Tuesday, February 23rd, 2010

Watoto Yatima.

Na Evance Seth.

 

Jamii  imeshauriwa  kuwa na moyo wa kutoa  vitu mbalimbali  kwa watoto yatima  wanao lelewa katika vituo mbalimbali ili kuwa fariji  na wao kuto kuona  kama jamii imewasahau.

 

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete  Mh. Hawa Ng’humbi  wakati akikabidhi  msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani  zaidi  ya shilingi laki moja  kwa watoto wa kituo cha yatima  cha Bulongwa  Lengo la ziara yake hiyo  ni kuona  kituo hicho  pamoja kuelewa  historia yake  na kuelewa kinaendeshwaje.

 

Akipokea  msaada wa vitu hivyo  mmoja wa watumishi  wa kituo hicho  amesema kituo hicho  kinahitaji msaada mkubwa  wa watu wa serikari  kwa ujumla  ili kiweze kujiendesha chenyewe kwani kwa sasa kinamtegemea  mzungu  mmoja  ambaye kwa sasa ni mzee anayeitwa  SISTER ANNA.

 

Mh.  Mkuu wa wilaya  pia aliwafariji watoto wanaolelewa  katika kituo hicho  ambacho kina watoto thelathini na miongoni  mwao  watoto sita  wanaishi na virusi vya UKIMWI

 

Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya  aliongozana  na  Diwani wa kata ya Bulongwa Bw. Estomih Mahenge, M/K  umojwa wa wanawake Tanzania wilaya ya Makete   na Bi. Erika Sanga,  pamoja na  Israel Green  Kutoka  kituo cha polisi  makete.

 

One Response to “Watoto Yatima.”


  1. malila says:

    Namshukuru sana huyo Mkuu wa wilaya aliyethubutu kufika na kuwajulia heri wadogo zetu hao. Kama watu wengi wangetoa cho chote walicho nacho nadhani mzigo kwa sister Anna ungepungua.

Leave a Reply