Tuesday, November 3rd, 2009

Ujenzi wa jengo la PIUMA wapamba moto.

Na Witness Ngumba.

Ujenzi wa jengo la PIUMA waenda kasi kwani wanachama wa PIUMA wanapenda ifikapo tarehe 1 December 2009 jengo lao liwelimekwisha na hatimaye waweze kuhamishia ofisi zao zote huko.

Hayo yalisemwa jana na mwenyekiti waPIUMA Bw. Kabuyu Kyando akizungumza na mtandao huu kwenye ofisi ya KatibuTarafa akiwa pamoja na baadhi ya viongozi waPIUMA katika kikao cha pamoja na serikali ya Tarafa.

Mkutano huu ulioitishwa na Katibu tarafa ya Bulongwa Bw. Ambilikile Mwaihola ulikuwa kwa ajili ya kukaa pamoja, kujadilina kupata ufumbuzi juu ya kumaliza jengo la PIUMA haraka.“Nimepata taarifa kuwa pesa za Ujenzi zipo lakini inaonekanakunakosekanauwajibikaji miongoni mwa viongozi na wanachama wa shirika” alisemaKatibu tarafaBw. Mwaihola

Akimtoa wasi wasi katibu tarafa, Mwenyekiti wa PIUMA alisema kuwa yeye na wanachama wa PIUMA wamejipanga kisawa sawa kuhakikisha jengo linaisha ifikapo December mwaka huu. “Mpaka sasa kila siku mwanachama wa PIUMA pamoja na viongozi wana shinda na mafundi kwenye jengo” alisema Bw. Kyando. Aliongeza kuwa kumekuwa na mafundi wakorofi na kuwa fundi ambaye ataonekana anasumbua hatua za kisheria zitachukuliwa juu yake.

Alisema kumekuwa na usumbufu wa hapana pale kutoka kwa mafundi, akitoa mfano Mwenyekiti alisema fundi seremala ameanza kutusumbua tumemwandikia barua ya onyo nakuhakikisha anamaliza kazialiyokuwa amekabidhiwa haraka vinginevyo hatua zakisheriazitachukuliwa.

Veranda imeshaisha kusakafiwa, wiki hili tunategemea kumaliza kufunga milango na hatimaye fundi waumeme na rangi waanze kazi. Tutahakikisha kuwa tunafanya mawasiliano na Mshauriwa wa ujenzi Mtaalam Mwamwala ili awakabidhi kazi mafundi wa umeme na rangi haraka iwezekanavyo. “Nitahakikisha nitalisimamia jengo letu mpaka litakapoisha ili niweze kupata matibabu bora kwa wakati muafaka” alisema Mwenyekiti.

Jengo la PIUMA linatarajiwa kitumika kama kituo cha tiba na ofisi kwa ajili ya upangaji na uendeshaji wa kiliniki ya upimaji na ushauri nasahaa.

 

 

 

 

 

5 Responses to “Ujenzi wa jengo la PIUMA wapamba moto.”


  1. Fabian Wirnsperger says:

    GREAT, that there is some progress here! Keep it up! Fabian


  2. Fabian Wirnsperger says:

    …and thanks for putting up the pics ;-)


  3. royal orr says:

    Thank you, Witness, for the report and the photos and congratulations to Kabuyu and Izaak for the progress.


  4. Mmaka Sanga says:

    Asanteni sana kwa ripoti… hongera kwa kazi zenu.

    Maongezi na usikilizaji wahitaji kupokewa ka vile twajenga sipitali - nyumba ya kutibu ndugu zetu. Fundi seremala anahitaji kuambiwa kiungwana kuwa hata ka vile analipwa, anahitaji kuwa na moyo wa kuelewa kuwa anasaidia kujenga nyumba ambayo itatibu ndugu zake, majirani wake, nk - mbeleni. Nakutakieni kila la kheri. Sote twahitaji kuwa na tabia za kujitolea ama kujali kuwa na bidii ya ujenzi wa nchi/wilaya yetu badala ya tabia ya kuwa “hii ni kazi ya kulipwa, sijali angalau ntalipwa” … nakushukuruni nyie hapo wa PIUMA, manake mna tabia za kujali kujenga wilaya yetu. Asanteni.

    * paraphrasing… we need to have in us and instill in builders that we and them are building something important that would actually service our own relatives and friends - now and in the future. Some of us tend to be short-sighted and interested in what personal profits we get now and tend to do a so-so job as we get paid and get away with un-audited jobs. Afrika and our district/village will be well-served when we all internalise that we are building our own lives…

    Thanks to PIUMA workers and volunteers for exemplifying the best attitude that I speak of …


  5. Rainer Brandl says:

    Dear Mmaka Sanga!

    Thanks a lot for your comment! I think this is very valid, I would apreachiate if you go on teaching PIUMA.
    PIUMA go on, Kabuyu, the big chairman, it is your turn! Good that all of you seem to go on taking your drugs! I hope you will stay well and healthy!

    PIUMA imara kama simba!

    Rainer

Leave a Reply