Archive for the ‘News’ Category

Wednesday, January 6th, 2010

Mkutano mkuu wa mwaka PIUMA.

Na Witness Ngumba.

Mkutano mkuu wa mwaka wa PIUMA umefanika tarehe 18/12/2009, mgeni rasmi wa mkutano alikuwa ni Mkuu wa Wilaya Bi. Hawa Ng’humbi, wageni wengine waliokuwepo ni pamoja na Joseph Chaula – DAS, Felician Chawala  - Ag. DMO, Hamza – ofisi ya DSO, Erica Sanga – Viti maalumu, Estomih Mahenge – Diwani bulongwa, Ambikile Mwaihola – Afisa Tarafa, Clemence – WEO Bulongwa, Edward Masevela – Ad. BLH, Benitho Ngailo - MASUPHA wanachama wa PIUMA waliokuwa wamehudhuria walikuwa 75  na wengine wengi.

Ilisomwa taarifa ya Katibu na Katibu mkuu pamoja na taarifa ya fedha ilisomwa na Mtunza Hazina wa PIUMA.

Mkuu wa Wilaya alitoa salamu na shukrani nyingi kwa shirika la PIUMA kwa kazi nyingi zinazofanywa na shirika hili hasa  dhidi ya mapambano ya UKIMWI. Aliendelea kusema kuwa alipokuwa alifika katika Wilaya ya Makete shirika ambalo limekuwa likijishughulisha na masuala ya upimaji ni shirika la PIUMA , aliwaasa wanachama wa PIUMA kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya faida za kupima pamoja na hasara za kutokupima afya zao.

Pamoja na hayo Mkuu wa Wilaya alishukuru kwa ujenzi wa jengo la PIUMA ambalo tunategemea kuwa litakuwa Zahanati ya PIUMA hapo baadaye na kuwaahidi kuwa atachangia kiasi cha sh. 200,000/= kwa ajili ya ujenzi wa jengo la PIUMA.

 

wanachama wa PIUMA wakiwa kwenye mkutano

wanachama wa PIUMA wakiwa kwenye mkutano

 

Mkuu wa Wilaya Bi. Hawa Ng'humbi akitoa hotuba

Mkuu wa Wilaya Bi. Hawa Ng'humbi akitoa hotuba

 

Katibu mkuu akisoma taarifa ya mwaka.

Katibu mkuu akisoma taarifa ya mwaka.

 

Ag. DMO akitoa salamu.

Ag. DMO akitoa salamu.

 

DAS- Makete akitoa salamu

DAS- Makete akitoa salamu

Monday, December 21st, 2009

Wanachama wa PIUMA wakifanya usafi kwenye jengo lao.

Na Witness Ngumba

 

Wanachama wa PIUMA wiki iliyopita walikuwa wanafanya usafi kwenye jengo lao kwa ajili ya maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka.

 

Akizungumza katibu mkuu Bi. Anna Mwinuka alisema kuwa usafi utafanywa na wanachama walio katika vijiji vya karibu na jengo. Jumla ya wanachama waliofika kwenye usafi walikuwa 17

 

Usafi uliofanyika ulikuwa ni ndani ya jengo na usafi wa nje ya jengo utafanywa kwa siku nyingine na wanachama wote wa PIUMA baada ya jengo lote kuisha.

 

 

 

WanaPIUMA wakifanya usafi

WanaPIUMA wakifanya usafi

Dr. zin zin nae akiwa ndani ya usafi

Dr. zin zin nae akiwa ndani ya usafi

Afisa mtendaji nae akiwa ndani ya kazi

Afisa mtendaji nae akiwa ndani ya kazi

Thursday, December 3rd, 2009

Siku ya UKIMWI duniani 1.12.2009

Na Witness Ngumba

Siku ya UKIMWI duniani ni siku ambayo huwa inaadhimishwa kila mwaka Tanzania nzima kwa ajili ya kuwakumbuka watu waliokufa kwa ugonjwa wa UKIMWI pamoja na wanaoishi na Virusi vya UKIMWI.

 

Kwa Wilaya ya Makete Tarafa  ya Bulongwa Siku hii  imeadhimishwa katika tarafa ya Bulongwa kijiji cha kitula ikiwa ni muunganiko wa kata mbili, kata ya Kipagalo na kata Bulongwa. Sherehe hii ilianza rasmi saa 6:00 mchana ikiongozwa na katibu Tarafa wa Bulongwa Bw. Ambikile Mwaihola, Mgeni rasmi wa sherehe hii alikuwa ni Mh. Diwani Estomih Mahenge. Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa “UHURU NI UWEZO

 

Mgeni rasmi aliwashukuru watu wote wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kwa kufuata taratibu zote za dawa pamoja na mashirika yanayosaidia kutoa huduma ikiwemo PIUMA.

