Latest News

August 28th, 2009

Upimaji wa Aridhi

Na Evance Seth

 

Wilaya ya Makete imeungana na wilaya zingine za Tanzania katika zoezi la kitaifa la upimaji wa Aridhi na viwanja. Zoezi hili linaratibiwa na kuendeshwa na Mpango wa Kurasimisha Rasimali na Biashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA).

 

Akizungumza na mtandao huu mwenyekiti wa kijiji cha Iniho Bw. Ferance Sanga alisema zoezi hili limeanza katika wilaya ya Makete mwezi April. Hata hivyo Bw. Sanga alisema mvua zilizokuwa zikinyesha wakati wa masika zilipunguza kasi ya upimaji wa viwanja na mashamba.

 

Alipohojiwa na Mtandao huu kama anaona faida zozote za zoezi hilo Bi. Roda Muhando alisema, upimaji unawasaidia watu kuwa na hati ya umiliki wa mali zao. “kukatia hati miliki hiyo ni faida kwako kwani hakuna mtu atakaye kupokonya  shamba lako kwani utakuwa umekatia hati miliki na litatambuliwa ni la kwako” aliongeza Bi. Muhando.

 

Bi. Roda aliwaasa wanawake kujitokeza kwa wingi kupewa hati za kumiliki mashamba na Viwanja  kwani inawapa nguvu wanawake. “Nikiwa mwanamke nashukuru Serikali kwa kuanzisha huu mpango kwani sasa sitanyanyaswa kutokana na jinsia yangu kwenye umiliki wa aridhi” aliendelea kusema Mama Muhando.

 

Pamoja na zoezi la upimaji shirika pia litasaidiana na wanachi kujenga ofisi kwa ajili ya matumizi ya maofisa wa kijiji, baraza la aridhi na maofisa wa aridhi. Katika ujenzi huo wananchi watachangia nguvu, uwanja na mawe kwa ajili ya ujenzi na gharama zingine zote zitagharamiwa na MKURABITA.

haya ni baadhi ya mashamba yaliyopimwa.
Sehemu ya Mashamba yaliyopimwa Kijijini Bulongwa

Picha na Witness

August 13th, 2009

Vijana wapewa stadi za maisha

Na Evance Seth

 

Wakati vijana wa kijiji cha iniho wakiendelea na semina nyingine kijijini kwao kama ilvyoripotiwa na mtandao huu, vijana wengine wa umri kati ya miaka kumi na nne hadi kumi na nane walikuwa wakipata elimu nyingine ya stadi za maisha kijijini Bulongwa.

 

Katika semina iliyofanyika ukumbi wa Dinduka kijijini Bulongwa iliratibiwa na wakufunzi Salum Sanga, afisa utamaduni wa wilaya ya Makete na Bw. Juma Sanga, afisa utamduni wa wilaya ya Makete iliwashirikisha vijana kutoka katika vijiji vyote vya tarafa za magoma na Bulongwa.

 

Vijana wawili kutoka katika kila kijiji walifanya jumla ya vijana sitini walioshiriki semina hiyo waliowawakilisha vijana wenzao wa kata nne za tarafa hizo mbili za Bulongwa na Magoma. 

 

Wakizungumza na mtandao huu kutoka katika ukumbi wa semina hiyo Vijana Mary Baghdad wa Iniho na Joseph Muvela wa kijiji cha Iyoka walisema “Hii semina ilikuwa na nia ya kuwapa vijana nyenzo za kukabiliana na mazingira hatarishi ya maambukizi ya UKIMWI”

 

“Tumejifunza namna ya kukabiliana na mihemko, mahusiano, kuwa wabunifu, ushirikeli na kujitambua,” walisema vijana hao. Wakizungumzia stadi ya kujitambua vijana hao walioungwa mkono na wenzao waliokuwa wamewazunguka wakati wa mahojiano na mwandishi walisema, stadi hii ni muhimu kwani inamfanya kijana ajijue anatoka wapi, yupo wapi , anafanya nini na anakwenda wapi.

