Mkutano mkuu wa mwaka PIUMA.
Na Witness Ngumba.
Mkutano mkuu wa mwaka wa PIUMA umefanika tarehe 18/12/2009, mgeni rasmi wa mkutano alikuwa ni Mkuu wa Wilaya Bi. Hawa Ng’humbi, wageni wengine waliokuwepo ni pamoja na Joseph Chaula – DAS, Felician Chawala - Ag. DMO, Hamza – ofisi ya DSO, Erica Sanga – Viti maalumu, Estomih Mahenge – Diwani bulongwa, Ambikile Mwaihola – Afisa Tarafa, Clemence – WEO Bulongwa, Edward Masevela – Ad. BLH, Benitho Ngailo - MASUPHA wanachama wa PIUMA waliokuwa wamehudhuria walikuwa 75 na wengine wengi.
Ilisomwa taarifa ya Katibu na Katibu mkuu pamoja na taarifa ya fedha ilisomwa na Mtunza Hazina wa PIUMA.
Mkuu wa Wilaya alitoa salamu na shukrani nyingi kwa shirika la PIUMA kwa kazi nyingi zinazofanywa na shirika hili hasa dhidi ya mapambano ya UKIMWI. Aliendelea kusema kuwa alipokuwa alifika katika Wilaya ya Makete shirika ambalo limekuwa likijishughulisha na masuala ya upimaji ni shirika la PIUMA , aliwaasa wanachama wa PIUMA kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya faida za kupima pamoja na hasara za kutokupima afya zao.
Pamoja na hayo Mkuu wa Wilaya alishukuru kwa ujenzi wa jengo la PIUMA ambalo tunategemea kuwa litakuwa Zahanati ya PIUMA hapo baadaye na kuwaahidi kuwa atachangia kiasi cha sh. 200,000/= kwa ajili ya ujenzi wa jengo la PIUMA.






Royal Orr says:
Thank you, Witness for the report. The photos are getting much stronger!
Rainer Brandl says:
Masevella, isn’t he one of the people who was responsible for the diocesan projects when several 100.000 Euro had been stolen by church employees, he is now the BLH adimistrator, that is what directors of the german missions NMZ and Mission Centrum ONE world call “People have been held responisble”?
It is intersting how sticky NGOs and Churches and criminal Missions are when it comes to stay with money and the Charity Business!
malila says:
Piuma mtaendelea kuwa chachu na mwanga kwa taasisi nyingine hapo Makete. Mungu awajalie nyote.