February 26th, 2010
Na Evance Seth.
Makarani na wasimamizi wa SENSA ya mifugo wamepatiwa mafunzo yatakayo wawezesha kupima mpango mzima wa kuondoa kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa mwaka 2009/2010.
Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika wilaya ya Makete kaimu katibu tawala wa mkoa wa Iringa Bw. Adam Swai amesema mwaka 2008 mpango wa sekta ya kilimo kwa pato la taifa kulikuwa ni asilimia 25.8, kati ya asilimia hiyo ya kilimo cha mazao kilichangia asilimia 19 huku mifugo ikichangia asilimia 4.7.
Kwa upande Meneja takwimu mkoa wa Iringa amesema sense hiyo hufanyika kila baada ya miaka mitano na kwamba katika mafunzo hayo watachagua wakulima kumi , kutoka katika mafunzo hayo watachagua wakulima kumi na tano kutokana na vigezo vilivyowekwa vya wakulima bora katika kila wilaya .
Posted in News | No Comments »
February 26th, 2010
Na Evance Seth.
Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa UMA inakusudia kuwa watumishi wa serikari kuanza kupokea mishahara dirishani badara ya kuwaingizia katika akaunti zao.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa Nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa uma Mh. Hawa Ghasia alipokuwa akiwahutubia watumishi wa halmashauri ya wilaya ya makete. Alisema ofisi yake inafikilia kufanya hivyo kutokana na kulipa mishara hewa ya watumishi.
Mpango huo wa watumishi kupokea dirishani utasaidia kuondoa udanganyifu ambao serikari inalipa mishahara hewa na kusababisha serikari hasara kubwa. Amesema katika kupitia utafiti uliofanywa na wizara yake imebaini katika sekta ya afya na sekta ya elimu baadhi ya watumishi wanalipwa mishahara hewa.
Mh. Ghasia alikuwa katika ziara yake ya kutoa semina kwa halmashauri ya wilaya ya makete inyohusu mabadiliko mahali pa kazi na utawala bora ambapo hii leo akitoka hapa anaelekea wilayani Ludewa.
Mikoa mingine ambayo amepitia kutoa semina hiyo ni MANYARA, KIGOMA, LINDI, MTWARA, PWANI , IRINGA na akimalizia SINGIDA.
Posted in News | 1 Comment »
February 26th, 2010
Na Evance Seth.
Katika Wilaya ya Makete kata ya Iniho kumefanyika chanjo ya watu wazima kuanzia miaka mitano na kuendelea.
Chanjo hiyo ilikuwa ni agizo la serikari kuwa kila mwananchi anatakiwa kupata chanjo ilimradi ana miaka kuanzia mitano. Chanjo hiyo alihudumia Bw. Tigrath Sanga toka kata ya Iniho kwani ndiye aliye pata mafunzo hayo.
Bw. Tigrath kabla ya kuanza kuhudumia alitoa maelezo kwa ufupi kwa wananchi wa wake kuwa, chanjo hii ni ya vidonge na alisema maana ya chanjo hii ni ya kuzuia magonjwa nyemelezi pamoja na kuua minyoo mwilini, alitoa mfano mmoja wa magonjwa nyemelezi kama kuvimba matezi.
Alisema chanjo hii hawaruhusiwi watoto wadogo kupata kwani vidonge hivi vina nguvu sana mwilini vinapo fanya kazi , na alisema upatapo chanjo hii huruhusiwi kutumia kinywaji cha aina ya kileo kwa siku uliyopata chanjo.
Posted in News | No Comments »
February 23rd, 2010
Na Evance Seth.
Jamii imeshauriwa kuwa na moyo wa kutoa vitu mbalimbali kwa watoto yatima wanao lelewa katika vituo mbalimbali ili kuwa fariji na wao kuto kuona kama jamii imewasahau.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Hawa Ng’humbi wakati akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani zaidi ya shilingi laki moja kwa watoto wa kituo cha yatima cha Bulongwa Lengo la ziara yake hiyo ni kuona kituo hicho pamoja kuelewa historia yake na kuelewa kinaendeshwaje.
Akipokea msaada wa vitu hivyo mmoja wa watumishi wa kituo hicho amesema kituo hicho kinahitaji msaada mkubwa wa watu wa serikari kwa ujumla ili kiweze kujiendesha chenyewe kwani kwa sasa kinamtegemea mzungu mmoja ambaye kwa sasa ni mzee anayeitwa SISTER ANNA.
Mh. Mkuu wa wilaya pia aliwafariji watoto wanaolelewa katika kituo hicho ambacho kina watoto thelathini na miongoni mwao watoto sita wanaishi na virusi vya UKIMWI
Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya aliongozana na Diwani wa kata ya Bulongwa Bw. Estomih Mahenge, M/K umojwa wa wanawake Tanzania wilaya ya Makete na Bi. Erika Sanga, pamoja na Israel Green Kutoka kituo cha polisi makete.
Posted in News | 1 Comment »
February 23rd, 2010
Na Evance Seth.