 

Bw. Salum Sanga alisema wamefanya mafunzo na vijana walio chini ya miaka kumi na tisa kwasababu vijana wa umri chini ya miaka kumi na tisa wengi wao hawajapata nafasi ya kupata elimu ya stadi za maisha wakiwa nje ya mashule.

 

“Vijana wengi wa umri huu wametoka mashuleni hivi karibuni kwa hiyo kuna ulazima kuwapa elimu inayofanana na mazingira wanayoishi sasa, mazingira ya nje ya shule” alisema mkufunzi wa semina hiyo Bw. Sanga. Vijana hao wanategemewa kuwa mabalozi na kutoa elimu kwa vijana wenzao vijijini wanakotoka.

 

Vijana wakipata semina ya stadi za maisha

Vijana wakipata semina ya stadi za maisha

 

 

 

August 13th, 2009

Vijana na UKIMWI

Na Evance Seth

 

Wiki hii vijana wapatao ishirini wa kijiji cha Iniho wamefaidika na elimu juu ya ugonjwa wa UKIMWI. Elimu iliyotolewa katika semina iliyowashirikisha vijana kuanzia miaka kumi na tano.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii mkufunzi wa semina hiyo Bw. Maonyesho Ngohani alisema semina hiyo ililenga kuwajengea uwezo vijana hao  wa kuweza kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazoambatana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

“UKIMWI huleta madhara kwa mtu binafsi, familia yake na jamii kwa ujumla kwa hivyo ni muhimu kuwapa vijana nyenzo  na stadi za maisha kuweza kukabiliana na madhara hayo” alisema Bw. Ngohani. Mada nyingine iliyotolewa ilikuwa ni pamoja na namna ya kuwatunza walioathirika na VVU pamoja na kuondoa Unyanyapaa.

Akizungumzia sehemu za stadi za maisha za kuwakinga na VVU vijana Bw. Ngohani alieleza kuwa vijana hawana budi kujishirikisha na michezo, pia kushiriki katika shughuri za kimaendeleo zitakazo wainulia vipato vyao. Alisema ajira kwa vijana, vifaa na viwanja ya michezo ni changamoto mojawapo inayowakabili vijana katika kushiriki kikamilifu kwenye mapambano ya VVU.

“Tunawashauri vijana kuendelea kushikiria na kufuata ABC za kuepuka maambukizi ya VVU” alisema Mkufunzi huyo. Akizitaja ABC hizo bwana Ngohani alisema vijana lazima wajiepushe na Ngono, wawe waaminifu kwa wapezi wao na kutumia kondomu kila wanapofanya tendo la ngono. “Kila mtu ana mchango katika mapambano dhidi ya UKIMWI” alimalizia Bw. Ngohani.

 

“Vijana tunahitaji kujitambua na kujua umuhimu wetu katika mapambano dhidi ya UKIMWI” alisema Eva Lufingo mmoja wa washiriki wa semina hiyo. Akifafanua zaidi kijana huyo alisema vijana wana nyenzo na uwezo wa kutokomeza UKIMWI na kuasa jamii kuwa iwape nyenzo na nafasi ya kushiriki kwenye mapambano ya dhidi ya UKIMWI

August 3rd, 2009

Kitulo - Matema Tourism

By Evance Seth

The Kitulo national park for the first time last week has received biggest number of fifteen tourist at one time from Europe. Although Tanzania is a country with large and beautiful national park and reserve as Serengeti and Selous Kitulo is of its kind.

Unlike other national parks which are rich of animals, Kitulo is a national park with thousands of flower species and is a resting point of bird when flying from the northern pole to the southern pole.

Speaking through their translator these tourists said they were very much impressed by the beauty that they have experienced in Kitulo national park which they called it a natural garden.

