Walemavu na Mikakati
Na Evance Seth
Katika wilaya ya Makete kuna kikundi cha walemavu kilichopo hapahapa Makete kinacho itwa (KICHAWAMA) kimepanga mipango madhubuti juu ya kuijengea uwezo jamii ya watu wenye matatizo ya ulemavu kwa kutoa elimu ya ufundi stadi pamoja na kutoa elimu kwa jamii kutambua haki za walemavu wa aina zote.
Akizungumuza na mwandishi wa habari Mwenyekiti wa kikundi cha walemavu Makete Bw. Niko Mbwilo amesema watu wenye matatizo ya ulemavu wamefikia hatua ya kukata tama kutokana na jamii kuona kama walemavu hawawezi lolote.
Bw Mbwilo ameeleza matatizo yanayo wakabili kuwa ni pamoja na kukosa nyumba ya kufundishia pamoja na chakula kwa walemavu ambao wangependa kujifunza fani mbalimbali.
Pia amesema kama kikundi wameweza kutoa mafunzo ya ufundi katika kata ya Ipepo pamoja na kata ya Iwawa, lakini ameomba serikari kuwasaidia kupata idadi ya walemavu ili kuweza kupanga miundo mbinu katika mwaka 2010
