Nani Amsemee Dr. Jumbe?
Jackson Mbogela
Napenda kuungana na wanamakete wote na hasa wana PIUMA kusikitika juu ya msiba wa Dr. Jumbe Maphingo. Tukiwa kama wagonjwa wa UKIMWI ambao tunahitaji tiba ya mara kwa mara na ya uhakika, tunamhitaji daktari kuliko mtu yeyeyote. Kuuawa kwa Daktari ni kuuawa kwa wadau wa huduma ya afya na watu wanaoishi na VVU wote.
Nchini Tanzania Daktari mmoja kwa wastani anahudumia watu laki moja, kwa hiyo basi kuuawa kwa daktari mmoja ni sawa na kuuawa watu lakini moja na moja. Wanachama wetu wengi walitibia na Dr. Jumbe, na katika madaktari waliotoa tiba na huduma ya kuridhisha alikuwa ni Dr. Jumbe. Wanachama wetu walimpenda na walifanya naye kazi kwa ushirikiano mkubwa, kuuawa kwake ni pigo kubwa sio tu kwa Bulongwa bali ni kubwa zaidi kwetu sisi ambao tulimtegemea kila siku tunapoingia Klinik. Sisi kama wadau wa huduma katika hospitali ya Bulongwa tumeuawa pamoja na Dr. Jumbe.
Wanachama kadhaa wa PIUMA wameonyesha kusikitishwa na tatizo hili. Na tunadhani kanisa (KKKT), Dayosisi (DKK), pamoja Hospitali ya Bulongwa (BLH) wanahitajika kuwajibika kwa tukio hili. Nashangaa kuona viongozi wa hospitali akiwemo mganga Mkuu na mkuu wa chuo cha sayansi ya tiba Dr. John Mscheshi na Mtawala wa Hospitali Edward Masevella bado wanaitwa mganga mkuu na mkuu wa chuo na Mwingine mtawala. Walipaswa kujiuzuru siku nyingi sana ili kusaidia upelelezi utakao baini ukweli wa mambo na sababu zilizopelekea kifo cha Dr. Jumbe. Sio tu kujua ukweli lakini pita itasaidia vyombo vya dola kuweza kuwachukulia hatua watu wote waliohusika na kunyosha mikono yao, kutoa maneno yaliyopelekea Dr. Jumbe Kuuwawa kikatili.
Kanisa lingeweza kuunda tume ndogo itakayofanya uchunguzi wake (internal enquiry) na kubaini ukweli. Timu hiyo ya uchunguzi ionyeshe mianya ya uongozi na kiutendaji iliyopo BLH. Kwa mfano BLH inawajibika kwa DKK katika matatizo tu linapofika suala la pesa BLH inajitenga na uongozi wa DKK. Kwamfano hivi karibuni BLH wamepokea ufadhiri mkubwa kutoka Rapid Fund Envelop (RFE) ambao Dr. Jumbe alikuwa mratibu wake. Vyombo vya dola pamoja na tume ya uchunguzi ichunguze kama mahusiano ya Dr. Jumbe na watendaji wenzake wanaohusika na mfuko huu yalikuwa sawa sawa? Hasa siku za karibuni na kuuawa kwakwe Kama kulikuwa na dosari ningependekeza hapo pawe ndio pa kuanzia kutatua utata unaozingira kifo chake.
Kanisa halijataka kuchukua hatua za makusudi za kufanikisha upelelezi wa jambo hili. Dr. Jumbe hajatendewa haki. Awe alikuwa mbakaji au hapana, hakuna mtu ana ruhusa ya kuhukumu tena hukumu ya Kifo zaidi ya mahakama. Ningependekeza maandamano kwa wanamakete wanaoitakia huduma ya afya mema, yaitishwe maandamano yatakayokuwa na malengo mawili. 1. Kulaani kuuawa kwa daktari 2. Kuieleza dunia jinsi sisi tulivyoathirika na kifo chake, 3. Kulitaka kanisa lichukue hatua zaidi hasa kwa uongozi wa BLH kwa kushindwa kuwalinda madaktari. Mtu asimame amtetee Dr. Jumbe. Mtu asimame amsemee Dr. Jumbe.
Uwezo wa hospitali ya Bulongwa ya kutoa huduma bora umekuwa ukishuka kila siku. Hopsitali imekosa vitendea kazi muhimu, hospitali imekosa watalaam na huduma imekuwa ya ghari sana. Kama hakuna huduma bora na nafuu ya tiba athari zake ni kubwa na hata huweza kusababisha KIFO kwa watumiaji wa huduma hiyo.
PIUMA tunasimama leo na kudai haki za tiba Bora, Kanisa liwajibike kwa kifo cha Dr. Jumbe. PIUMA tunadai kuwa na huduma inayokidhi mahitaji ya wanachama wake. TUNATAKA TIBA BORA.

Asifiwe Malila says:
Nimejisikia vibaya baada ya kusoma tukio hili. Mungu peke yake anajua. Nina mipango ya kutembelea BLH na wageni fulani mwaka huu september, pengine nitasikia zaidi.
Kila ninapopata fursa ya kwenda Bulongwa nakutana na jambo baya, mara ya kwanza nilikutana na mzozo wa matumizi mabaya ya fedha na msukosuko ule ukaishia kumtoa Askofu, safari ya pili ndio niliyoonana na Ven Sanga na siku chache baada ya kuonana, Ven alifariki na sasa nakwenda huko,kifo cha Dr ni balaa lingine.