WANACHAMA WA PIUMA WAALIKWA KUTEMBELEA KIKUNDI CHA CHAKUNIMU – NJOMBE.
Na Witness Ngumba.
Wanachama watano wa PIUMA wiki iliyopita walialikwa kwenda Njombe kuonana na kikundi cha CHAKUNIMU(Chama cha Kupambana na UKIMWI ,Nyumbanitu, Itulike, Mvelela, Ulembwe) ili kujifunza na kubadilishana mawazo juu ya kuhudumia wagonjwa majumbani (HBC) na kujifunza kazi mbalimbali zinazofanya na kikundi hicho.
Wanachama hao wameenda kukaa siku kumi (10) na wanachama waliokwenda ni Markusi Chaula, Apolo Mbogela , Esterina Swalo, Anamere Pilla na Sabina Sanga.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii mkuu wa msafala Bwana Markusi Chaula alisema kuwa matembezi hayo yalikuwa ya siku kumi na tumetembelea vijiji sita vyenye umbali wa kilomita 114,na wagonjwa tuliotembelea ni 84, vijiji vyote hivyo tulikuwa tunatembea kwa mguu.Vijiji vyote hivyo tuliongozwa na Lawrence Lilawola- Mwenyekiti wa CHAKUNIMU na Amoni Msigwa- Katibu wa CHAKUNIMU. Na jumla ya watu liokuwa tumeshiriki katika matembezi haya tulikuwa watu 30 tuliokuwa tumetoka sehemu mbalimbali.
Aliendelea kusema kuwa kazi zinazofanywa na kikundi cha CHAKUNIMU ni kuhamasisha jamii kwenda kupima Virusi vya Ukimwi kwa hiari, kuwatembelea wagonjwa majumbani katika vijiji vyote vilivyo ndani ya CHAKUNIMU.
Lakini kuna baadhi ya tofauti tulizoziona kati ya PIUMA na CHAKUNIMU, CHAKUNIMU ni kukundi cha watu mchanganyiko waliopima Virusi vya Ukimwi na ambao hawajapima na wakati sisi PIUMA ni kikundi cha tuliopima na tunaishi na Virusi vya Ukimwi na wao kituo cha kuchukulia dawa ni mbali sana sio sawa na sisi PIUMA. Pia wao hutembelea wagonjwa kila kijiji kilichopo ndani ya CHAKUNIMU wakati sisi PIUMa hatufanyi hivyo.
Baada ya kumaliza kutembelea vijiji sita tulikusanyika pamoja na kukaa kikao cha kutathimini kazi ilivyofanyika, wajumbe wa pande zote mbili walisema kuwa tumefanya kazi kubwa kwani watu wengi wamefurahi kuwatembelea kwani wameelika sana juu yetu kwa kujieleza ni jinsi gani tunavyoishi na VVU na kutualika tena tuweze kuwatembelea kwa wakati mwingine.


Jackson says:
Jamaa wanaonekana wamechoka sana!!! poleni sana. Naamini PIUMA wamejifunza mbinu nzuri za jirani kumtembelea jirani na sasa tutaona watu wakipewa huduma bora kutoka kwa majirani zao.
royal orr says:
Hongera sana!
Great to see this kind of cooperation with our friends at CHAKUNIMU. Neighbours can help neighbours and make a big difference in the quality of life of people living with HIV.