Tuesday, October 27th, 2009

Ujenzi wa Sekondari Iwawa

Na Evance Seth

 

Wananchi wa kata ya Iwawa wanakabiliwa na shughuli  za ujenzi  wa  majengo yanayoendelea kujengwa shuleni hapo  ikiwa pamoja na  ujenzi wa Hosteli , Maabara , Maktaba pamoja na  jengo kwa ajili ya kidato cha tano na kidato cha sita.

 

Hayo  yamezungumuzwa na  Afisa mtendaji  wa Kata  ya Iwawa Bw Selemani Kiwone katika mazungumzo yake na mwandishi wa habari hii.

 

Akizungumzia ujenzi huo mkuu wa shule hiyo Bw.  Omath Sanga amesema kuwa wananchi wametoa mchango  mkubwa  katika ujenzi unaoendelea kwa usombaji  wa mawe, mbao, uchimbaji kiwanja pamoja na  mafundi kujenga majengo hayo.

 

‘’viongozi wa serikali wanatakiwa kutambua  umuhimu  kushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi” alisema Bw. Kiwone. Akifafanua juu ya suala hilo Bw. Kivone alisema katika ujenzi wa shule za ya sekondari  baadhi ya viongozi wa Halmashauri wapo nyuma  katika kuchangia  ujenzi. “Hali hiyo inasababisha  kuwakatisha tama wananchi wanaotoa michango pamoja na nguvu zao shuleni hapo” alimalizia Bw. Kiwone.

 

Naye mkuu wa shule ametoa changamoto zinazo wakabili shuleni hapo kuwa ni pamoja na upungufu wa walimu, nyumba za walimu, baadhi ya vyumba vya madarasa kuto karabatiwa na kusababisha wanafunzi kulundikana katika darasa moja, hali ambayo ina sababisha mwalimu kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

Leave a Reply