Friday, February 26th, 2010

Watumishi wa UMA

 

Na Evance Seth.

 

Ofisi ya Rais  menejimenti ya utumishi wa UMA inakusudia kuwa watumishi  wa serikari  kuanza  kupokea mishahara  dirishani  badara ya kuwaingizia  katika akaunti zao.

Kauli hiyo imetolewa  na waziri wa  Nchi  ofisi ya Rais  menejimenti ya utumishi wa uma Mh. Hawa Ghasia alipokuwa akiwahutubia watumishi  wa halmashauri ya wilaya ya makete. Alisema  ofisi yake inafikilia  kufanya hivyo kutokana na  kulipa mishara hewa ya watumishi.

 

Mpango huo  wa watumishi kupokea dirishani  utasaidia kuondoa udanganyifu ambao serikari inalipa mishahara hewa na kusababisha  serikari hasara kubwa. Amesema katika kupitia  utafiti  uliofanywa na wizara yake imebaini katika sekta  ya afya  na sekta ya elimu  baadhi ya watumishi  wanalipwa  mishahara hewa.

Mh. Ghasia  alikuwa  katika ziara yake ya  kutoa semina  kwa halmashauri ya wilaya ya makete inyohusu mabadiliko  mahali pa kazi  na utawala bora  ambapo hii leo  akitoka hapa anaelekea  wilayani Ludewa.

Mikoa mingine ambayo amepitia  kutoa semina hiyo ni  MANYARA, KIGOMA, LINDI, MTWARA, PWANI , IRINGA  na akimalizia SINGIDA.

One Response to “Watumishi wa UMA”


  1. joseph says:

    Jamani yaani tumeshindwa kabisa kutumia kumbukumbu zinazokusanywa kila mwaka kwa kujua ni nani yupo kazini na nani hayupo kazini ili kuondoa watumishi hewa na badala yake tunarudi tena kule mwaka arobaini na saba kwenye tatizo la mishahara kucheleweshwa na kuongeza wimbi la ujambazi kwenye swala zima la mishahara ya watumishi.
    Kweli safari ni ndefu kwenye swala la technolojia na kuna kazi kwenye hii nchi bila mabadiliko ya kweli safari bado ni ndefu sana wandugu.

Leave a Reply