Archive for November, 2009

Wednesday, November 18th, 2009

Mradi wa Rafiki wa Vijana

Na Evance Seth

 

Vijana  wa kijiji cha Ivalalila wametakiwa kutumia  HUDUMA  YA RAFIKI KWA VIJANA ili waweze kujitambua.

 

Hayo yamesemwa na  Daktari Bw. Jonathan  Kitundu wakati akitoa elimu  ya Rafiki Kijana iliyo fanyika katika kijiji hicho cha Ivalalila. Daktari Kitundu amesema huduma ya Rafiki inatolewa kwa vijana  ili kukuidhi mahitaji  aliyo nayo kwa muda mwafaka.

 

Amesema vijana wanatakiwa kufika  katika Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya  na vituo vya vijana  kwa ajili ya huduma hiyo  na kuwataka kupima afya zao kwa ajili ya kupanga malengo yao ya baadaye.

 

Na mwisho Katibu wa vijana  tawi  la Ivalalila Bw Agano Sanga  amesema elimu waliyo ipata  itawasaidia vijana kuepukana na  maambukizi ya virusi vya ukimwi hususani katika HUDUMA YA RAFIKI KWA VIJANA.

Wednesday, November 18th, 2009

Walemavu na Mikakati

Na Evance Seth

 

Katika wilaya ya Makete kuna kikundi cha walemavu  kilichopo hapahapa Makete kinacho itwa (KICHAWAMA)  kimepanga  mipango madhubuti juu ya kuijengea uwezo  jamii ya watu wenye matatizo  ya ulemavu kwa kutoa elimu ya ufundi stadi pamoja  na kutoa elimu  kwa jamii kutambua  haki za walemavu wa aina zote.

 

Akizungumuza na mwandishi wa habari Mwenyekiti wa kikundi  cha walemavu  Makete Bw. Niko Mbwilo  amesema watu wenye matatizo ya  ulemavu wamefikia hatua  ya kukata tama kutokana na jamii kuona kama  walemavu hawawezi lolote.

 

Bw Mbwilo ameeleza matatizo yanayo wakabili  kuwa ni pamoja na  kukosa nyumba  ya kufundishia  pamoja na  chakula kwa walemavu ambao wangependa  kujifunza fani mbalimbali.

 

Pia amesema  kama kikundi  wameweza kutoa  mafunzo ya ufundi  katika kata ya Ipepo pamoja na kata ya Iwawa, lakini ameomba serikari kuwasaidia kupata idadi ya walemavu  ili kuweza kupanga  miundo mbinu katika mwaka 2010

Tuesday, November 3rd, 2009

Ujenzi wa jengo la PIUMA wapamba moto.

Na Witness Ngumba.

Ujenzi wa jengo la PIUMA waenda kasi kwani wanachama wa PIUMA wanapenda ifikapo tarehe 1 December 2009 jengo lao liwelimekwisha na hatimaye waweze kuhamishia ofisi zao zote huko.

Hayo yalisemwa jana na mwenyekiti waPIUMA Bw. Kabuyu Kyando akizungumza na mtandao huu kwenye ofisi ya KatibuTarafa akiwa pamoja na baadhi ya viongozi waPIUMA katika kikao cha pamoja na serikali ya Tarafa.

Mkutano huu ulioitishwa na Katibu tarafa ya Bulongwa Bw. Ambilikile Mwaihola ulikuwa kwa ajili ya kukaa pamoja, kujadilina kupata ufumbuzi juu ya kumaliza jengo la PIUMA haraka.“Nimepata taarifa kuwa pesa za Ujenzi zipo lakini inaonekanakunakosekanauwajibikaji miongoni mwa viongozi na wanachama wa shirika” alisemaKatibu tarafaBw. Mwaihola

Akimtoa wasi wasi katibu tarafa, Mwenyekiti wa PIUMA alisema kuwa yeye na wanachama wa PIUMA wamejipanga kisawa sawa kuhakikisha jengo linaisha ifikapo December mwaka huu. “Mpaka sasa kila siku mwanachama wa PIUMA pamoja na viongozi wana shinda na mafundi kwenye jengo” alisema Bw. Kyando. Aliongeza kuwa kumekuwa na mafundi wakorofi na kuwa fundi ambaye ataonekana anasumbua hatua za kisheria zitachukuliwa juu yake.

Alisema kumekuwa na usumbufu wa hapana pale kutoka kwa mafundi, akitoa mfano Mwenyekiti alisema fundi seremala ameanza kutusumbua tumemwandikia barua ya onyo nakuhakikisha anamaliza kazialiyokuwa amekabidhiwa haraka vinginevyo hatua zakisheriazitachukuliwa.

Veranda imeshaisha kusakafiwa, wiki hili tunategemea kumaliza kufunga milango na hatimaye fundi waumeme na rangi waanze kazi. Tutahakikisha kuwa tunafanya mawasiliano na Mshauriwa wa ujenzi Mtaalam Mwamwala ili awakabidhi kazi mafundi wa umeme na rangi haraka iwezekanavyo. “Nitahakikisha nitalisimamia jengo letu mpaka litakapoisha ili niweze kupata matibabu bora kwa wakati muafaka” alisema Mwenyekiti.

Jengo la PIUMA linatarajiwa kitumika kama kituo cha tiba na ofisi kwa ajili ya upangaji na uendeshaji wa kiliniki ya upimaji na ushauri nasahaa.