On their way to Matema beach the Tourist made a camp in Iniho Village at Ivala grazing plateau. Mr. Allain Mbilinyi who was coordinating this trip from Iniho said Ivala is a communal land put aside for grazing. “Since waking are no longer rearing large groups of cattle we can convert this place into a camping site and become more useful” said Mr. Mbilinyi

Ivala is a mid way from Kitulo to Matema beach of Lake Nyasa via the Livingstone ranges with Kitulo being 3000 meters above sea level and Matema beach at Lake Nyasa 1.5 below sea level. The two places are separated with walking time of two days with good vicinity on the way including the Kapunji animals which are one of the extinct creatures on earth found in forests around Livingstone ranges.

Apart from the natural beauty experienced, the the tourist said that they were also impressed by people life in the villages on their way, the life of peace and respect with each other including clean and good environment.

When talking to this website one of the youth who was helping carrying luggage of the tourists said for youth it mean business as they make some money from helping the tourists with their luggage. “It is like a temporary employment for me and my fellow young men” commented the young man.

 

Tourists camping at Ivala, Iniho for a night break before they could proceed to Matema the next day

Tourists getting ready to walk down slope of more than 2500M to Matema beach

Photo by Evance

July 30th, 2009

Ajira na Mazingira

 Na Evance Seth

Wakati suala la mazingira ni ajenda namba moja duniani kuna baadhi wanaonekana haiwahusu. Mtandao huu ulifanikiwa kuzungumza na vijana wa kikundi cha ugongaji wa kokoto wa kijiji cha iniho. Vijana hawa walioko katika kijiji cha Iniho wamejiajiri kwa kutengeneza kokoto.

 

Kuanzia mwaka 2007 ushirika huu wenye jumla ya vijana wannne unajishughurisha na utengenezaji na usambazaji wa kokoto za mawe magumu. Akizungumza na mtandao huu mmoja wa vijana hao Baraka Mdonya alisema waliamua kujishughurisha na biashara ya ugongaji wa kokoto kwa sababu kulikuwa na ujenzi unaendelea kijijini Iniho na vijiji vya jirani lakini walikuwa wanakosa malighafi hiyo. “kwa mfano ujenzi wa madarasa wa shule ya sekondari ya mwakavuta unahitaji kokoto kwa wingi kwa hiyo ilikuwa lazima watu wafanye hiyo kazi” alisema kijana huyo.

 

Uhafifu wa zana za kutendea kazi unarudisha nyuma uzalishaji kwa kiasi kikikubwa. Kikundi hiki kinatumia nyumdo kubwa moja na nyundo ndogo kadhaa. Utaratibu wa utengenezaji wa kokoto ni kutindua miamba mikubwa baada ya hapo kuigonga kwa nyundo kubwa kutoa vipande vya ukubwa wa wastani, kisha hutumia nyundo ndogo kuvifanya hivyo vipande vya wastani kuwa na ukubwa wa kokoto inayotakiwa.

 

Walipoulizwa kwa miamba mikubwa inayoshindakana kuvunjika vijana walisema huwa wanaichoma moto hiyo miamba, ikipata moto mwamba mkubwa hufanya nyufa na kisha kuachaia katika vipande vikubwa vikubwa ambayo hugongwa na nyundo.

 

Wakizungumzia namna wanavyoweza kuufanya moto mkubwa wa kupasua jiwe vijana hao walisema kuwa  “huwa tunatumia miti moto wa kuni” walisema . Miti mingi huwa ni inayokatwa katika misitu ya karibu na sehemu  ya uchimbaji.

 

Vijana hao wanasema huuza kokoto yao kufuatana na mahitaji ya mteja. Huwauzia kuanzia wale wanaotaka kununua kwa kiasi cha ndoo moja ya lita kumi ambayo huuzwa kwa shilingi elfu moja, ndoo ya lita ishirini ambayo huuzwa kwa shilingi elfu mbili na trip moja ya roli inayouzwa kwa shilingi laki moja.