Katika sherehe hii PIUMA waliandaa kwaya, igizo pamoja na kugombea umiss Uhuru Bulongwa, aliyeongoza kwa umiss alikuwa ni Rehema Nyamule, akifuatiwa na  Wema Sanga, Anna Mwinuka,Tulingila Sanga.

Mh. Diwani akitoa zawadi kwa mamiss PIUMA

Mh. Diwani akitoa zawadi kwa mamiss PIUMA

 

 

 Miss uhuru PIUMA 2009 ni Rehema nyamule.

Miss uhuru PIUMA 2009 ni Rehema nyamule.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Wednesday, November 18th, 2009

Mradi wa Rafiki wa Vijana

Na Evance Seth

 

Vijana  wa kijiji cha Ivalalila wametakiwa kutumia  HUDUMA  YA RAFIKI KWA VIJANA ili waweze kujitambua.

 

Hayo yamesemwa na  Daktari Bw. Jonathan  Kitundu wakati akitoa elimu  ya Rafiki Kijana iliyo fanyika katika kijiji hicho cha Ivalalila. Daktari Kitundu amesema huduma ya Rafiki inatolewa kwa vijana  ili kukuidhi mahitaji  aliyo nayo kwa muda mwafaka.

 

Amesema vijana wanatakiwa kufika  katika Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya  na vituo vya vijana  kwa ajili ya huduma hiyo  na kuwataka kupima afya zao kwa ajili ya kupanga malengo yao ya baadaye.

 

Na mwisho Katibu wa vijana  tawi  la Ivalalila Bw Agano Sanga  amesema elimu waliyo ipata  itawasaidia vijana kuepukana na  maambukizi ya virusi vya ukimwi hususani katika HUDUMA YA RAFIKI KWA VIJANA.

Wednesday, November 18th, 2009

Walemavu na Mikakati

Na Evance Seth

 

Katika wilaya ya Makete kuna kikundi cha walemavu  kilichopo hapahapa Makete kinacho itwa (KICHAWAMA)  kimepanga  mipango madhubuti juu ya kuijengea uwezo  jamii ya watu wenye matatizo  ya ulemavu kwa kutoa elimu ya ufundi stadi pamoja  na kutoa elimu  kwa jamii kutambua  haki za walemavu wa aina zote.

 

Akizungumuza na mwandishi wa habari Mwenyekiti wa kikundi  cha walemavu  Makete Bw. Niko Mbwilo  amesema watu wenye matatizo ya  ulemavu wamefikia hatua  ya kukata tama kutokana na jamii kuona kama  walemavu hawawezi lolote.

 

Bw Mbwilo ameeleza matatizo yanayo wakabili  kuwa ni pamoja na  kukosa nyumba  ya kufundishia  pamoja na  chakula kwa walemavu ambao wangependa  kujifunza fani mbalimbali.

 

Pia amesema  kama kikundi  wameweza kutoa  mafunzo ya ufundi  katika kata ya Ipepo pamoja na kata ya Iwawa, lakini ameomba serikari kuwasaidia kupata idadi ya walemavu  ili kuweza kupanga  miundo mbinu katika mwaka 2010

Tuesday, November 3rd, 2009

Ujenzi wa jengo la PIUMA wapamba moto.

Na Witness Ngumba.

Ujenzi wa jengo la PIUMA waenda kasi kwani wanachama wa PIUMA wanapenda ifikapo tarehe 1 December 2009 jengo lao liwelimekwisha na hatimaye waweze kuhamishia ofisi zao zote huko.

Hayo yalisemwa jana na mwenyekiti waPIUMA Bw. Kabuyu Kyando akizungumza na mtandao huu kwenye ofisi ya KatibuTarafa akiwa pamoja na baadhi ya viongozi waPIUMA katika kikao cha pamoja na serikali ya Tarafa.

Mkutano huu ulioitishwa na Katibu tarafa ya Bulongwa Bw. Ambilikile Mwaihola ulikuwa kwa ajili ya kukaa pamoja, kujadilina kupata ufumbuzi juu ya kumaliza jengo la PIUMA haraka.“Nimepata taarifa kuwa pesa za Ujenzi zipo lakini inaonekanakunakosekanauwajibikaji miongoni mwa viongozi na wanachama wa shirika” alisemaKatibu tarafaBw. Mwaihola

Akimtoa wasi wasi katibu tarafa, Mwenyekiti wa PIUMA alisema kuwa yeye na wanachama wa PIUMA wamejipanga kisawa sawa kuhakikisha jengo linaisha ifikapo December mwaka huu. “Mpaka sasa kila siku mwanachama wa PIUMA pamoja na viongozi wana shinda na mafundi kwenye jengo” alisema Bw. Kyando. Aliongeza kuwa kumekuwa na mafundi wakorofi na kuwa fundi ambaye ataonekana anasumbua hatua za kisheria zitachukuliwa juu yake.

