Thursday, October 29th, 2009

RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA KATA YA BULONGWA AKIELEKEA MKOA WA MBEYA.

Na Witness Ngumba.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika ziara ya kutembelea mkoa wa Iringa ametembelea kijiji cha Bulongwa leo mnamo saa 4:30 asubuhi akielekea mkoa wa Mbeya.

Alipofika katika kijiji cha Bulongwa njia panda Namanga, alikumbana na mkusanyiko wa wanakijiji wa bulongwa, wanafunzi pamoja na wanachama wa PIUMA wakiwa kati kati ya barabara wakitaka kuonana na Rais.

Rais alimwomba mwenyekiti wa kijiji cha bulongwa ili aweze kuzungumza nae kwa niaba ya wanakijiji wote ili atoe matatizo yanayowakabili wananchi wa kijiji hiki.

Mwenyekiti wa kijiji cha Bulongwa Bw. Merikizedeki Jekela alisema kuwa tatizo la kwanza ni mbolea za ruzuku hazifiki kwa muda mwafaka na zikifika  haziwafikii walengwa. Rais alisema kuwa tatizo hili amelipata kwa vijiji vingi na ameshaongea na viongozi wa Wilaya juu ya kutatua tatizo hili.

Tatizo la pili  ni mawasiliano ya barabara alimweleza Rais kuwa bara bara yetu wakati wa masika huwa inaharibika na kusababisha kukosekana kwa mawasiliano ya bara bara. Rais alisema kuwa hili tatizo ameliona na alivyokuja mwaka jana aliwaagiza viongozi wa Wilaya ya Makete waanze kutengeneza barabara kwa lami kuanzia Njombe hadi Makete, alisema kuwa amepitia kuangalia utekelezaji huo na ameona wameshaanza utengenezaji wa barabara hiyo, lakini alisema kuwa kwa barabara ya Bulongwa kwenda Mbeya atapitia kuiangalia na kuona ni jinsi gani ya kuikarabati.

Tatizo la tatu ni maji ya bombani, mwenyekiti alimweleza Rais kuwa tulikuwa na maji ya bombani ambayo yalitengenezwa na DANIDA miaka ya nyuma sana lakin kwa sasa vifaa vya maji vimechakaa, na kusababisha maji kushindwa kuwafikia wananchi wa Bulongwa, alimwomba Rais ukarabati wa mradi huo ili wananchi waendelee kupata maji. Rais alisema kuwa alimepokea hilo lakini uongozi wa kijiji uandike madai hayo na kupeleka kwa uongozi wa Wilaya ili wao wapeleke kwenye uongozi wa mkoa na hatimaye taifani ukiwafikia wao wataangalia ni jinsi gani ya kuwasaidia wananchi wa Bulongwa.

 

Tatizo la nne Umeme; Mwenyekiti alimweleza Rais kuwa kijiji cha bulongwa mto Luvanyina ambao unaweza kuzalisha umeme sasa mheshimiwa atatusaidije juu ya hili. Rais alisema kuwa alishawahi kupata habari za mto huo, kwa hiyo bado wanaufanyia kazi.

 

Wananchi wa Bulongwa walifurahi sana kuweza kumfahamu Rais na kuweza kuwasikiliza matatizo yao na Rais mwenyewe alisema kuwa amefurahi sana kuweza kuonana nao kwani kupita vijijini ndipo anapogundua matatizo mengi ya wananchi, baada ya hapo aliwaaga wananchi na kuondoka kuelekea mkoa wa Mbeya.

Rais Jk akiongea na Mwenyekiti wa kijiji cha Bulongwa

Rais Jk akiongea na Mwenyekiti wa kijiji cha Bulongwa

 

 

 

wanaPIUMA wakiwa miongoni mwa kumpokea Rais

wanaPIUMA wakiwa miongoni mwa kumpokea Rais

 

wananchi wamekusanyika wakimsubiri Rais

wananchi wamekusanyika wakimsubiri Rais

 

 

 

 

One Response to “RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA KATA YA BULONGWA AKIELEKEA MKOA WA MBEYA.”


  1. Rainer Brandl says:

    Hi, did you ask him about his promises to PIUMA and PLWHA?

Leave a Reply