Walipokuwa wanaongea na mtandao huu vijana hao walisema wana trip sita za maroli kwenye stoo yao. “pesa tunayoipata kwenye kazi hii hutusaidia kutatua matatizo muhimu ya maisha kama kulipia ada za shule za watoto” walisema vijana hao. Mipango ya baadaye ya kikundi hiki ni kuongeza uzalishaji  na kutafuta vifaa vya kisasa zaidi.

 

Wakizungumzia changamoto zinazowakabili walisema soko bado ni tatizo, walesema wanaweza kuuza kiwango cha kutosha cha kokoto kunapokuwa na makampuni ya ujenzi  wilayani makete. Wakitaja mfano wa makampuni hayo, walisema makampuni ya simu yanapojenga minara yao, TANROAD wanapokuwa wanafanya ujenzi wa madaraja na mifereji ya maji barabarani

 

Pamoja na kuwa biashara ya utengenezaji wa kokoto inawapatia kipato wanaushirika huu lakini pia unasababisha uharibifu wa mazingira. Uchimbaji wa mawe na Ukataji wa miti kwa ajili ya moto wa kupasulia miamba ni sehemu ya uharibu huo. Wakiongea na mtandao huu vijana hao walisema wanatambua madhara hayo lakini hawana namna nyingine. “Hili linaweza lisiwe tatizo kama tutawezeshwa na miradi ya kutunza mazingira kwenye maeneo yetu ya machimbo au kupewa kazi mbadala” alimazia Bw. Mdonya kiongozi wa kundi hilo.

 

Ugongaji wa kokoto

Ugongaji wa kokoto

 Picha na Evance

July 22nd, 2009

New Hope

                                         

   

    Jackson Mbogela 

    The Netherlands

 

 

 

Members of PIUMA and the population of Makete district at large will be receiving a new doctor in next coming month.

 

Information provided by PIUMA officers says that they are expecting to receive Dr. Zin Zin any time from third week of August this year.

 

Speaking from her office the general secretary for PIUMA Ms. Anna Mwinuka said their members have prepared themselves to receive a new doctor who will care for their health.

 

In Makete Dr. Zin Zin will work under close cooperation with the highlands hope initiative for the well being of patients in the highlands. The highlands hope initiative includes TANWAT cooperate hospital, Consolata Ikonda Mission hospital and PIUMA a self support group of people living with HIV/AIDS

 

PIUMA are on their way to set a health facility that will provide medical service for more than 30,000 people living around Bulongwa and Magoma wards.

 

“I need to have a doctor that I will have confidence in, a doctor that I will trust” said Markus one of the members of PIUMA when spoke over phone from Bulongwa. Members of PIUMA several times have expressed dissatisfactions on the medical service provided by the government and church health facilities in Makete district.

 

In year 2006 members of PIUMA when meeting minister for health and social wellfare Professor David Mwakyusa, complained the substandard services provided by incompetent providers in the district and they were promised improvement the promise which has hardly been fulfilled.

 

“The coming of Dr. Zin Zin will help to improve the service that has deteriorated so much in this area” said Ms. Mwinuka. Patients under Care and Treatment Centre have been going without important laboratory diagnostic tests for years in this heavily HIV affected district.

 

In his e-mail the member of the PIUMA trustees board Dr. Rainer Brandl said he hopes for cooperation and solidarity to be provided to this new doctor more than demand for Money. “Personally, I wish Zin Zin all the best and I believe and trust that she has the skills to put the ongoing death of PIUMA members to an end” added Dr. Brandl in his mail.

Dr. Zin Zin

Dr. Zin Zin

July 21st, 2009

Kujiajiri Kijijini

Na Evance Seth

 

Mboga mboga ni sehemu muhimu ya mlo kwa wananchi wa wilaya ya Makete. Katika kijiji cha Lumage mtandao huu uliweza kumtembelea Frank mjasiriamali anayeshughulika na kilimo cha mboga  mboga.