Zaidi ya shilingi milioni hamsini na saba pointi nane zinatarajia kutumika kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Unyangala na Igumbilo katika kipindi cha mwaka 2009-2010 wilayani Makete.
Akizungumza mratibu wa mfuko wa maendeleo ya jamii wilayani Makete Bi Jaklini Mroso ameeleza kuwa fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi pamoja na nguvu za wananchi zitahitajika kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Naye katibu wa zahanati ya Unyangala Bw. Boaz Sanga pamoja na mtunza hazina Bw. Erasto Mvela wamesema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati kwao kwani wamekuwa wakitumia muda mwingi kuwa peleka wagonjwa katika zahanati ya Utengule ambapo ni mbali.
Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF wilayani Makete umekuwa mkombozi kwa wananchi wengi wilayani Makete hasa vijijini kwa kusaidia misaada mbalimbali ambayo wamekuwa wakiibua kupitia mikutano ya hadhara, aidha kufuatia hali , katibu wa mradi wa ujenzi wa zahanati Igumbilo Bw. Godfrey Sanga ameeleza kuwa zahanati hiyo kwa sasa ipo hatua ya mwisho na ameshukuru TASAF kwa ufaddhili wa mradi huo na amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na TASAF wilayani makete.
Posted in News | 1 Comment »
February 22nd, 2010
Na Evance Seth.
Mnada wa mifugo uliopo katika kijiji cha isapulano kata ya Iwawa ulioanza kujengwa mwaka 2009-2010 kwa ufadhili wa DADS NA DADPS pamoja na nguvu za wananchi ulioghalimu kiasi cha shilingi milioni kumi na nne na thelathini na nane elfu 14,380,000 umezinduliwa .
Uzinduzi wa mnada huo umefanywa na mgeni rasimi ambaye ni mbunge wa wilaya ya makete MH BINILITI SAATANO MAHENGE ambapo amewatakia wananchi wa kijiji cha Isapulano na wananchi wa wilaya makete kwa ujumla kuutumia mnada huo ili kujiongezea kipato.
Aidha ameendelea kusema wananchi wote wanatakiwa kuonesha upendo kwa wageni watokao nje ya makete kwa kuto wakatisha tama kwa kuwaibia mali zao pindi wanapo kuja kwenye mnada huo. Na ameeleza mafanikio yaliyo patikana katika awam ya nne ya uongozi kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu kwa wakazi wa wilaya ya makete ambayo ni kufufua zao la pareto pamoja na elimu ambapo kila kata kumejengwa shule za sekondari na wanafunzi wengi kufanikiwa kujiunga na elimu ya sekondari.
Katika sherehe za uzinduzi wa mnada huo MH mahenge aliongozana na mwenyekiti wa Halmashauri wa wilaya ya makete ambaye pia ni diwani wa kata ya Iwawa MH ONO SIKUNALA NKWAMA , mtendaji Iwawa KIWONE , AFISA KILIMO NA MIFUGO WA WILAYA BW ERNEST MKONGO pamoja na watalam wake. Aidha changamoto kubwa inayo ukabili mnada huo ubovu wa barabara inayotoka makete kwenda kijiji hapo ambayo wakati wa masika haipitiki kwa uraisi pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya maji ambapo kwa suala la maji MH ONA nkwama ametoa liri mbili za bomba kwa ajili ya kusogeza maji eneo la mnada na suala barabara kuahidi kushughulikia ipitike muda wote.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wananchi wa kijiji hicho wameonekana kufurahishwa na na mnada ambao utakuwa ukifanyika mara mbili kwa mwezi tarehe kumi na tano na tarehe thelathini ya kila mwezi na kusema mifugo yote itauzwa mnadani ili kupata soko la uhakika na si la kuuzia mitaani.
Posted in News | No Comments »
February 22nd, 2010
Na Evance Seth
Semina ya maelekezo kuhusu usimamizi wa mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya msingi iliyo fanyika katika ukumbi wa Halimashauri ya wilaya ya makete.
Akinzungumza katika semina hiyo mkuu wa wilaya ya makete Bi HANA HUMBI amesema wasimamizi wanatakiwa kuepuka vishawishi kama vile rushwa katika zoezi hilo la usimamizi.
Alisema kuwapa watoto mtihani au majibu ni kujenga Taifa lenye watu wajinga wasio na elimu wala taaluma na kusema yeyote atakaye gundulika kufanya hivyo atawajibika kisheria.
Akifunga semina hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya makete Bi IMELDA ISHUZA ametaka wasimamizi hao wa mtihani kuwa na upendo kwa watoto kwa kuwaelekeza vizuri pale wanapo hitaji msaada wa msimamizi.
Posted in News | No Comments »
February 22nd, 2010
Na Evance Seth
Katika wilaya ya makete kuna shirika moja lisilo la kiserikali linaloitwa CUAMM linalotokea mkoani Iringa.
Shirika hilo linajishughulisha na mambo ya upimaji VCT . Na shirika hilo liliomba kufanya kazi na mashirika mengine yaliyopo katika wilaya ya makete yanayo jishughulisha na mambo ya upimaji.
