Mradi wa Rafiki wa Vijana
Na Evance Seth
Vijana wa kijiji cha Ivalalila wametakiwa kutumia HUDUMA YA RAFIKI KWA VIJANA ili waweze kujitambua.
Hayo yamesemwa na Daktari Bw. Jonathan Kitundu wakati akitoa elimu ya Rafiki Kijana iliyo fanyika katika kijiji hicho cha Ivalalila. Daktari Kitundu amesema huduma ya Rafiki inatolewa kwa vijana ili kukuidhi mahitaji aliyo nayo kwa muda mwafaka.
Amesema vijana wanatakiwa kufika katika Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya na vituo vya vijana kwa ajili ya huduma hiyo na kuwataka kupima afya zao kwa ajili ya kupanga malengo yao ya baadaye.
Na mwisho Katibu wa vijana tawi la Ivalalila Bw Agano Sanga amesema elimu waliyo ipata itawasaidia vijana kuepukana na maambukizi ya virusi vya ukimwi hususani katika HUDUMA YA RAFIKI KWA VIJANA.
