Watoto Yatima.
Na Evance Seth.
Jamii imeshauriwa kuwa na moyo wa kutoa vitu mbalimbali kwa watoto yatima wanao lelewa katika vituo mbalimbali ili kuwa fariji na wao kuto kuona kama jamii imewasahau.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Hawa Ng’humbi wakati akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani zaidi ya shilingi laki moja kwa watoto wa kituo cha yatima cha Bulongwa Lengo la ziara yake hiyo ni kuona kituo hicho pamoja kuelewa historia yake na kuelewa kinaendeshwaje.
Akipokea msaada wa vitu hivyo mmoja wa watumishi wa kituo hicho amesema kituo hicho kinahitaji msaada mkubwa wa watu wa serikari kwa ujumla ili kiweze kujiendesha chenyewe kwani kwa sasa kinamtegemea mzungu mmoja ambaye kwa sasa ni mzee anayeitwa SISTER ANNA.
Mh. Mkuu wa wilaya pia aliwafariji watoto wanaolelewa katika kituo hicho ambacho kina watoto thelathini na miongoni mwao watoto sita wanaishi na virusi vya UKIMWI
Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya aliongozana na Diwani wa kata ya Bulongwa Bw. Estomih Mahenge, M/K umojwa wa wanawake Tanzania wilaya ya Makete na Bi. Erika Sanga, pamoja na Israel Green Kutoka kituo cha polisi makete.

















