini kinatokea kwenu kwa sababu vyombo vya habari havifiki. Kapimeni maeneo yenu na mtunze hati zenu vizuri. Kwa wale wanaozunguka Kitulo wajihadhali,wanaozunguka milima ya Mang`oto kule Ibaga kuweni makini sana. Makete itageuka kuwa bidhaa adimu muda si mrefu.
Jackson says:
Kweli Kaka Malila, watu wengi sasa hivi hawajajua thamani iliyopo kwenye wilaya hii, mvua karibu mwaka mzima, huwezi amini kuwa hizi picha zimepigwa kiangazi mwezi wa Saba lakini unaona hiyo ever green? Kuna umuhimu wa wana Makete kuiindeleza wilaya yao, milima isiwe kikwazo bali iwe ni nyenzo.
malila says:
Mambo ninayofahamu kuhusu Makete ni haya, lami itajengwa toka njombe mpaka Isyonje Mbeya,lini mi sijui(nasikia soon wataanza pale Mang`oto). Kitulo patakuwa recreation area ya kimataifa baada ya Uwanja wa Ndege wa Songwe kukamilika. Sijui nini kinaendelea kuhusu Umeme wa maji na madini, ila siku moja umeme mkubwa utatoka Bulongwa. Kiwango cha miti kilichopandwa Makete kinatia moyo sana. Shamba kubwa la ng`ombe litahamia Ibaga. Tayari kuna fununu za kilimo cha mashamba ya maua huko makete,sijui sehemu pamekuwa- located. Nawasihi kwa nguvu zangu zote,hakuna kipande cha ardhi kilichoko makete kisicho na thamani.