Mvua za ezua Mapaa.
Na Evance Seth.
Katika wilaya ya makete Tarafa ya Bulongwa na Magoma kata ya Ipelele na kata ya Kipagalo kumetokea na hasara kubwa itokanayo na mvua.
Viongozi wa tarafa zote mbili wakimweleza mwenyekiti wa Halmashauri wa wilaya ya makete Mh Ona Skunara Nkwama walisema wiki hii mvua kubwa sana imenyesha ikiambatana na upepo mkali imesababisha maafa ya nyumba za wananchi pamoja na shule moja ya msingi kuezuriwa.
Mwenyekiti wa halmashauri wa wilaya wa makete alifika sehemu zote za matukio na kutoa pole kwa wananchi wa tarafa zote mbili na kuahidi kutoa mchango wa bati kila nyumba .
Na wananchi walimshukuru mwenyekiti wa halmashauri na kusema tunamshukuru mungu kwani hakuna aliyepata jeraha wala kufa. Na mwisho mwenyekiti huyo aliwaambia wananchi hao kuwa mvua zinapo nyesha wazazi tujitahidi kuwa nyumbani kwenye familia zetu kwa ajili ya msaada endapo linatokea swala kama hili kwani mvua bado zinaendelea kunyesha.