Alisema kumekuwa na usumbufu wa hapana pale kutoka kwa mafundi, akitoa mfano Mwenyekiti alisema fundi seremala ameanza kutusumbua tumemwandikia barua ya onyo nakuhakikisha anamaliza kazialiyokuwa amekabidhiwa haraka vinginevyo hatua zakisheriazitachukuliwa.

Veranda imeshaisha kusakafiwa, wiki hili tunategemea kumaliza kufunga milango na hatimaye fundi waumeme na rangi waanze kazi. Tutahakikisha kuwa tunafanya mawasiliano na Mshauriwa wa ujenzi Mtaalam Mwamwala ili awakabidhi kazi mafundi wa umeme na rangi haraka iwezekanavyo. “Nitahakikisha nitalisimamia jengo letu mpaka litakapoisha ili niweze kupata matibabu bora kwa wakati muafaka” alisema Mwenyekiti.

Jengo la PIUMA linatarajiwa kitumika kama kituo cha tiba na ofisi kwa ajili ya upangaji na uendeshaji wa kiliniki ya upimaji na ushauri nasahaa.

 

 

 

 

 

Thursday, October 29th, 2009

RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA KATA YA BULONGWA AKIELEKEA MKOA WA MBEYA.

Na Witness Ngumba.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika ziara ya kutembelea mkoa wa Iringa ametembelea kijiji cha Bulongwa leo mnamo saa 4:30 asubuhi akielekea mkoa wa Mbeya.

Alipofika katika kijiji cha Bulongwa njia panda Namanga, alikumbana na mkusanyiko wa wanakijiji wa bulongwa, wanafunzi pamoja na wanachama wa PIUMA wakiwa kati kati ya barabara wakitaka kuonana na Rais.

Rais alimwomba mwenyekiti wa kijiji cha bulongwa ili aweze kuzungumza nae kwa niaba ya wanakijiji wote ili atoe matatizo yanayowakabili wananchi wa kijiji hiki.

Mwenyekiti wa kijiji cha Bulongwa Bw. Merikizedeki Jekela alisema kuwa tatizo la kwanza ni mbolea za ruzuku hazifiki kwa muda mwafaka na zikifika  haziwafikii walengwa. Rais alisema kuwa tatizo hili amelipata kwa vijiji vingi na ameshaongea na viongozi wa Wilaya juu ya kutatua tatizo hili.

Tatizo la pili  ni mawasiliano ya barabara alimweleza Rais kuwa bara bara yetu wakati wa masika huwa inaharibika na kusababisha kukosekana kwa mawasiliano ya bara bara. Rais alisema kuwa hili tatizo ameliona na alivyokuja mwaka jana aliwaagiza viongozi wa Wilaya ya Makete waanze kutengeneza barabara kwa lami kuanzia Njombe hadi Makete, alisema kuwa amepitia kuangalia utekelezaji huo na ameona wameshaanza utengenezaji wa barabara hiyo, lakini alisema kuwa kwa barabara ya Bulongwa kwenda Mbeya atapitia kuiangalia na kuona ni jinsi gani ya kuikarabati.

Tatizo la tatu ni maji ya bombani, mwenyekiti alimweleza Rais kuwa tulikuwa na maji ya bombani ambayo yalitengenezwa na DANIDA miaka ya nyuma sana lakin kwa sasa vifaa vya maji vimechakaa, na kusababisha maji kushindwa kuwafikia wananchi wa Bulongwa, alimwomba Rais ukarabati wa mradi huo ili wananchi waendelee kupata maji. Rais alisema kuwa alimepokea hilo lakini uongozi wa kijiji uandike madai hayo na kupeleka kwa uongozi wa Wilaya ili wao wapeleke kwenye uongozi wa mkoa na hatimaye taifani ukiwafikia wao wataangalia ni jinsi gani ya kuwasaidia wananchi wa Bulongwa.

 

Tatizo la nne Umeme; Mwenyekiti alimweleza Rais kuwa kijiji cha bulongwa mto Luvanyina ambao unaweza kuzalisha umeme sasa mheshimiwa atatusaidije juu ya hili. Rais alisema kuwa alishawahi kupata habari za mto huo, kwa hiyo bado wanaufanyia kazi.

 

Wananchi wa Bulongwa walifurahi sana kuweza kumfahamu Rais na kuweza kuwasikiliza matatizo yao na Rais mwenyewe alisema kuwa amefurahi sana kuweza kuonana nao kwani kupita vijijini ndipo anapogundua matatizo mengi ya wananchi, baada ya hapo aliwaaga wananchi na kuondoka kuelekea mkoa wa Mbeya.

