Maisha katika kipindi cha mtazamo.
Na Evance Seth.
Imefahamika kuto jipenda kwa baadhi ya akina mama na kutokuwa na ubunifu wa miradi ndio sababisho kubwa kuwafanya wanaume kuleta visa katika ndoa zao.
Wakichangia dondoo za maisha katika kipindi cha mtazamo cha Kitulo FM Redio , baadhi ya wachangiaji hao wamesema matatizo hayo katika ndoa yanasababishwa na wanawake wenyewe kwa kukosa ubunifu katika ndoa zao.
Aidha wamesema wakati mwingine baadhi ya wanawake hujisahau mara wanapokuwa ndani ya ndoa zao pamoja na kuacha kuboresha usafi katika familia zao. Pia imeonekana baadhi ya akina baba wamekosa elimu ya ndoa pamoja na uvumilivu.
Kipindi cha mtanzamo hurushwa kila jumatatu na ijumaa kuanzia saa tatu kamili asubuhi mpaka saa saba kamili mchana katika studio za KITULO FM RADIO.
