Archive for February, 2010

Friday, February 26th, 2010

Sensa ya Mifugo.

Na Evance Seth.

Makarani na  wasimamizi  wa SENSA  ya mifugo  wamepatiwa mafunzo yatakayo wawezesha  kupima mpango mzima  wa kuondoa  kwenye sekta ya kilimo na mifugo  kwa mwaka 2009/2010.

 

Akifungua mafunzo hayo  yaliyofanyika katika  wilaya ya Makete  kaimu katibu tawala wa mkoa  wa Iringa  Bw. Adam Swai amesema  mwaka 2008  mpango wa sekta ya kilimo kwa pato la taifa  kulikuwa ni asilimia  25.8, kati ya asilimia hiyo ya kilimo  cha mazao  kilichangia  asilimia 19 huku mifugo  ikichangia asilimia 4.7.

 

Kwa upande Meneja takwimu  mkoa wa Iringa  amesema  sense  hiyo hufanyika  kila baada ya miaka mitano na kwamba  katika mafunzo  hayo  watachagua  wakulima kumi , kutoka  katika  mafunzo hayo watachagua  wakulima kumi na tano kutokana na vigezo vilivyowekwa  vya wakulima bora  katika kila wilaya .

Friday, February 26th, 2010

Watumishi wa UMA

 

Na Evance Seth.

 

Ofisi ya Rais  menejimenti ya utumishi wa UMA inakusudia kuwa watumishi  wa serikari  kuanza  kupokea mishahara  dirishani  badara ya kuwaingizia  katika akaunti zao.

Kauli hiyo imetolewa  na waziri wa  Nchi  ofisi ya Rais  menejimenti ya utumishi wa uma Mh. Hawa Ghasia alipokuwa akiwahutubia watumishi  wa halmashauri ya wilaya ya makete. Alisema  ofisi yake inafikilia  kufanya hivyo kutokana na  kulipa mishara hewa ya watumishi.

 

Mpango huo  wa watumishi kupokea dirishani  utasaidia kuondoa udanganyifu ambao serikari inalipa mishahara hewa na kusababisha  serikari hasara kubwa. Amesema katika kupitia  utafiti  uliofanywa na wizara yake imebaini katika sekta  ya afya  na sekta ya elimu  baadhi ya watumishi  wanalipwa  mishahara hewa.

Mh. Ghasia  alikuwa  katika ziara yake ya  kutoa semina  kwa halmashauri ya wilaya ya makete inyohusu mabadiliko  mahali pa kazi  na utawala bora  ambapo hii leo  akitoka hapa anaelekea  wilayani Ludewa.

Mikoa mingine ambayo amepitia  kutoa semina hiyo ni  MANYARA, KIGOMA, LINDI, MTWARA, PWANI , IRINGA  na akimalizia SINGIDA.

Friday, February 26th, 2010

CHANJO YA WATU WAZIMA

  

Na Evance Seth.

 

Katika Wilaya ya Makete kata ya Iniho  kumefanyika chanjo ya watu wazima  kuanzia miaka mitano na kuendelea.

 

Chanjo hiyo ilikuwa ni agizo la serikari kuwa kila mwananchi anatakiwa kupata  chanjo ilimradi ana miaka kuanzia mitano. Chanjo hiyo  alihudumia  Bw. Tigrath  Sanga toka kata ya Iniho  kwani ndiye  aliye pata mafunzo hayo.

 

Bw. Tigrath kabla ya kuanza kuhudumia alitoa  maelezo kwa ufupi  kwa wananchi wa wake kuwa, chanjo hii ni ya vidonge na alisema  maana ya chanjo hii  ni ya kuzuia magonjwa nyemelezi pamoja na kuua minyoo mwilini, alitoa mfano mmoja wa magonjwa nyemelezi kama  kuvimba matezi.

 

Alisema chanjo hii hawaruhusiwi  watoto wadogo kupata  kwani vidonge hivi vina nguvu sana mwilini vinapo fanya kazi , na alisema upatapo chanjo hii huruhusiwi kutumia kinywaji cha aina ya kileo  kwa siku  uliyopata chanjo.

 

 

 

Tuesday, February 23rd, 2010

Watoto Yatima.

Na Evance Seth.

 

Jamii  imeshauriwa  kuwa na moyo wa kutoa  vitu mbalimbali  kwa watoto yatima  wanao lelewa katika vituo mbalimbali ili kuwa fariji  na wao kuto kuona  kama jamii imewasahau.

 

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete  Mh. Hawa Ng’humbi  wakati akikabidhi  msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani  zaidi  ya shilingi laki moja  kwa watoto wa kituo cha yatima  cha Bulongwa  Lengo la ziara yake hiyo  ni kuona  kituo hicho  pamoja kuelewa  historia yake  na kuelewa kinaendeshwaje.

 

Akipokea  msaada wa vitu hivyo  mmoja wa watumishi  wa kituo hicho  amesema kituo hicho  kinahitaji msaada mkubwa  wa watu wa serikari  kwa ujumla  ili kiweze kujiendesha chenyewe kwani kwa sasa kinamtegemea  mzungu  mmoja  ambaye kwa sasa ni mzee anayeitwa  SISTER ANNA.