Rais Jk akiongea na Mwenyekiti wa kijiji cha Bulongwa

Rais Jk akiongea na Mwenyekiti wa kijiji cha Bulongwa

 

 

 

wanaPIUMA wakiwa miongoni mwa kumpokea Rais

wanaPIUMA wakiwa miongoni mwa kumpokea Rais

 

wananchi wamekusanyika wakimsubiri Rais

wananchi wamekusanyika wakimsubiri Rais

 

 

 

 

Tuesday, October 27th, 2009

Ujenzi wa Sekondari Iwawa

Na Evance Seth

 

Wananchi wa kata ya Iwawa wanakabiliwa na shughuli  za ujenzi  wa  majengo yanayoendelea kujengwa shuleni hapo  ikiwa pamoja na  ujenzi wa Hosteli , Maabara , Maktaba pamoja na  jengo kwa ajili ya kidato cha tano na kidato cha sita.

 

Hayo  yamezungumuzwa na  Afisa mtendaji  wa Kata  ya Iwawa Bw Selemani Kiwone katika mazungumzo yake na mwandishi wa habari hii.

 

Akizungumzia ujenzi huo mkuu wa shule hiyo Bw.  Omath Sanga amesema kuwa wananchi wametoa mchango  mkubwa  katika ujenzi unaoendelea kwa usombaji  wa mawe, mbao, uchimbaji kiwanja pamoja na  mafundi kujenga majengo hayo.

 

‘’viongozi wa serikali wanatakiwa kutambua  umuhimu  kushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi” alisema Bw. Kiwone. Akifafanua juu ya suala hilo Bw. Kivone alisema katika ujenzi wa shule za ya sekondari  baadhi ya viongozi wa Halmashauri wapo nyuma  katika kuchangia  ujenzi. “Hali hiyo inasababisha  kuwakatisha tama wananchi wanaotoa michango pamoja na nguvu zao shuleni hapo” alimalizia Bw. Kiwone.

 

Naye mkuu wa shule ametoa changamoto zinazo wakabili shuleni hapo kuwa ni pamoja na upungufu wa walimu, nyumba za walimu, baadhi ya vyumba vya madarasa kuto karabatiwa na kusababisha wanafunzi kulundikana katika darasa moja, hali ambayo ina sababisha mwalimu kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

Sunday, October 25th, 2009

We are Hope

 

PIUMA

PIUMA

Ari Mpya, Nguvu Mpya kwa Pamoja Tutashinda!
Ari Mpya, Nguvu Mpya kwa Pamoja Tutashinda!

 We are proud to be part of the great army that battles HIV/AIDS on the field. We are one Army under one comander “HOPE”

Friday, October 23rd, 2009

Wagoma kuzika maiti

Na Mwandishi wetu

Jeshi la polisi  kituo cha matamba  limewakemea  wananchi wa Tarafa hiyo  kuacha tabia  ya Imani potofu  pindi  kifo cha mtu kinapo tokea  hasa katika mazingira ya kutatanisha.

 

Kauli hiyo imetolewa na  na Jeshi hilo kutokana na wananchi wa kijiji cha Lugoda kilichopo kata ya Mlondwe kuweka mgomo  kuto mzika  mkakazi  mmoja wa kijiji hicho Bi Salai Nkwama  kwa kile kinacho sadikika  kuwa mama huyo amefariki kwa imani za kishirikina.

 

Uchunguzi uliofanywa na madaktari kituo cha afya  cha Matamba , imeonekana mama huyo haja fariki  kwa imani za kishirikina  wanavyo zani wanajamii wa kijiji hicho.

 

Kwa upande wao wananchi  wamesema kifo  cha Bi. Salai kimetokea usiku  wa kuamkia  ambapo  mama huyo aliugua  ghafla na kukimbizwa kituo cha afya  Matamba  ambapo alifariki muda  mchache baadaye.

 

Hata hivyo wananchi hao wamesema endapo serikali kutolifumbia macho suala la  watu wenye imani za kishirikina  kwani kama serikali haitakemea tatizo hilo ndio mwanzo wa uvunjifu wa amani na haki za binadamu.

 

Hivi karibuni kumekuwa na upigaji kura zoezi liloendelea nchi nzima kuwabaini watu wanaojihusiha na vitendo vya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi “albino”  Habari za uhusika wa ganga wa jadi na imani za kishirikina kwenye mauji hayo zilifichuliwa na mwandihishi mwandamizi wa BBC nchini Bi. Vicky Ntetema.

 

“Unajua hata vita dhidi ya UKIMWI inakuwa ngumu sana kama tutaendelea kusadiki kuwa watu wanauawa kichawi” alisema Bw. Kambanyuma mwenyekiti wa PIUMA alipokuwa akitafakari pamoja na mwandishi wa habari hii.