Archive for March, 2010

Wednesday, March 31st, 2010

Matokeo ya kidato cha Nne.

 Na Evance Seth.

Kumetokea mabadiliko  katika kiwango cha kufaulu kwa wanafunzi  tofauti na mwaka  uliopita  katika shule ya sekondari  Iwawa iliyopo wilayani Makete.

 Akizungumuza  mkuu wa  shule hiyo  Bw OMATH SANGA  amesema jumla ya  wanafunzi mia moja kumi na nane waliofanya mtihani wa Taifa,  wanafunzi wawili wamepata  divisheni one , wanafunzi  kumi na tatu wamepata divisheni two  na wanafunzi thelathini na saba wamepata divisheni three, wakati wanafunzi wane wamepata divisheni ziro.

Mwalimu OMATH SANGA  amesema mpaka sasa  hajapata tathimini  ya kujua  shule yake  imepanda kiasi gani  au imeshuka  kiasi gani  kulingana na shule zingine ,na  hivyo mwisho  amewaomba wananchi  kutambua  umuhimu wa kuwatafutia nafasi za masomo watoto wao.

 

Wednesday, March 31st, 2010

Michezo

Na Evance Seth

Katika  uwanja wa Luvanyina uliopo kata ya Bulongwa , kumefanyika mechi ya kirafiki  ya mpira wa miguu kati ya shule ya sekondari ya mwakavuta na shule ya sekondari kipagalo.

Kwani  shule hizo zimekutana  ikiwa mwakavuta sekondari ni kongwe  ilianza mwaka 1992 na  Kipagalo ilanza mwaka 2007.

Mchezo huo ulianza  mnamo muda wa saa kumi kamili alasili na mchezo huo uliendeshwa na refarii Bw Timu Sanga. Mnamo dakika ya kumi na mbili  Kipagalo walianza kuandika goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wao Noah Sanga huku Mwakavuta wakiwa hawajapata kitu, mpira uliendelea  huku mwakavuta  wakiendelea kushambuliwa  na dakika ya  thelathini na saba  Kipagalo walifunga goli la pili kupitia kwa mshambuliaji wao Juma Nsemwa , hadi mpira unakwenda mapumziko  Kipagalo mbili na Mwakavuta  sifuri.

Kipindi cha pili kilianza kwa nguvu sana pande zote mbili,  huku Mwakavuta  Sekondari  wakishambulia kwa nguvu sana goli la Kipagalo  na dakika ya  hamsini na nne mwakavuta wafunga goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wao Partson Mbogela na dakika  ya sitini na tisa  Mwakavuta walifunga goli la pili kupitia kwa mchezaji wao Frank Fungo lililo fungwa kwa njia ya faulo , na Mwakavuta walizidi kuliandama goli la Kipagalo  huku kipagalo wakizidi kuchoka  , mnamo dakika ya  themanini na tatu mwakavuta walifunga goli la tatu kupitia kwa mchezaji wao Regi Sanga  na dakika ya tisini na mbili za nyongeza  mwakavuta walifunga goli la nne kupitia kwa mchezaji wao  yuleyule  Frank Fungo   hadi mpira unamalizika  Mwakavuta Sekondari nne na Kipagalo Sekondari mbili.

Mwalimu wa  michezo wa shule ya Sekondari ya Kipagalo  alisema  kwamba  nimekubali matokeo  kwani mpira wa miguu una matokeo ya aina tatu  kufunga , kufungwa na kutoa sale , naye mwalimu wa Mwakavuta  sekondari alisema kwamba nimefurahi sana na ushindi  kwani kipindi cha kwanza tulitangulizwa goli mbili bila  nilipata tabu kwani kwa sasa nina jiandaa  wiki ijayo  kuwapeleka  vijana  wangu  kucheza na shule ya Sekondari Ipelele.

 

Wednesday, March 31st, 2010

Shamba la Ng’ombe Kitulo.

Na Evance Seth.

Akisoma taarifa ya shamba hilo kwa mkuu wa mkoa wa Iringa  MH MOHAMEDI ABDILAZIZI  mwakilishi wa  shamba hilo  amesema lengo la shamba hilo  ni kuongeza ng’ombe wazalishaji  pamoja na kufufua zaidi  ya hekta hamsini  za malisho kwa kutoa  magugu na kuweka mbolea.