 

Mh.  Mkuu wa wilaya  pia aliwafariji watoto wanaolelewa  katika kituo hicho  ambacho kina watoto thelathini na miongoni  mwao  watoto sita  wanaishi na virusi vya UKIMWI

 

Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya  aliongozana  na  Diwani wa kata ya Bulongwa Bw. Estomih Mahenge, M/K  umojwa wa wanawake Tanzania wilaya ya Makete   na Bi. Erika Sanga,  pamoja na  Israel Green  Kutoka  kituo cha polisi  makete.

 

Tuesday, February 23rd, 2010

Ujenzi wa Zahanati Unyagala.

 

Na Evance Seth.

 

Zaidi ya shilingi milioni hamsini na saba  pointi  nane zinatarajia kutumika  kwa ajili ya ujenzi wa  zahanati ya Unyangala   na Igumbilo  katika kipindi cha  mwaka  2009-2010 wilayani Makete.

Akizungumza  mratibu wa  mfuko wa maendeleo  ya jamii  wilayani Makete  Bi Jaklini Mroso  ameeleza kuwa fedha hizo  zitatumika kwa ajili ya ununuzi  wa vifaa vya ujenzi  pamoja na nguvu za wananchi  zitahitajika  kukamilisha miradi  hiyo kwa wakati.

Naye katibu wa  zahanati ya Unyangala  Bw. Boaz Sanga   pamoja na mtunza hazina  Bw. Erasto Mvela wamesema  kuwa msaada huo  umekuja kwa wakati  kwao kwani wamekuwa wakitumia muda mwingi  kuwa peleka wagonjwa  katika  zahanati ya Utengule ambapo ni mbali.

Mfuko wa maendeleo ya jamii   TASAF  wilayani Makete  umekuwa mkombozi  kwa wananchi wengi  wilayani Makete hasa vijijini kwa kusaidia misaada mbalimbali ambayo wamekuwa wakiibua  kupitia mikutano ya hadhara, aidha kufuatia hali , katibu  wa mradi  wa ujenzi  wa zahanati  Igumbilo  Bw. Godfrey Sanga  ameeleza  kuwa zahanati hiyo  kwa sasa ipo hatua ya mwisho na ameshukuru  TASAF kwa ufaddhili  wa mradi  huo  na  amewataka wananchi  kuendelea kuunga mkono  jitihada  zinazo fanywa  na TASAF  wilayani makete.

 

 

Monday, February 22nd, 2010

Mnada wa Ng’ombe.

 

Na Evance Seth.

 

Mnada wa mifugo  uliopo katika kijiji cha isapulano kata ya  Iwawa  ulioanza kujengwa mwaka  2009-2010 kwa ufadhili wa DADS   NA  DADPS  pamoja na nguvu za wananchi  ulioghalimu kiasi cha  shilingi  milioni kumi na nne na thelathini na nane elfu  14,380,000 umezinduliwa .

Uzinduzi wa mnada huo  umefanywa na mgeni rasimi  ambaye  ni mbunge wa wilaya ya makete MH BINILITI SAATANO MAHENGE  ambapo amewatakia wananchi  wa kijiji cha Isapulano na wananchi wa wilaya  makete  kwa ujumla kuutumia  mnada huo  ili kujiongezea kipato.

Aidha ameendelea kusema wananchi wote wanatakiwa  kuonesha upendo kwa wageni  watokao nje ya makete kwa kuto wakatisha tama kwa kuwaibia mali zao pindi  wanapo kuja kwenye mnada huo. Na  ameeleza mafanikio yaliyo patikana katika  awam ya nne ya uongozi  kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu  kwa wakazi wa wilaya ya makete  ambayo ni kufufua  zao la pareto pamoja na elimu ambapo kila kata  kumejengwa  shule za sekondari na wanafunzi wengi kufanikiwa kujiunga na elimu ya sekondari.

Katika sherehe za uzinduzi wa mnada huo MH mahenge aliongozana na mwenyekiti  wa Halmashauri  wa wilaya ya makete  ambaye pia  ni diwani wa kata ya Iwawa MH ONO SIKUNALA NKWAMA , mtendaji  Iwawa  KIWONE ,  AFISA KILIMO NA MIFUGO WA WILAYA BW ERNEST MKONGO pamoja na watalam wake.  Aidha changamoto kubwa  inayo ukabili mnada huo  ubovu wa barabara inayotoka  makete kwenda kijiji hapo ambayo wakati  wa masika haipitiki kwa uraisi pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya maji ambapo  kwa suala  la maji MH ONA nkwama ametoa liri mbili za bomba kwa ajili ya kusogeza  maji eneo la mnada  na suala  barabara kuahidi kushughulikia  ipitike muda wote.

 

Wakiongea kwa nyakati tofauti  wananchi wa kijiji hicho  wameonekana kufurahishwa na  na mnada ambao  utakuwa ukifanyika  mara mbili kwa mwezi tarehe kumi na tano na tarehe thelathini ya kila mwezi na kusema mifugo yote itauzwa  mnadani  ili kupata soko la uhakika  na si  la kuuzia mitaani.