Pia shirika hilo lilitoa mafunzo mbalimbali yakiwemo mafunzo ya;
1. UANDIKAJI WA RASMU NA MRADI
2. UTAFUTAJI WA VYANZO VYA FEDHA
3. UFUATILIAJI NA TATHIMINI
Mashirika yaliyo shiliki mafunzo hayo ni1.MAKEYODENI , PIUMA, MAWATA5, LCCB, FEMA, IDYDC, SUMASESU, MAHEPO na MASUPHA.
Na kila shirika liliwakilisha viongozi wane. Na mafundisho hayo yaliendeshwa na WILLIAM YOTHAM - UNV na ABRAHAM SANGA - CHAC.
Na mafunzo hayo yalifungwa na FLORA NSEMWA toka shirika la CUAMM na kuagana na kutakiana safari njema pamoja na utendaji wa kazi njema.
Posted in News | No Comments »
February 17th, 2010
Na Evance Seth.
Katika Wilaya ya Makete kuna mtandao mmoja unajishughulisha na vijana unaojulikana kwa jina la MAKEYODEN.
Mtandao huo uliamua kufanya kikao cha viongozi wa mtandao tarehe 22/01/2010 na kujadili malengo mbalimbali ya kufanya 2010-2013, na malengo hayo ni kama
1.KUBORESHA UONGOZI ni kufanya marekebisho katiba ya makeyoden, kuandika sera kanuni na taratibu za makeyoden, kanuni za utendaji na uendeshaji , kanuni na taratibu za fedha na kanuni za ustawi na mahusiano na kuendesha vikao vya kamati kuu na mkutano mkuu.
2.KUBORESHA UTENDAJI ni kuajili watendaji wa ofisi kuu, kumaliza ujenzi wa ofisi ya mtandao na vituo vya kata, kununua samani na vitendea kazi, kuendesha vikao vya utendaji na kuanzisha tovuti na internet ya makeyoden.
3.KUBORESHA MAHUSIANO NA USHIRIKIANO BAINA YA MAKEYODEN NA WADAU WENGINE ni kuandaa utambulisho wa shughuli za makeyoden kuandaa orodha ya wadau mbalimbali, kusambaza utambulisho wa makeyoden kwa njia mbalimbali na kuhudhulia matukio ya wadau mbalimbali.
4.KUENDELEZA SHUGHULI ZA MAKEYODENI ZILIZOPO ni kuhimiza umaliziaji wa vituo vya kata tisa , kusaidia vituo saba vilivyokamilika vianze vianze utekelezaji wa mipango na kukamilisha usajili wa redio na kutayarisha mpango wa kazi na wa kujitegemea wa redio na kuongeza nguvu ya kudhibiti maambukizi dhidi ya ukimwi.
Kikao hicho kilifanyika na viongozi wa mtandao ambao ni
1. NAHAMAN SANGA - MWENYEKITI
2. JUMA SINENE - KATIBU
3. EMANUEL SANGA - MWASIBU
4. FRANCISKO SIGARA - MJUMBE
5. SALEHE NGULO - MJUMBE
Na mwisho viongozi hao walihitimisha kikao kuagana na kutakiana safari njema.
Posted in News | 1 Comment »
January 25th, 2010
Na Witness Ngumba.
Viongozi wa PIUMA pamoja na baadhi ya wanachama wa PIUMA wiki iliyopita walitembelea kijiji cha Utanziwa kwa ajili ya kuwatembelea wanachama wa PIUMA wanaoishi katika kijiji hicho.
Zoezi hili liliongozwa na Katibu Mkuu wa PIUMA pamoja na Mwenyekiti, Daktari Zin zin, na wanachama wawili ambao ni Izack Sanga na John Nyivaha.
Kazi ambazo walikwenda kuzifanya ni pamoja na;
· kuwasajili wanachama waliokuwepo kwa upya kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo, kuhakikisha kila mwanachama yumo kwenye orodha ya wanachama hai na waliopiga picha.
· Kutoa ushauri nasaha kwa wasio wanachama ili wajiunge na shirika la PIUMA kwa ajili ya kupata huduma zinazotolewa na shirika.
· Kujua maendeleo ya wanachama kiafya na kwa wale wanaoumwa wapewe huduma inayostahili.
· kwa wale ambao walikuja kwenye zoezi hilo waliombwa kuwaambia wenzao kuwa wafike ofisini ili waweze kupigwa picha kwa ajili ya vitambulisho.
Kwa wale ambao walishindwa kufika kwenye kituo tulichokuwa tumekusanyikia kutokana na afya zao kuwa mbaya tulihakikisha tunawetembelea majumbani kwao ili kuwajulia hali na kuwapa ushauri. Zoezi hili litaendelea kwa kila wiki kwa kijiji kimoja mpaka tutakapomaliza vijiji vyote “alisema Katibu Bi. Anna Mwinuka”

Timu ya wanaPIUMA wanaotembelea vijijini


Posted in News | 4 Comments »