Zoezi la kuandikisha wapiga kura
na Evance Seth
Wananchi wilayani Makete kwa muda wa siku tano mfululizo wameungana na watanzania wenzao wa mkoa wa Iringa kushiriki katika zoezi la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura. Zoezi hili lilimhusu kila mwananchi mwenye umri wa kuanzia miaka kumi na nane na kuendelea na mwenye akili timamu.
Akiongea na wananchi wa kata ya Iniho Mtendaji wa kata ya Iniho Bw. Christopher Fungo aliwaambia wananchi wa kata hiyo kuwa umri wa miaka zaidi ya kumia na nane na akili timamu ndio sifa pekee za kumfanya mtu aandikishwe katika daftari la kudumu la wapiga kura
Akifafanua zaidi mtendaji huyo alisema “mtu ambaye hana kadi ya kupigia kura au endepo amepoteza hataruhusiwi kupiga kura” hata Hivyo alizidi kusema watu wanaofikisha miaka hiyo wataandikishwa na kupewa kadi za kupigia kura na baadaye kuruhusiwa kushiriki katika zoezi la upigaji kura.
Kuhusu wapiga kura waliondikishwa lakini wamefariki mtendaji huoyo alisema kuwa kadi zao zinapswa kurudishwa kwa muandikishaji ili taarifa zao ziweze kufahamika.
Akiongea na mtandao huu mmoja wa wanachama wa PIUMA aliyejiandikisha katika zoezi hili Bw. Shem Kilemile alisema kupiga kura ni haki na niwajibu wa kila raia. “Nikiwa kama raia wa nchi hii nina haki ya kuchagua na kuchaguliwa, na ninaona ni wajibu wangu kutimiza haki hii” alisema Bwana Kilemile.