 

Akiongea na mtandao huu Frank alisema alianza kilimo hicho mwaka jana akiwa na mtaji wa shilingi elfu tano zilizotosha kununua mbegu tu. “Kilimo cha mboga mboga hakihitaji mtaji mkubwa sana unachohitaji ni mbegu tu” alisema bwana Frank ukizingatia aridhi sio tatizo kwa wilaya ya Makete. 

 

Pamoja na mtaji wa mbegu Frank alihitaji nguvu na muda wa kufanya kazi kwenye bustani yake. Frank analima kwa jembe la mkono na kumwagilia bustani yake kwa  ndoo wakati wa kiangazi. Pia mboga za Frank hazitumii mbolea za viwandani kwani anatumia mbolea ya wanayama na anasema imemsaidia sana kwani inaleta mazao mazuri yanayovuti walaji.

 

“Katika bustani yangu nimepanda mbogamboga za aina tatu ambazo ni kabeji,chainizi na saradi” aliongeza Frank. Alisema kuwa mboga hizo zimesaidia kujipatia mboga mboga za majani kwa urahisi pamoja na kuziuza kwa jamii inayomzunguka na na kujipatia pesa zinazomsadidia kwa matumizi mengine.

 

Frank anayeuza mboga  kuanzia shilingi mia mbili kwa fungu alipokuwa anzungumza na mtandao huu alikuwa na  shilingi elfu hamsini zilizotokana na uuzaji wa mboga. “wakati mwingine nakuwa na pesa nyingi zaidi” aliongeza Frank.

 

Matatizo yanayomkabili ni pamoja na soko duni ,pembejeo za kilimo pamoja na madawa ya kuulia wadudu waharibifu.  Frank alisema vifaa vya umwagiliaji ni tatizo kubwa, anahitaji vifaa vitakavyomuwezesha kuokoa muda wa umwagiliaji kwani anahitaji kumwagilia mara mbili kwa siku.

 

Mipango ya baadaye ya frank ni pamoja na kuongeza eneo kubwa zaidi la bustani na kutafuta soko kubwa la uhakika la mazao yake. Timu ya mtandao huu inampongeza Frank kwa kuwa mjasiriamali wa eneo lake na tunawahamasisha wananchi wengine kuiga mfano wake katika maeneo mengine.

 

Kijana Frank akiwa katik shamba lake la mboga mboga

Kijana Frank akiwa katik shamba lake la mboga mboga

July 20th, 2009

Vijana na maisha ya Kijijini

Evance Seth

Kijana Emanuel ni mzaliwa wa kijiji cha Iniho wilayani Makete. Toka kuhitimu kwake elimu ya msingi 1997 Emmanuel alikuwa akiishi kijijini Iniho kama vijana wengine wa kijijini akifanya shughuri za kujikimu ikiwemo kilimo mpaka mwaka 2003 aliposafiri kwenda Mufindi kutafuta kazi katika mashamba ya chai.

Bwana Emanuel alibahatika kupata kazi ya kuchuma chai katika mashamba hayo. Hata hivyo baada ya mwezi mmoja alishindwa kuendelea na hii na kazi tena. Kazi hii haikuweza kumpa kipato hata cha kukidhi mahitaji yake kwani kwa siku aliweza kuchuma chai kilo nne wakati kwa wastani mtu anachuma kilo mpaka mia moja. Kilo ya chai ilikuwa ikinunuliwa kwa shilingi mia mbili. “Niliamua kucha kazi hii kwa hiari yangu” alisema Emanuel alipokuwa akizungumza na mtandao huu. Alipoacha kazi Emanuel alienda kuomba kazi sehemu nyingine ambapo alipata kazi ya kufyaka vichaka na miti inayoota kando kando ya bara bara . Kazi hii ilikuwa inamuingizia kipato cha shilingi elfu moja na mia tano kwa siku na pia aliweza kuimudu hii kazi .