 

                                    

Monday, February 22nd, 2010

Semina ya usimamizi wa mitihani ya darasa la Saba.

 

Na Evance Seth

 

Semina ya maelekezo  kuhusu  usimamizi wa mtihani  wa taifa  wa kuhitimu elimu ya msingi iliyo fanyika  katika  ukumbi wa Halimashauri ya wilaya ya makete.

 

Akinzungumza katika semina hiyo mkuu wa wilaya ya makete Bi HANA HUMBI  amesema  wasimamizi wanatakiwa  kuepuka vishawishi  kama vile rushwa  katika  zoezi hilo la usimamizi.

Alisema kuwapa watoto mtihani au majibu  ni kujenga  Taifa lenye watu wajinga  wasio na elimu wala  taaluma na kusema  yeyote atakaye gundulika  kufanya hivyo  atawajibika kisheria.

Akifunga semina hiyo Mkurugenzi  wa Halmashauri ya wilaya ya makete  Bi IMELDA ISHUZA  ametaka wasimamizi hao wa mtihani kuwa na upendo  kwa watoto  kwa kuwaelekeza vizuri  pale wanapo hitaji msaada  wa msimamizi.

 

Monday, February 22nd, 2010

Mafunzo ya CUAMM.

 

 Na Evance Seth

 

Katika wilaya ya makete  kuna shirika moja lisilo la kiserikali linaloitwa CUAMM linalotokea mkoani Iringa.

 

Shirika hilo linajishughulisha na  mambo  ya upimaji VCT . Na shirika hilo liliomba kufanya  kazi na mashirika mengine yaliyopo katika wilaya ya makete yanayo jishughulisha  na  mambo ya upimaji.

 

Pia shirika hilo lilitoa mafunzo  mbalimbali yakiwemo mafunzo ya;

1. UANDIKAJI WA RASMU NA MRADI

2. UTAFUTAJI WA VYANZO VYA FEDHA

3. UFUATILIAJI  NA TATHIMINI

 

Mashirika yaliyo shiliki mafunzo hayo ni1.MAKEYODENI , PIUMA, MAWATA5, LCCB, FEMA, IDYDC, SUMASESU, MAHEPO na  MASUPHA.

Na kila shirika liliwakilisha viongozi wane. Na mafundisho hayo  yaliendeshwa  na  WILLIAM YOTHAM -    UNV   na ABRAHAM   SANGA - CHAC.

 

Na  mafunzo hayo  yalifungwa na FLORA  NSEMWA  toka shirika la CUAMM  na kuagana  na kutakiana safari njema pamoja na utendaji wa kazi njema.

 

Wednesday, February 17th, 2010

Mtandao wa vijana Makete.

 

Na Evance Seth.

 

Katika Wilaya ya Makete kuna mtandao  mmoja unajishughulisha na vijana unaojulikana kwa jina la MAKEYODEN.

 

Mtandao huo uliamua kufanya kikao cha viongozi wa mtandao tarehe 22/01/2010 na kujadili malengo mbalimbali ya kufanya  2010-2013, na malengo hayo ni kama

 

1.KUBORESHA UONGOZI  ni kufanya marekebisho katiba ya makeyoden, kuandika sera kanuni na taratibu za makeyoden, kanuni za utendaji na uendeshaji , kanuni na taratibu za fedha na kanuni za ustawi na mahusiano na kuendesha vikao vya kamati kuu na mkutano mkuu.

 

2.KUBORESHA UTENDAJI ni kuajili watendaji wa ofisi kuu, kumaliza  ujenzi wa ofisi ya mtandao na vituo vya kata, kununua  samani  na vitendea kazi, kuendesha vikao vya utendaji na  kuanzisha tovuti na internet  ya makeyoden.

 

3.KUBORESHA  MAHUSIANO NA USHIRIKIANO BAINA YA MAKEYODEN NA WADAU WENGINE  ni kuandaa utambulisho wa  shughuli za makeyoden kuandaa orodha ya  wadau mbalimbali, kusambaza utambulisho wa makeyoden kwa njia mbalimbali na kuhudhulia matukio  ya wadau mbalimbali.

 

4.KUENDELEZA SHUGHULI ZA MAKEYODENI ZILIZOPO ni kuhimiza  umaliziaji wa vituo vya kata  tisa , kusaidia vituo saba vilivyokamilika vianze vianze utekelezaji wa mipango na  kukamilisha  usajili wa redio na kutayarisha mpango wa kazi na wa  kujitegemea  wa redio na kuongeza  nguvu  ya kudhibiti maambukizi dhidi ya ukimwi.

 

Kikao hicho kilifanyika  na viongozi wa mtandao  ambao  ni

1.       NAHAMAN SANGA  - MWENYEKITI

2.       JUMA  SINENE  - KATIBU

3.       EMANUEL SANGA  - MWASIBU

4.       FRANCISKO  SIGARA - MJUMBE

5.       SALEHE  NGULO  - MJUMBE

 

Na mwisho viongozi hao walihitimisha kikao  kuagana na kutakiana safari njema.