Amesema kwa kufanya hivyo  utaboresha  uzalishaji mkubwa wa kiwanda  hicho kwa upande  wa ulaji wa ng’ombe  wenye afya na uzito  wa kutosha punde  unapofika wakati wa kuuzwa. Amesema mbali na  hatua hiyo  pia shamba lina mpango  wa kuongeza   ng’ombe  katika kundi la ukamilishaji kufikia ng’ombe  mia mbili ili kupata ndama bora  kwa ajili ya kusambaza kwa wakulima.

Malengo mengine ni  kuboresha upatikanaji wa maji hasa wakati wa kiangazi  pamoja na kutengeneza njia za ndani ya shamba hili  zipitike wakati wote  na kumalisha  ukarabati wa nyumba za watumishi pamoja na kuendelea  kuingiza umeme kwenye nyumba za watumishi.

Wednesday, March 31st, 2010

Mvua za ezua Mapaa.

Na Evance Seth.

 

Katika wilaya ya makete  Tarafa ya Bulongwa na Magoma kata ya Ipelele na kata ya Kipagalo kumetokea na hasara kubwa itokanayo na mvua.

 

Viongozi wa tarafa  zote mbili wakimweleza  mwenyekiti wa Halmashauri wa wilaya ya makete Mh Ona Skunara Nkwama walisema wiki hii mvua  kubwa sana  imenyesha ikiambatana na upepo mkali imesababisha maafa ya nyumba za wananchi pamoja na shule moja ya msingi  kuezuriwa.

 

Mwenyekiti wa halmashauri  wa wilaya wa makete  alifika sehemu zote za matukio na kutoa pole kwa wananchi wa tarafa zote mbili  na kuahidi kutoa mchango  wa bati kila nyumba .

 

Na wananchi   walimshukuru mwenyekiti wa halmashauri na kusema  tunamshukuru mungu kwani hakuna aliyepata jeraha wala kufa. Na mwisho  mwenyekiti huyo aliwaambia wananchi hao kuwa  mvua zinapo nyesha wazazi tujitahidi kuwa nyumbani kwenye familia zetu kwa ajili ya msaada endapo linatokea swala kama hili kwani mvua bado zinaendelea kunyesha.

 

 

 

 

 

Wednesday, March 31st, 2010

Maisha katika kipindi cha mtazamo.

Na Evance Seth.

Imefahamika  kuto jipenda  kwa baadhi ya akina  mama na kutokuwa na  ubunifu  wa miradi ndio  sababisho  kubwa  kuwafanya wanaume  kuleta visa  katika ndoa zao.

Wakichangia   dondoo  za maisha  katika kipindi  cha mtazamo  cha Kitulo FM Redio  , baadhi ya wachangiaji  hao wamesema  matatizo hayo katika ndoa  yanasababishwa na wanawake wenyewe kwa kukosa ubunifu katika  ndoa zao.

Aidha wamesema  wakati mwingine  baadhi ya wanawake  hujisahau mara wanapokuwa  ndani  ya ndoa zao  pamoja na kuacha  kuboresha usafi katika familia zao. Pia imeonekana  baadhi ya akina baba  wamekosa elimu ya ndoa  pamoja na uvumilivu.

Kipindi cha mtanzamo hurushwa kila jumatatu na ijumaa  kuanzia saa tatu kamili asubuhi  mpaka  saa saba kamili mchana  katika  studio za KITULO FM RADIO.

Wednesday, March 31st, 2010

Uogeshaji wa Ng’ombe.

 

Na Evance Seth

 

Katika kata ya Iniho wamejipatia Josho  kwa ajili ya kuogeshea ng’ombe. Afisa mifugo wa kata ya hiyo  Bw. Nova  alisema kwamba  tumepata josho hili kwa malengo ya kuogeshea ng’ombe  ili kuua wadudu kama kupe na nk.

 

Pia alisema josho hili  ni letu sisi wenyewe kinachotakiwa  kila mwananchi mwenye ng’ombe  anapokuja kuogesha  atalipia shilinngi mia moja kwa kila ng’ombe na hizo fedha zitafanya kazi ya kutengenezea josho pale linapo halibika na kununulia dawa za kuogeshea ng’ombe.

 

Na mwisho alisema kuwa itapangwa ratiba ya kuogesha ng’ombe kwa vijiji  kwani kwa mwezi ni mara moja na kwa yule ambaye ataonekana ajaogesha ng’ombe atachukuliwa hatua ya kisheria