Baada ya miezi mitatu Emanuel tatu tangu ameanza kazi ya kuasafisha barabara alipata marafiki waliokuwa wamekuja likizo Mufindi wakaitokea Dar Es salaam. Marafiki hawa walikuwa ni waimbaji wa nyimbo za kizazi kipya maarufu kama bongo flava. Wana muziki hawa hakukawia kutambua kipaji cha uimbaji kilichofichika ndani ya Emanuel. Wakamtaka Emanuel ajiunge nao na waongozane kwenda Dar Es salaam.

Emanuel akasafiri na hao wasanii rafiki zake mpaka Dar Es Salaam ambako alifikia kwa mtu wa kijijini kwao ambaye ni mmiliki wa shule ya Nia Njema Mjini Dar Es Salaam. Mwenyeji wa Emanuel alimpa kazi ya kulisha Nguruwe na Kuku, kazi aliyotakiwa kufanya mchana mzima na kupumzika usiku. Kutoka na kuwa na kazi nyingi mchana hakupata nafasi ya kwenda kufanya mazoezi ya uimbaji na wenzake. Emanuel akatafuta namna atakavyoweza kutekeleza dhamira yake ya kuimba na siku moja awe miongoni mwa watu wanaong’ara katika anga za muziki na hatimaye kuwa na pesa za kuweza kujitegemea kama sio tajiri. Ilimlazimu Emanuel kutafuta muda zaidi ya mchana, akawa anatoroka usiku kwenda kufanya mazoezi na rafiki zake.

“Usiku mmoja nilipokuwa nimetoroka kwenda kwenye mazoezi ya uimbaji mwenyeji wangu akajua sipo, akafunga geti nyuma baada ya mimi kutoka” anaeleza Bwana Emanuel. Kurudi nyumbani asubuhi Emanuel anakumbana na geti lilofungwa.  Tajiri wa Emanuel alimwachisha kazi mara tu ya Emanuel Kufunguliwa geti kuingia ndani. Tajiri wake anampa masaa mawili awe amechukua kilicho chake na kuondoka kwenye viwanja vya mji wake. Mwenyeji wa Emanuel aliogopa kuwa huenda Emanuel akitoka usiku alikuwa akijihusisha na vitendo vya kijambazi.  Alimkabidhi shilingi elfu sabini ikiwa sehemu ya mishahara yake ya kufanya kazi, pesa ilikuwa inatosha kumrejesha mpaka nyumbani Makete.

Badala ya kwenda kijijini “Hata Hivyo sikwenda kituo cha mabasi Ubungo kunakopatikana usafiri wa kwenda Makete, niliamua kwenda kivukoni kuchukua usafiri wa Zanzibar kwasababu rafiki zangu walikuwa na safari ya kwenda kufanya onyesho Zanzibar”  . Emanuel alifika Zanzibar kwa kuchelewa rafiki zake walikuwa wameshamaliza tamasha na hawakuweza kumsubiri wakawa wamechukua boti ya kurudi bara.  Emanuel anafanya kosa la msingi badala ya kugeuza mara moja anakaa afurahie uzuri wa Zanzibar kidogo, anajikuta anamaliza pesa yote aliyokuwa amebakiwa nayo pale Rambo Motel alipofikia kisiwani Zanzibar.

Emanuel anashukuru kwani kabla ya kuishiwa mpaka nauli anaweza kurudi bara, anakofika mchana anaanza mara moja kuwatafuta rafiki zake maana muda huo alikuwa  hana kwa kula wa kulala, anapigwa na mshangao kuona jamaa zake hawapo Dar Es Salaama wanamtaarifu kuwa wapo Mwanza kushiriki kwenye onesho. Inamlazimu emanuel kutafuta kazi ili aweze kujikimu mpaka rafiki zake warudi. Baadaye anapata kazi ya muda kwa dada mmoja, anaye mpa chakula na mahali pa kuishi katika nyumba yake. Emanuel anaishi na huyu dada asiye na mume na baadaye wanaingia kwenye uhusiano na kushiriki ngono zembe. “Nimekaa naye miezi sita mpaka nilipopata habari za kufariki kwa mama yangu kijijini” anaeleza Emanuel kisha kilichomfany aachane na huyu dada. Baada ya kupokea taarifa za kufariki kwa mama yake Emanuel kwa kusaidiwa na mwenyeji wake wanatafuta nauli ya kumrudisha nyumbani, ambako yupo mpaka leo.

