Tuesday, February 23rd, 2010

Ujenzi wa Zahanati Unyagala.

 

Na Evance Seth.

 

Zaidi ya shilingi milioni hamsini na saba  pointi  nane zinatarajia kutumika  kwa ajili ya ujenzi wa  zahanati ya Unyangala   na Igumbilo  katika kipindi cha  mwaka  2009-2010 wilayani Makete.

Akizungumza  mratibu wa  mfuko wa maendeleo  ya jamii  wilayani Makete  Bi Jaklini Mroso  ameeleza kuwa fedha hizo  zitatumika kwa ajili ya ununuzi  wa vifaa vya ujenzi  pamoja na nguvu za wananchi  zitahitajika  kukamilisha miradi  hiyo kwa wakati.

Naye katibu wa  zahanati ya Unyangala  Bw. Boaz Sanga   pamoja na mtunza hazina  Bw. Erasto Mvela wamesema  kuwa msaada huo  umekuja kwa wakati  kwao kwani wamekuwa wakitumia muda mwingi  kuwa peleka wagonjwa  katika  zahanati ya Utengule ambapo ni mbali.

Mfuko wa maendeleo ya jamii   TASAF  wilayani Makete  umekuwa mkombozi  kwa wananchi wengi  wilayani Makete hasa vijijini kwa kusaidia misaada mbalimbali ambayo wamekuwa wakiibua  kupitia mikutano ya hadhara, aidha kufuatia hali , katibu  wa mradi  wa ujenzi  wa zahanati  Igumbilo  Bw. Godfrey Sanga  ameeleza  kuwa zahanati hiyo  kwa sasa ipo hatua ya mwisho na ameshukuru  TASAF kwa ufaddhili  wa mradi  huo  na  amewataka wananchi  kuendelea kuunga mkono  jitihada  zinazo fanywa  na TASAF  wilayani makete.

 

 

One Response to “Ujenzi wa Zahanati Unyagala.”


  1. Timin Lwilla says:

    I have been following with keen interest articles published in your blog.
    Big up PIUMA staff and reporters. This really explains the slogan “Makete- wilaya ya kazi”

    Timin Lwilla
    Lugoda hospital
    P O Box 40
    MUFINDI

Leave a Reply