Friday, October 23rd, 2009

Matumizi ya Benki Yaongezeka Makete

Na Evance Seth

 

Meneja wa NMB tawi la Makete Bi. Doris  Luvanda amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la wateja wa Benki hiyo katika msimu wa Januar hadi machi kwa mwaka huu 2009.

 

Bi. Luvanda ameyasema hayo wiki iliyopita alipokuwa akizungumza na na mwandishi wa habari hizi kuhusu hali ya ongezeko la wateja pamoja na huduma na huduma zitolewazo na Benki ya NMB tawi la Makete.

 

Aidha amesema kuwa wateja wote waliokuwa wamejaza fomu kwa ajili ya kupata kadi za ATM, kadi zao zimekwisha wasili tangu mwezi wa pili mwaka huu. Hata hivyo Bi. Luvanda alitoa angalizo kw wateja watakao chelewakuchukua kadi zao, “atakayechelewa kuchukua kadi hizo ndani ya miezi sita atatakiwa kuomba upya na atalazimikakulipia gharama za kadi upya yaani kamisheni” aliongeza Bi. Luvanda.

 

Akielezea hali ya watu waliofariki wakati wakiendesha akaunti zao katika Benki hiyo amewaomba ndugu wa marehemu kufika katika benki hiyo ili kupata maelezo ya kina na namna ya kupata pesa katika akaunti za marehemu hao.

 

Bi. Luvanda amewataka wale wote waliofungua akaunti katika benki hiyo na kukaa zaidi ya mwaka mmoja bila bila kuweka wala kuchukua fedha, hivyo kusababisha akaunti zao kulala wanatakiwa kufika na picha za paspoti size ili kufufua akaunti zao.

 

Kumekuwa na ongezeko kubwa la utunzaji wa pesa kwa wanachi wa Makete hivi karibu, Vijana wengi wamekuwa wakitunza pesa zao benki.

Leave a Reply