Alipoulizwa kama hana wasi wasi wa kuwa hana maambukizi ya UKIMWI kutokana na uhusiano wake Emanuel anasema kuwa amekuwa siku zote akihisi labda aliambukizwa na angependa kupima afya ili aweze kujitambua kama ameathirika au la. Alisema ameshindwa kupata huduma ya kupima kwani huduma ya hii inapatikana mbali mpaka hospitali ya Bulongwa ambayo bado mtu hana uhakika kama utapata huduma ukitembea umbali wote kuifuata.

Alipohojiwa uwezekano wa maambukizi Mganga wa PIUMA , Juma Nzige akiongea namtandao huu anasema vijana wengi wapo kwenye nafasi kubwa ya kuambukizwa maambukizi ya VVU kutokana na kutokuweza kuachana na ngono, au kuwa waaminifu au kutumia kinga. 

Akieleza upatikanaji wa huduma ya upimaji karibu na watu,  Bw. Nzige anasema shirika lake limejitahidi kusogeza huduma ya upimaji karibu na walengwa vijijini ili vijana kama Emanuel wanaoshindwa kuifuata huduma hiyo waipate. “Kama serikali ingeweka huduma za klinik inayotembea au kusaidia mashirika katika upimaji na utoaji wa dawa za ARV tungeweza kuwafikia watu wengi zaidi kuliko tunavyofanya sasa” anamalizia Juma Nzige.

Mwenyekiti wa kitongoji anapotokea Bw. Emanuel Bw. Mchaga aliuambia mtandao huu tatizo la vijana kuhamia mijini lina sura mbili. Sehemu moja ni ya kuwalaumu vijana wenyewe kwa kutokupenda shughuri za kilimo na kuishi kijijini wakifikiri wakienda mjini watapata kazi na maisha rahisi zaidi. Lakini pia anaitaka serikali na jamii kutoa msaada  zaidi wa kijamii na kiuchumi kwa vijana hasa baada ya kumaliza elimu zao ili waweze kuyakubali maisha ya kijijini.

Wilaya ya makete ni miongoni mwa wilaya zenye tatizo kubwa la uhamaji wa watu kutoka wilayani humo kwenda mijini kutafuta kazi pamoja na kuwa na maliasili nyingi kama za miti na aridhi nzuri yenye kustawisha mazao mengi na mvua zinazonyesha sehemu kubwa ya mwaka. 

July 15th, 2009

Get tested and have a brand new T-shirts!!

PIUMA MOBILE VCT-to date

By Juma.

Today the PIUMA mobile VCT has been scheduled at MAFIGA, 30km from Bulongwa areas…During the session discipline of counselling skills has been employed

Out of 22 individuals counselled and tested there’s only one new client been HIV positive.PIUMA   t-shirts has also advertized and 17 pcs been sold.

...Get tested..

...Get tested..

...have a T-shirt at a reasonable price..

...have a T-shirt at a reasonable price..

 

..and shine...

..and shine...

Woman with development..during testing....

Woman with development..during testing....

July 5th, 2009

BARUA

Barua kutoka kwa Daktari.

Hivi karibuni nimesikia kwamba watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI ambao wanatumia dawa za kufubaza VVU wanachanganyikiwa juu ya suala la unywaji wa pombe / kileo wakati wanatumia dawa hizo. 

