Matokeo ya kidato cha Nne.
Na Evance Seth.
Kumetokea mabadiliko katika kiwango cha kufaulu kwa wanafunzi tofauti na mwaka uliopita katika shule ya sekondari Iwawa iliyopo wilayani Makete.
Akizungumuza mkuu wa shule hiyo Bw OMATH SANGA amesema jumla ya wanafunzi mia moja kumi na nane waliofanya mtihani wa Taifa, wanafunzi wawili wamepata divisheni one , wanafunzi kumi na tatu wamepata divisheni two na wanafunzi thelathini na saba wamepata divisheni three, wakati wanafunzi wane wamepata divisheni ziro.
Mwalimu OMATH SANGA amesema mpaka sasa hajapata tathimini ya kujua shule yake imepanda kiasi gani au imeshuka kiasi gani kulingana na shule zingine ,na hivyo mwisho amewaomba wananchi kutambua umuhimu wa kuwatafutia nafasi za masomo watoto wao.
