Siku ya UKIMWI duniani 1.12.2009
Na Witness Ngumba
Siku ya UKIMWI duniani ni siku ambayo huwa inaadhimishwa kila mwaka Tanzania nzima kwa ajili ya kuwakumbuka watu waliokufa kwa ugonjwa wa UKIMWI pamoja na wanaoishi na Virusi vya UKIMWI.
Kwa Wilaya ya Makete Tarafa ya Bulongwa Siku hii imeadhimishwa katika tarafa ya Bulongwa kijiji cha kitula ikiwa ni muunganiko wa kata mbili, kata ya Kipagalo na kata Bulongwa. Sherehe hii ilianza rasmi saa 6:00 mchana ikiongozwa na katibu Tarafa wa Bulongwa Bw. Ambikile Mwaihola, Mgeni rasmi wa sherehe hii alikuwa ni Mh. Diwani Estomih Mahenge. Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa “UHURU NI UWEZO”
Mgeni rasmi aliwashukuru watu wote wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kwa kufuata taratibu zote za dawa pamoja na mashirika yanayosaidia kutoa huduma ikiwemo PIUMA.
Katika sherehe hii PIUMA waliandaa kwaya, igizo pamoja na kugombea umiss Uhuru Bulongwa, aliyeongoza kwa umiss alikuwa ni Rehema Nyamule, akifuatiwa na Wema Sanga, Anna Mwinuka,Tulingila Sanga.






Jackson says:
Guys you made me laugh like nothing!
Rehema Nyamule a PIUMA member, won a 2009 Miss Uhuru ha ha ha Congratulation Rehema, Bravo PIUMA for taking part in the World AIDS Day.
royal orr says:
Great report, Witness! Thanks very much for keeping us informed and congratulations to the organizers of this event.
malila says:
Hongereni sana,wakati mwingine stress ktk miili yetu huondoka kwa burudani za pamoja kama walivyofanya piuma