Nataka kuwasaidia na ntatumaini kwamba nitaweza kuondoa hofu hiyo ili kuwasaidia kuimarisha afya zenu na kurefusha maisha yenu. 

Mara nyingi imekuwa ikisemwa kwamba siyo vizuri kutumia dawa za kufubaza VVU na kunywa pombe wakati huo huo.  Ninyi wote mmeambiwa kamwe msiguse pombe mnapotumia dawa hizo zinazookoa maisha yenu! 

Sasa ? msikilizeni daktari wenu na watu wanaowapenda na kuwajali kwa dhati.  Mtawafahamu kwa kuwa hawatawatisha na wala hawatawafanya mjisikie vibaya.

Kwanza, ni dhahiri kwamba ni VEMA kwa afya yako KUTOKUNYWA (pombe) au kutumia dawa za kulevya wakati unatumia matibabu hayo.  Kutokana na uzoefu wenu mnajua kwamba ukinywa pombe nyingi unachoka na unasahau muda na majukumu yako au wajibu wako.   Katika hali hii unaweza kusahau kunywa dawa zako kwa wakati muafaka au unaweza kutokunywa dawa hizo kabisa. 

Dawa zote zinalenga kukufanya uwe na afya nzuri na hivyo unapewa katika utaratibu fulani na kwa namna nzuri sana.  Pombe inakufanya ubadili utaratibu huu na hii ni hatari kwa afya yako.  Tumia dawa hizo kama unavyoagiza, na kamwe usibadilishe utaratibu huo. 

Pili, Pombe yenyewe siyo nzuri kwa afya yako kama unakunywa sana na hasa inaweza kuleta madhara kwa ini lako katika kipindi cha miaka kadhaa.  Watu wanaoishi na VVU ? hata wengine ? wana virusi vingine (virusi vya Hepatitis) ambavyo vinashambulia ini.  Na hakuna vipimo vya maradhi hayo Bulongwa.  

 Kama umeambukizwa na virusi hivyo na pia una VVU madhara kwenye ini  yataongezeka ukitumia Pombe.  Kwa hiyo nitapendezwa zaidi endapo hutakunywa pombe sana!

 LAKINI KAMA UNAKUNYWA POMBE na unafurahi sana:

BADO ? KUNYWA DAWA KWA WAKATI MUAFAKA kama ulivyoagizwa na daktari na kamwe usibadilishe ratiba ya kunywa dawa hizo.  Hii ina maanisha kwa mfano:  Kama unakunywa TRIOMUNE  -  kula kidonge kimoja asubuhi na kidonge kimoja jioni katika muda ule ule!

Usisahau:  Haya yote ni kwa ajili ya afya yako na maarifa yako.  Hakuna mtu mwenye haki ya kukunyima dawa au kukutisha? iwe daktari, muuguzi, afisa wa serikali au mtu yeyote kutoka katika kanisa au mganga wa kienyeji mwenye haki ya kufanya hivyo.  Kama unatumia dawa hizo kila mara, na kama matabibu wanafuatilia tiba yako vizuri, ni vema kula dawa hizo ? hata kama unakunywa pombe! 

Kumbuka:  Ni bora kutokunywa pombe wala kufanya ngono. kama huwezi kujizuia kufanya ngono!kunywa dawa zako  na utumie Kondomu!

Nakutakieni maisha mema yasiyo na uwoga!  Na endapo una swali lolote ?  muulizeni daktari katika ofisi za PIUMA!  Tupo hapo kwa ajili yenu na mnaweza kupata ushauri kutoka duniani kote!!”

(Translated from english)

Dr Rainer Brandl  MD,MTMH. 

Dr. Rainer Brandl mwenye suti nyeusi na miwani kushoto akimpa maelezo Mh. Rais Jakaya Kikwete ya mashine ya kupima CD4 ya Cyflow_SL3 mali ya PIUMA wilayani Makete. Mashine za Cyflow hutengenezwa na kampuni ya PARTEC ya Ujerumani