Wednesday, March 31st, 2010

Michezo

Na Evance Seth

Katika  uwanja wa Luvanyina uliopo kata ya Bulongwa , kumefanyika mechi ya kirafiki  ya mpira wa miguu kati ya shule ya sekondari ya mwakavuta na shule ya sekondari kipagalo.

Kwani  shule hizo zimekutana  ikiwa mwakavuta sekondari ni kongwe  ilianza mwaka 1992 na  Kipagalo ilanza mwaka 2007.

Mchezo huo ulianza  mnamo muda wa saa kumi kamili alasili na mchezo huo uliendeshwa na refarii Bw Timu Sanga. Mnamo dakika ya kumi na mbili  Kipagalo walianza kuandika goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wao Noah Sanga huku Mwakavuta wakiwa hawajapata kitu, mpira uliendelea  huku mwakavuta  wakiendelea kushambuliwa  na dakika ya  thelathini na saba  Kipagalo walifunga goli la pili kupitia kwa mshambuliaji wao Juma Nsemwa , hadi mpira unakwenda mapumziko  Kipagalo mbili na Mwakavuta  sifuri.

Kipindi cha pili kilianza kwa nguvu sana pande zote mbili,  huku Mwakavuta  Sekondari  wakishambulia kwa nguvu sana goli la Kipagalo  na dakika ya  hamsini na nne mwakavuta wafunga goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wao Partson Mbogela na dakika  ya sitini na tisa  Mwakavuta walifunga goli la pili kupitia kwa mchezaji wao Frank Fungo lililo fungwa kwa njia ya faulo , na Mwakavuta walizidi kuliandama goli la Kipagalo  huku kipagalo wakizidi kuchoka  , mnamo dakika ya  themanini na tatu mwakavuta walifunga goli la tatu kupitia kwa mchezaji wao Regi Sanga  na dakika ya tisini na mbili za nyongeza  mwakavuta walifunga goli la nne kupitia kwa mchezaji wao  yuleyule  Frank Fungo   hadi mpira unamalizika  Mwakavuta Sekondari nne na Kipagalo Sekondari mbili.

Mwalimu wa  michezo wa shule ya Sekondari ya Kipagalo  alisema  kwamba  nimekubali matokeo  kwani mpira wa miguu una matokeo ya aina tatu  kufunga , kufungwa na kutoa sale , naye mwalimu wa Mwakavuta  sekondari alisema kwamba nimefurahi sana na ushindi  kwani kipindi cha kwanza tulitangulizwa goli mbili bila  nilipata tabu kwani kwa sasa nina jiandaa  wiki ijayo  kuwapeleka  vijana  wangu  kucheza na shule ya Sekondari Ipelele.

 

Leave a Reply