Monday, February 22nd, 2010

Mnada wa Ng’ombe.

 

Na Evance Seth.

 

Mnada wa mifugo  uliopo katika kijiji cha isapulano kata ya  Iwawa  ulioanza kujengwa mwaka  2009-2010 kwa ufadhili wa DADS   NA  DADPS  pamoja na nguvu za wananchi  ulioghalimu kiasi cha  shilingi  milioni kumi na nne na thelathini na nane elfu  14,380,000 umezinduliwa .

Uzinduzi wa mnada huo  umefanywa na mgeni rasimi  ambaye  ni mbunge wa wilaya ya makete MH BINILITI SAATANO MAHENGE  ambapo amewatakia wananchi  wa kijiji cha Isapulano na wananchi wa wilaya  makete  kwa ujumla kuutumia  mnada huo  ili kujiongezea kipato.

Aidha ameendelea kusema wananchi wote wanatakiwa  kuonesha upendo kwa wageni  watokao nje ya makete kwa kuto wakatisha tama kwa kuwaibia mali zao pindi  wanapo kuja kwenye mnada huo. Na  ameeleza mafanikio yaliyo patikana katika  awam ya nne ya uongozi  kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu  kwa wakazi wa wilaya ya makete  ambayo ni kufufua  zao la pareto pamoja na elimu ambapo kila kata  kumejengwa  shule za sekondari na wanafunzi wengi kufanikiwa kujiunga na elimu ya sekondari.

Katika sherehe za uzinduzi wa mnada huo MH mahenge aliongozana na mwenyekiti  wa Halmashauri  wa wilaya ya makete  ambaye pia  ni diwani wa kata ya Iwawa MH ONO SIKUNALA NKWAMA , mtendaji  Iwawa  KIWONE ,  AFISA KILIMO NA MIFUGO WA WILAYA BW ERNEST MKONGO pamoja na watalam wake.  Aidha changamoto kubwa  inayo ukabili mnada huo  ubovu wa barabara inayotoka  makete kwenda kijiji hapo ambayo wakati  wa masika haipitiki kwa uraisi pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya maji ambapo  kwa suala  la maji MH ONA nkwama ametoa liri mbili za bomba kwa ajili ya kusogeza  maji eneo la mnada  na suala  barabara kuahidi kushughulikia  ipitike muda wote.

 

Wakiongea kwa nyakati tofauti  wananchi wa kijiji hicho  wameonekana kufurahishwa na  na mnada ambao  utakuwa ukifanyika  mara mbili kwa mwezi tarehe kumi na tano na tarehe thelathini ya kila mwezi na kusema mifugo yote itauzwa  mnadani  ili kupata soko la uhakika  na si  la kuuzia mitaani.

 

                                    

Leave a Reply